Mtanda fuatilia kwa karibu mradi wa jengo la uwanja wa ndege la kimataifa Mwanza, limesimama tena

Mtanda fuatilia kwa karibu mradi wa jengo la uwanja wa ndege la kimataifa Mwanza, limesimama tena

Umeangalia mkataba wa ujenzi inasemaje? Au umekimbilia kwa Mtanda bila kusema kama kuna sehemu ametajwa ndani ya mkataba? Watu kama nyie ndo wanasababisha kuaribika kwa kazi.
suala siyo kutajwa kwani ile miradi mingine anayotembelea ametajwa kwenye mikataba kumbuka huyu ni political commissar wa mkoa vinginevyo, tuambieni Mhandisi Mshauri tumfuatilie tujue kulikoni.
 
Umeangalia mkataba wa ujenzi inasemaje? Au umekimbilia kwa Mtanda bila kusema kama kuna sehemu ametajwa ndani ya mkataba? Watu kama nyie ndo wanasababisha kuaribika kwa kazi.
Suala siyo RC kutajwa kwenye mkataba kwani kule kwenye Soko,Meli nk anapotembelea na kukagua maendeleo ya miradi ametajwa kwenye mikataba,huyu ni Political Commissar wa mkoa na mwakilishi wa Rais mkoani ni jukumu lake kufuatilia miradi yote na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa ujumla. Vinginevyo tuambieni Mhandisi Mshauri wa mradi huu wa airport ni nani tumpime.
 
Mwanza haina abiria wengi wanaoweza kusababisha kujengwa international airport. Hakuna shughuli za kimataifa kama Arusha, Dar, Dodoma. Mnataka international airport ya nini?
jiji la pili kiuchumi likose shughuli, uelewa wako mdogo
 
Hii orodha umeitoa wapi? Weka chanzo cha taarifa hii tuione wenyewe.

Kwa hiyo kwa kigezo hiki Arusha (ARK) inastahili kuwa International Airport, lakini Mwanza haistahili kwa kuwa haina kigezo hicho?

Ukweli ni huu, pamoja na Arusha kuwa na mkao ya Jumuia ya Afrika Mashariki, mji huo hautakuwa tofauti sana na miji kama Washington D.C., kubaki tu na sifa hiyo ya kuwa makao makuu; lakini kiuchumi haitakwenda mbali sana.
Abiria 800000 kwa Mwaka Mwanza Airport bado haistahili kuwa MIA
 
Abiria 800000 kwa Mwaka Mwanza Airport bado haistahili kuwa MIA
Mbona unatanguliza mkokoteni na punda anabaki nyuma? Unakielewa unachozungumzia hapa?
KIA ilipojengwa kulikuwa na abiria wangapi kwa mwaka? Zanzibar ina abiria wangapi?
Moi international kule jirani, inao abiria wangapi? Eldoret, Kisumu; Kigali, Bujumbura, n.k., n.k.

Unataka ujenge International airport ya kuhudumia abiria milioni moja, wakishafikia hiyo milioni ndani ya miaka miwili, utafanya nini, utaanza kujenga upya uwanja wa kuhudumia zaidi ya hao milioni moja?
Kwa Mwanza, ndani ya miaka mitano ijayo, milioni mbili hata tatu kwa mwaka itakuwa ni kidogo sana.
 
KIA ilijengwa ikiwa na abiria 300000 tu kwa Mwaka sembuse kwa Mwanza ndege 7 kwa siku angalia Strategic location ya jiji, je Uwanja wa Dodoma una abiria wangapi lakini msalato inajengwa.Kuna vigezo vingi vya ICAO kujenga uwanja wa kimataifa mahala, hii ni pamoja na mahitaji ya kiuchumi,siyo Idadi tu ya abiria. Mwanza imecheleweshwa mno tena kisiasa tu, kwa sasa uamuzi ulikwisha pitishwa mpaka kwenye ilani ya uchaguzi,watu wanafuatilia.
 
Sasa hapo Mwanza international international airport ya nini? Walikimbilia kujenga Songwe international airport zaidi ya miaka 10 iliyopita lakini umewahi kusikia ikifanya international flights? Hakuna sababu ya maana ya kuwa na international airport Mwanza.
Mwanza aiport huwezi kulinganisha na uwanja mdogo wa Songwe,wenye abiria 150000 kwa Mwaka Mwanza inakimbilia 800000 kwa mwaka.
 
Mwanza aiport huwezi kulinganisha na uwanja mdogo wa Songwe,wenye abiria 150000 kwa Mwaka Mwanza inakimbilia 800000 kwa mwaka.
Achana na huyo mjinga, ameshavuta bangi zake hapo ukichananganya na chuki za kikanda akija hawezi kukupa logical argument yoyote zaidi ya kuandika uharo tu wa kuokoteza huko google
 
KIA ilijengwa ikiwa na abiria 300000 tu kwa Mwaka sembuse kwa Mwanza ndege 7 kwa siku angalia Strategic location ya jiji, je Uwanja wa Dodoma una abiria wangapi lakini msalato inajengwa.Kuna vigezo vingi vya ICAO kujenga uwanja wa kimataifa mahala, hii ni pamoja na mahitaji ya kiuchumi,siyo Idadi tu ya abiria. Mwanza imecheleweshwa mno tena kisiasa tu, kwa sasa uamuzi ulikwisha pitishwa mpaka kwenye ilani ya uchaguzi,watu wanafuatilia.
Naona hujui hata unachozungumzia, maana unajipinga mwenyewe kama hujui.

Haya, tufahamishe hivyo vigezo vya ICAO ambavyo Mwanza haina, lakini KIA ikawa navyo, na Msalato ikawa navyo.

Sasa unageuka tena unasema" Mwanza imecheleweshwa mno"! Sasa kama imecheleweshwa ndiyo iwe sababu ya kuzuia kuwa na vigezo vya ICAO unavyovisema bila kuvitaja?
KIA ilijengwa ikiwa na abiria 300000 tu kwa Mwaka sembuse kwa Mwanza ndege 7 kwa siku angalia Strategic location ya jiji
Inawezekana wewe unaandika humu ukiwa umelewa, au huna uelewa tu wa unacho andika!
 
Mwanza aiport huwezi kulinganisha na uwanja mdogo wa Songwe,wenye abiria 150000 kwa Mwaka Mwanza inakimbilia 800000 kwa mwaka.
Hata wakifikia abiria 10M sio hoja ya kuwa na intrernational airport kama hao abiria ni domestic. Tunahitaji kuwa na international passengers wengi kuwa na international airport. Kwasasa bado Mwanza haifai kuwa na international airport, only K"Njaro, Dar na Znz.
 
Abiria international utawapataje bila uwanja wa ndege kuwa international,ebu tubadilike, kwani Dodoma kuna international pax pale kupelekea kujenga Msalato ebu tuache ubaguzi wa kimaendeleo. Hivi Mussa wa TAA ni mtu wa wapi?
 
Tuwe makini tusijenge viwanja kama vile kule Chato ambako sasa kiwanja cha ndege kinatumika kuanikia mpunga kwasababu tu watu wanafikiri kuwa na international airport ni sifa. JPM alifanya mambo kwa sifa na kuishia kusababishia nchi hasara kubwa kubwa. Songwe international airport ilijengwa kwa mashinikizo ya wanasiasa wa Mbeya, leo hii hata domestic flights hazitoshi pale Songwe. Ukweli ni kwamba Mwanza itakuwa regional airport kufeed abiria K"Njaro, Dar au Zanzibar na huko ndio safari za kimataifa zinafanyika.
 
Hivi kitu kinajengwa Mwanza jitu linatoka huko kupinga.
Mwanza ndio katikati ya UKanda ya Afrika mashariki kuna Warundi,Wanyarwanda,Waganda,Wakenya na Wakongo ambao wameshakuwa kama makabila ya kanda ya ziwa kwahiyo wanastahili uwanja zaidi ya huo unaojengwa.
 
Dah ila hii nchi tunachelewashana wenyewe Centralization haijawahi kulitoa taifa Lazima tujifunze Decentralisation ili tuongeze base ya Mapato yetu na kusogeza Huduma kwa Wananchi yaani kweli unaona ni sawa minofu ya samaki kusafirishwa kupitia Entebe na Nairobi kwa hoja tu tuendelee kufeed KIA na JKA, Ni mara ngapi watanzania wanataifishwa Dhahabu hapo Kenya kwasababu tu ya kutafuta International Flight, Umeng'ang'ania Idadi ya Abilia wa kimataifa umefanya research ukajua ni abiria wangapi wanafanya International Flight kutokea Mwanza, Kwa kifupi tu International Airport ndo kwanza inajengwa ndege kumi za kimataifa zimeshaomba kuutumia huu uwanja.
 
Kuna Wafanyabiashara wangapi wanaenda nje kutokea Mwanza na mikoa ya kanda ya ziwa, Vip je Kampuni za Madini zenye Foreigners kama Capital Drilling, Scandinavian, Buzwagi, Geita Gold, na Mgodi mwingine unataka kuanza Nyanzaga, Usafirishaji wa Bidhaa zitokazo ukanda huu kama Samaki, Bondo, Dhahabu achilia mbali utalii ambao nao haupo Nyuma, Punguzeni hofu Tanzania ni kubwa acha tuijenge sote na Kate dhana ya wale wanastaili kuliko hawa tuiache hata Songwe upewe full operation Walau kila kanda kuwe na International Flight hii italiongezea taifa base ya makusanyo yake ya mapato lakini pia kusogeza huduma karibu International Flight sio kwa ajili ya utalii peke yake
 
Hata wakifikia abiria 10M sio hoja ya kuwa na intrernational airport kama hao abiria ni domestic. Tunahitaji kuwa na international passengers wengi kuwa na international airport. Kwasasa bado Mwanza haifai kuwa na international airport, only K"Njaro, Dar na Znz.
'Concept' ya International Airport kwako ni mchana na usiku kabisa.
Utakuwaje na abiria 10 milioni watumie uwanja, halafu kati ya hao wasiwemo wasafiri wa nje?
Hao milioni kumi, wao hawasafiri kwenda nje ya nchi, ni watu wa humo humo tu ndani?

Wewe vipi 'fazil' mbona unajitoa ufahamu kiasi hicho? Unayo maslahi yapi katika haya maswala? Mwanza kuwa na 'International Airport sasa siyo swala tena la kujadiliwa; ni 'fact' usiyoweza kuizuia.
Kumekuwepo na mchezo mchafu sana kwa muda mrefu toka kwa watu kama wewe. Hili sasa ni lazima likomeshwe.
 
Ukweli ni kwamba Mwanza itakuwa regional airport kufeed abiria K"Njaro, Dar au Zanzibar na huko ndio safari za kimataifa zinafanyika.
Utaumia sana, kwa sababu huwezi kuizuia Mwanza kuchukuwa nafasi yake.
Kwa nini Zanzibar isiwe na hadhi hiyo unayoizungumzia wewe 'Regional Airport' ku-feed Dar na Mombasa, na Nairobi!; na kwa hali hiyo hiyo, kwa nini KIA isiwe 'feeder ya Mwanza International Airport? Toka Mwanza kwenda hapo KIA ni mwendo mfupi tu? Mwanza itatumia hadhi ya Jiji lake na kuwa 'hub' ya ukanda wote wa ziwa na nchi jirani. Abiria toka nje, badala ya kwenda porini KIA wanafikia JIJINI, halafu wanasambazwa kwenda maeneo mengine ikiwemo KIA.
"Ukweli" kwako usiulazimishe kuwa ndio ukweli na kwa wengine.
 
Mnatamani tu viwanja vya kimataifa bila kujua kwanini. JPM alifanya ujinga huo kuingiza nchi hasara ya mabilioni kujenga international airport Chato na ku-fosi marais wa Uganda na Kenya kuja moja kwa moja na kutua kijijini kwake Chato! Hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza na mwisho kwa Chato kutua ndege kutoka nje na hata za ndani zinatua moja kwa mwezi. Ni kutojua mambo kwa hali ya juu kutaka Mwanza iwe international airport wakati hakuna international passengers wa kutosha kufanya hivyo. Mnafikiri viwanja vya ndege ni kwa ajili ya maonesho au sifa za kijinga? Zanzibar ni semi-autonomous state, wana watalii kibao wanatua kule na kuondoka kwenda Ulaya moja kwa moja. Rais wa Zanzibar alikuwa Arusha wiki iliyopita akifanya maongezi ya kuweka ushirikiano kati ya Zanzibar na Arusha kwenye mambo ya utalii kwani watalii wakitoka Arusha huenda Zanzibar. Uwanja wa ndege wa Arusha upo bize mara tano ya Mwanza, unafikiri ni uwanja upi unapaswa kuwa wa kimataifa?
 
'Concept' ya International Airport kwako ni mchana na usiku kabisa.
Utakuwaje na abiria 10 milioni watumie uwanja, halafu kati ya hao wasiwemo wasafiri wa nje?
Hao milioni kumi, wao hawasafiri kwenda nje ya nchi, ni watu wa humo humo tu ndani?

Wewe vipi 'fazil' mbona unajitoa ufahamu kiasi hicho? Unayo maslahi yapi katika haya maswala? Mwanza kuwa na 'International Airport sasa siyo swala tena la kujadiliwa; ni 'fact' usiyoweza kuizuia.
Kumekuwepo na mchezo mchafu sana kwa muda mrefu toka kwa watu kama wewe. Hili sasa ni lazima likomeshwe.
Kwa kanda ya ziwa tumeona jinsi Chato International Airport inavyotumika kuanikia mipunga sasa mnataka kuanika nini hapo Mwanza airport, sangara? Subirini bado sana, labda sasa tuwe na Arusha International Airport manake kuna watalii wanataka kutua moja kwa moja Arusha kutoka nje.
 
Mnatamani tu viwanja vya kimataifa bila kujua kwanini. JPM alifanya ujinga huo kuingiza nchi hasara ya mabilioni kujenga international airport Chato na ku-fosi marais wa Uganda na Kenya kuja moja kwa moja na kutua kijijini kwake Chato! Hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza na mwisho kwa Chato kutua ndege kutoka nje na hata za ndani zinatua moja kwa mwezi
Kwa hiyo, kwa uelewa wako, Chato ndio mfano halisi wa kuilinganisha na Mwanza! Mbona unajivisha ujuha waziwazi hivi?
kibao wanatua kule na kuondoka kwenda Ulaya moja kwa moja. Rais wa Zanzibar alikuwa Arusha wiki iliyopita akifanya maongezi ya kuweka ushirikiano kati ya Zanzibar na Arusha kwenye mambo ya utalii kwani watalii wakitoka Arusha huenda Zanzibar. Uwanja wa ndege wa Arusha upo bize mara tano ya Mwanza, unafikiri ni uwanja upi unapaswa kuwa wa kimataifa?
"Watalii wa Zanzibar" wakiondokea Dar es Salaam hawafiki ulaya? Wanaotua Nairobi na kwenda mahala kwingine hawatoki na kufika Ulaya?

Umekwisha ambiwa mara kadhaa humu, kwamba viwanja vya ndege havipo kwa ajili ya utalii pekee, lakini wewe hilo ndilo jambo pekee unalolishikilia, kwa sababu hujui mengine yote.

Nilikupa mfano mmoja wa kule Marekani, uwanja wenye wasafiri wengi zaidi duniani, uliopo Atlanta, Georgia, Hartfield-Jackson, Georgia kuna utalii gani huko, unajua?

Ukweli ni kwamba huna unalojuwa katika maswala haya ya usafiri wa ndege, kinachokuumiza tu roho ni kudhani kwamba uwepo wa Mwanza utaiondolea au ipunguzia sifa Arusha. Lakini ukweli ni kwamba, wewe, pamoja na wengine wote waliokuwa na mategemeo ya kuifanya Mwanza kutotumia nafasi yake kikamilifu, matumaini yenu hayo hayaendi popote. Mwanza itashamiri na itachukuwa nafasi yake katika miji mashuhuri, siyo hapa Tanzania pekee, bali duniani kote.
Hili halizuiliki kwa hila zozote.
 
Back
Top Bottom