Mtandao wa Alibaba una magari ya bei nafuu sana, Sijajua ushuru wake kuyaingiza nchini

Mapank

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
4,130
Reaction score
6,097
Nimepitia mtandao wa Alibaba, naona kuna magari ya bei nafuu sana kuliko mitandao ya magari tuliyoizoea, Na kuna magari mengi ya umeme ya chini ya 5M Tzs, Sijajua ni kuna mlolongo upi wa manunuzi na masuala ya tax clearance kwenye bisahara ya magari huko Alibaba mpaka watu wanakomaa na mitandao ya beforward, Car junction, SBT Japan na sio hapa Alibaba,

Mfano wa bei na magari kwenye mtandao wa Alibaba



 
Wajuzi wa mambo si mseme namna kodi zilivyo huko alibaba
 
Sio nongwa
No roho mbaya
Kweli Kaka ni roho mbaya tu, Mjapan hana hata shida anakutupia tu gari kwa bei ya kutupa na wala hajui kuna kitu kinaitwa uchakavu, Kwa ujinga wetu tunampa hela ya kuthaminisha gari lake uchakazu, halafu tunalinunua, Hana taabu.
Mswahili sasa, ameona ndio mahali pa kuvuna pesa, eti na yeye anazungumzia uchakavu wakati Magari kibao yako mtaani zaidi ya Miaka 20 hapa hapa Bongo!!
Huyu ndio Mwafrika.
 
Wajuzi wa mambo si mseme namna kodi zilivyo huko alibaba
Hapo bado transport cost huo ni ushuru tu, ujaongeza bei ya gari
 
Tunaoishi kwenye hii nchi tuna moyo sana
 
hata mm hawa jamaa walinishangaaza.
Hata simu zao android version kubwa,RAM kubwa,internal storage km yote eti laki na ishirin sijajua hawa jamaa business wanaendeshaje.
 
Iyo gari milioni 4 au 0 imejificha? @Mwl.RCT

Tunakuomba huku?
 
hizo unaziona hapo zimewekwa kwa mnada the last bidder anachukua mzigo,
hiyo bei nyingi ni ile ya wa mwisho aliyeweka dau,
hata amazon wanafanya hiyo kitu,
ila kwa ushauri ukitaka gari nunua moja kwa moja kupitia platform sahihi zinazojihusisha na magari tu,
ukitaka kuamini ingia site zingine zinazouza magari utakutana na bei za juu kuzidi hizo
 
Hizi bei ni za kawaida tu, kama SBT au TCV. Unapoona ameweka range ya bei basi wewe utauziwa kwa hizo bei za kulia (kubwa), labda uwe sijui unachukua magari mangapi ndo upewe kwa bei za kushoto (ndogo).

By the way huko Alibaba kuna matapeli wanaouza PS5 mpaka Kwa $150, tena unaambiwa buy 2, get 1 extra free ila sasa ukilipa tu unakula block so sio pa kupaamini Sana.
 
Hahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…