Mtandano wa vikundi vya wakulima na Wafugaji Mkoa wa Arusha, Waandaa tuzo za waandishi wa habari kwenye mfumo endelevu wa chakula na kilimo ikolojia

Mtandano wa vikundi vya wakulima na Wafugaji Mkoa wa Arusha, Waandaa tuzo za waandishi wa habari kwenye mfumo endelevu wa chakula na kilimo ikolojia

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Mtandano wa vikundi vya wakulima na Wafugaji Mkoa wa Arusha (MVIWAARUSHA), Waandaa tuzo za waandishi wa habari kwenye mfumo endelevu wa chakula na kilimo ikolojia, zenye lengo la kutambua na kusherehekea uandishi wa habari uliotukuka kwenye masuala muhimu yanayohusiana na kilimo endelevu, usalama wa chakula, na uendelevu wa mifumo ya chakula.

Tuzo hizi zinalenga kuhamasisha ubora katika uandishi wa habari, kuhimiza ufuatiliaji wa kina kuhusu mbinu za kilimo cha kiikolojia, na kuongeza uelewa wa umma kuhusu umuhimu wa mifumo endelevu ya chakula mbele ya changamoto za mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la idadi ya watu.
Screenshot_20241114_180554_Word.jpg

MVIWAARUSHA kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo IDP na CARI wameandaa tuzo za umahiri wa uandishi wa habari za mfumo endelevu wa chakula na kilimo ikolojia kwa mwaka 2024 kama chachu kwa wanahabari kushughulikia masuala ya usalama wa chakula na kilimo ikolojia.

Tuzo hizo zitakazo fanyika wiki ya kwanza ya mwezi wa pili jijini Arusha zina lenga kuimarisha uelewa juu ya masuala ya mfumo endelevu wa chakula na kilimo ikolojia kwa waandishi wa Habari na uma kwa ujumla.

Akisoma taarifa hiyo kwa waandishi wa Habari, Katibu wa kamati ya maandalizi ya tuzo hizo ambaye pia ni afisa Habari wa taasisi hiyo Ndg. Imani Hezron amesema taasisi hizo zimechukua hatua hiyo mara baada ya kutoa mafunzo kwa waandishi wa Habari, wamiliki wa vyombo vya Habari Pamoja na wahariri juu ya masuala ya mifumo endelevu ya usalama wa chakula na kilimo ikolojia , hivyo tuzo hizi ni sehemu ya kutambua jitihada zao ikiwa ni Pamoja na kuwapa hamasa ya kuendelea kuandika juu ya masuala ya mifumo endelevu ya chakula na kilimo ikolojia.

Tuzo hizo zina Nyanja mbalimbali za ushindani ikiwemo;

1. Mwandishi bora alyeripoti masuala ya kilimo anuai (reporting on Agrobiodiversity/Agroecology)

2. Makala bora ya mfumo wa mbegu za asili (Best Feature on Traditional Seed Systems).

3. Habari bora inayohusu kilimo stahimilivu kwa mabadiliko ya tabia nchi (Best Story on Climate Resilience in Agriculture).

Waandishi washindani kwenye Nyanja hizo watakuwa na nafasi ya kuwasilisha Makala, na habari zao kuanzia sasa hadi tarehe 28, novemba 2024. Hii ikiwa ni kutoa muda kwa majaji kuchanganua na kupata washindi.

Akitoa ufafanuzi wa tuzo hizo Afisa program wa MVIWAARUSHA ndg. Damian Sulumo, amesema wapo wanahabari ambao hawakupata fursa ya kushiriki mafunzo lakini wamekuwa wakishiriki kwenye kuandaa Makala na kuandika juu ya mfumo endelevu wa chakula na kilimo ikolojia, watapata fursa ya kutuma kazi zao na kupitiwa na majaji.

Jinsi ya kutuma kazi:

damian.sulumo@mviwaarusha.or.tz

richard.masandika@mviwaarusha.or.tz

copy

erimelinda.temba@tz.ilesdepaix.org na Imani.hezron@mviwaarusha.or.tz
IMG_20241114_180058_256.jpg
IMG_20241114_180055_248.jpg
IMG_20241114_180053_632.jpg
IMG_20241114_180051_261.jpg
IMG_20241114_180049_556.jpg
IMG_20241114_180046_899.jpg
 
Back
Top Bottom