Mtakufa malofa na moto mtauingia kwa kuendekeza mpira

Umesema kweli.Angalia tangu mechi ya Yanga jana nguvu kazi kiasi gani na pesa zimepotea kujadili ujinga.
 
Ahsanteeeee umefikisha na Allah s.w shuhuda
 
Mtoa mada unataka kupangia watu cha kufanya, na wakati hata wewe mwenyewe maisha yako hayana tofauti na hao wanaojadili muda wote masuala ya michezo!

Acha ukuda wa kijinga, na ujifunze kuishi maisha yako.
Si shaka umri wako ni mdogo sana au ni mtu wa vijiweni vijiweni
 
 
Hivi, kila ukipita mitaani kwa watu jobless na wengine wenye kazi tu za maana, ukihesabu muda wanatumia kubishana juu ya mpira aisee unaona wazi kabisa Kuna hatari ya kiuchumi baadae, imagine mimi leo hii tar 8/10/2023 jioni hii, kwa sababu ya mapumziko nimepita kwenye kijiwe cha kahawa, kupata mawazo tofauti kwa watu tofauti, lakini nimefika hapa around 18:20pm na sasa ni 19:48pm watu wanabishana kuhusu mpira toka nimefika.

Msikatae, Kuna hatari ktk maendeleo kwa kuendekeza vitu visivyo walipa watu kuchukua muda wao kupita kiasi na hawaingizi chochote
 
Umesema mapumziko eehh basi na hao wanaobishananmpira wapo mapumziko
 
Vipi,badala ya kuleta sadaka wao wanapeleka viingilio vibanda umiza?

Sitisha na komesha mchezo wa mpira wa miguu haraka maana sadaka imepungua sana.
 
Vipi,badala ya kuleta sadaka wao wanapeleka viingilio vibanda umiza?

Sitisha na komesha mchezo wa mpira wa miguu haraka maana sadaka imepungua sana.
Sadaka misikitini imepungua kweli.Sijui huko makanisani.Hawa mamlaka ya mapato wanakandamiza wafanyabiashara wadogo lakini kwenye mpira wanaachia tu.Ndio maana huu upuuzi kila siku unapaa tu.Siku tukielemewa na madhara yake itakuwa tumechelewa.
 
Sadaka misikitini imepungua kweli.Sijui huko makanisani.Hawa mamlaka ya mapato wanakandamiza wafanyabiashara wadogo lakini kwenye mpira wanaachia tu.Ndio maana huu upuuzi kila siku unapaa tu.Siku tukielemewa na madhara yake itakuwa tumechelewa.
Vp na wewe ukiweka kibanda umiza hautapata hizo fedha badala ya kusubiria uletewe huko kanisani au msikitini?
 
Ipo siku serikali itazinduka japo kwa kuchelewa ifunge viwanja vya mpira watu wakalime.Nchi ina ardhi bora ya kilimo kwa dunia nzima halafu tunaagiza ngano Ukraine.Vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa wanahemkwa tu halafu wanakwenda kutafuta chips zilizochomwa mabarabarani.Wengi wao hawana wake kwa vile hawana nguvu za kiume.Zimepotea kwa kupiga makele kuhusiana na mpira.Hamu ya kuwa na mke nayo inachukuliwa na mawazo ya mpira jioni,kesho na keshokutwa au mwezi ujao.
 
Juzi nimetoka achisha mtu kazi kwa upumbavu wa kuaga kuwa anauguliwa na shangazi yake na kumbe alikuwa anasafiri kwenda kuishangilia timu huko Dar, alipopata ajali ndio akaniambia ukweli.

Huu ni zaidi ya uzwazwa.
Hahaha anapata kazi nyingine na anaendeleza ushabiki. Punguza makasiriko boss milazo
 
mkuu uliona mbali.
 
Timu Mbovu zilizofungwa na Yanga Msimu huu 2023/2024 mpaka sasa;

1. KMC - Goli 5
2. JKT Tanzania - Goli 5
3. AZAM - Goli 3
4. SIMBA - Goli 5
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…