Mtandao wa Quora unawezekana ukawa sababu ya wakristo wengi wa Ulaya kusilimu na kuwa Waislamu

Mtandao wa Quora unawezekana ukawa sababu ya wakristo wengi wa Ulaya kusilimu na kuwa Waislamu

Kijana utaendelea kuonekana kituko, hizo hadithi hazionyeshi ya kuwa watu hawaingii katika Uislamu au hawaukubali au hawashawishiki na Uislamu.

1. Hadithi ya kwanza inaelezea namna Uislamu ulivyo anza kuingia ulikuwa unaonekana ni kitu kipya yaani mgeni, na utarudi ukiwa katika hali hiyo hiyo ya ugeni kama ulivyoanza. Kisha Mtume akasema bishara njema kwa wale watakao onekana wageni, hii inamaanisha ya kuwa hao ndiyo watakuwa sahihi, leo hii Waislamu wako wengi lakini hawaufati ule uislamu sahihi na wale wanao ufata wanaonekana kuwa wameleta dini mpya na hii ndiyo maana ya Hadithi.

Lakini katika mapokezi mengine anasema mtume ya kuwa, hao watakao onekana wageni ni kwa sababu wanatengeneza yale ambayo wameyaharibu watu.

2. Hadithi ya pili inaonyesha zama za mwisho zinapokaribia watu watakuwa na imani haba, na imani itarudi kule ilipoanzia.

3. Hadithi ya tatu ina maana sawa na hadithi ya kwanza.

Sasa hoja yako hapo iko wapi kijana ? Mpaka najiuliza kwanini umetumia hadithi hizi ambazo ziko dhidi yako, ila nahitimisha ni kwa ujinga wako.
Kazi yangu ni kukuonesha uislamu utarudi pangoni kama nyoka na uta shrinks
“Faith will shrink back to Medina as a snake shrinks back to its hole.” (Bukhari and Muslim.) Mishkat al-Masabih 160
 
Sipo tayari kupoteza muda kubishana na wewe, mimi nimeleta taarifa iliyohakikiwa nimemaliza. Kama unazani ni utani watume ndugu zako waislam waende Italy kama wahamiaji watakupa mrejesho kamili.
Hakuna uhusiano wa akili na imani. Na kwa taarifa yako akili yako ni ndogo saana kuelewa mambo ya imani haswa ya kikristo.
Ni sawa na kipofu kukubishia kuwa hakuna rangi nyekundu kwa kuwa hukumuelewesha rangi nyekundu inafananaje.
Mungu ana mtoto ambaye ni Yesu Kristo. Alimpataje ndio hayo ya kujaribu kumfundisha kipofu rangi nyekundu inafananaje.
Waislam wanasema koran ilishuka kutoka mbinguni.
Hakuna anayewabishia kutaka ushahidi. Tunaishia kusema SAWA.
Tukitaka proof tutaishia kugombana tu.
 
Ikiwa imeshapita mwaka mmoja sasa tangu Kanisa kubwa la Byzantine empire liitwalo HAGIA SOPHIA kubadili muelekeo na kuwa Msikiti huko Instanbul, Quora inawezekana ikawa ni mtandao unao tegemewa sana katika harakati za kiimani,

Quora ni tovuti ya kijamii ya maswali na majibu iliyopo Mountain View, California. Ilianzishwa miaka ya 2010. Watumiaji wa mtandao huu wanaweza kushirikiana kwa kuhariri maswali na kutoa maoni kuhusu majibu ambayo yamewasilishwa na watumiaji wengine. Waislamu wa magharibi wametumia mtandao huu kuusambaza sana uislamu kwa kutoa majibu yanayo kinahisha nafsi za wengi.

Miongoni mwa maswali na majibu kutoka Quora.

SWALI

Je, ni sababu gani ya kawaida inayopeleka Wakristo wengi kubadili dini na kuwa waislamu kutoka Ukristo?

MAJIBU NI KWAMBA

-Uislamu unajibu maswali yote kwa uwazi, kila kitu katika uislamu kina sababu ya kimantiki.
  • Uislamu unajibu maswali yote kuhusu yanayoonekana na yasiyoonekana.
  • Qur'an haina ukinzani hata mmoja, tofauti na maandiko mengine.
  • Kutamalaki kwa amani, utulivu na furaha ya ndani.
  • Haki : utawajibika kwa dhambi zako mwenyewe, hakuna mtu anayeweza kuhesabiwa kwa dhambi za mwingine.
  • Madhambi yote yamesamehewa, isipokuwa shirki. Anayesamehe dhambi ni MUNGU na wala sio nabii wala Mwanaadamu
  • Hulinda wanawake na kuwaunga mkono na kuwanyanyua na kuwaheshimisha
  • Katika uislamu Amri zote za Mwenyezi Mungu, ni kwa manufaa ya mwanadamu.
  • Muumba, ni wa kipekee, anajitosheleza, ni mmoja na mkamilifu, Hana sifa za kiume wala za kike, hakuzaa wala hakuzaliwa, hana mfano na kitu chochote kile.
  • Katika uislamu Hakuna wapatanishi au watangulizi, kati yako na Muumba wako, wakati wowote unapomhitaji Muumba wako, unaweza kuwasiliana Naye, Tofauti na dini zingine hadi ukaungame.

Nadhani haya ni baadhi ya mambo makuu, yaliyoathiri kusilimu kwa wazungu wengi kuacha ukristo na kuingia uislamu.

View attachment 2230031
Zanzibar waislamu wako 99% mbona wanatinduana marinda sana tu. Waelimishe ulio nao kuacha dhambi na sio kufurahia wengine kuongeza idadi
 
Kingine cha kuongezea, wazungu wako so curious kujifunza. Asilimia kubwa ya hawa watu “smiles” zao haziko genuine. Be smart kuwaelewa.
 
Mungu yupo,ukiangalia tu umbile lako unajua mungu yupo...una macho yanayoona tu kwenye mwanga,duniani Kuna mwanga..macho yalijuaje duniani Kuna mwanga hata uwe nayo!?..Kuna mtu kakusanifu,huyo ndiyo mungu,hivyohivyo kwa pua na oksijeni,kinywa na umeng'enyaji...
Logical non sequitur.

Unajua hoja yako inaeleza kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo kuliko inavyoeleza Mungu huyo yupo?

Unaelewa hilo au unahitaji nikufafanulie?
 
Sijapanga kukuthibitishia. Mimi ninaamini na nimethibitisha kwamba Mungu yupo na roho ipo, hilo linanitosha.
Unaruhusiwa kuamini uongo wowote unaotaka, na huwezi kuthibitisha uongo huo ni ukweli, ndiyo maana unajificha katika kichaka cha "sijapanga kukuthibitishia".
 
Unaruhusiwa kuamini uongo wowote unaotaka, na huwezi kuthibitisha uongo huo ni ukweli, ndiyo maana unajificha katika kichaka cha "sijapanga kukuthibitishia".
Mkuu mimi imani inanitosha kabisa. Na nilipoamini pia nilielewa kwa ufasaha mkubwa.
 
Logical non sequitur.

Unajua hoja yako inaeleza kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo kuliko inavyoeleza Mungu huyo yupo?

Unaelewa hilo au unahitaji nikufafanulie?
Umeolewa ndugu..au uko vague!!?..hueleweki
 
Mkuu mimi imani inanitosha kabisa. Na nilipoamini pia nilielewa kwa ufasaha mkubwa.
Kwani huo ndio mjadala?

Kwani wapi mimi nimekataa na kusema imani haikutoshi?

Kwani imani ya uongo haiwezi kukutosha?
 
Unazungumzia mjadala gani?
Nakwambia hivi, in point form.

1. Unaruhusiwa kuamini chochote unachotaka, hii ni haki yako ya kuamini, haina mjadala. Mpaka kwenye Universal Declaration of Human Rights ipo.

2. Wewe kuruhusiwa kuamini chochote, haina maana kuwa unachoamini ni kitu kipo kweli, kwa sababu hata uongo unaaminika, hivyo imani tu si kitu cha msingi katika kutafuta ukweli wa mambo.

3. Mimi najadili ukweli, kwa mantiki, kwa vipimo. Ukiujua ukweli, huhitaji imani.Imani inatumika pale ambapo huujui ukweli.

4.Kwa kupima kutafuta ukweli, Mungu muumba vyote, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

5. Mungu huyu anathibitishika kuwa hayupo kimantiki, na hawezi kuthibitishika kuwa yupo kimantiki.Zzaidi ya hapo ni ngonjera za kupandisha na kushusha uongo tu.

Kama unabisha, thibitisha kimantiki kwamba Mungu huyo yupo.
 
Back
Top Bottom