Mtandao wa vodacom mwisho lini kuwaibia watumiaji wake

Gulio Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,325
Reaction score
7,807
Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu huu mtandao kuibia watumiaji wake lakini hatuoni maboresho yoyote mimi leo nimelazimika kuandika uzi sababu nimeibiwa salio langu la tsh 300 na huu mtandao baada ya kujaza vocha wananitumia sms umekatwa sh 300 baada ya kujiunga na huduma ya "chekecha mkwanja "

Ni huduma ambayo sijawahi kujiunga wala sihijui lakini natumia sms kuwa umekatwa Tsh 300 kutokana na kujiunga huduma hii ni utapeli mkubwa sana voda wanaufanya nilazima serikali itoe jicho kufuatilia hii mitandao kwa hichi kinachoendelea naona watakuwa wanavuna pesa nyingi kuibia watumiaji

Screenshot_20230530-203436.png
 
Mwenyewe umejiwekea kajero ujiunge na MB 200.
 
Uliwafanyaje

Ova
niliwasongesha 120k na kukopa salio la 3k ,huu ni mwaka wa pili sasa laini iko hewani ila siweki vocha wala sifanyi miamala tena wamebaki kunipa gb2 kila siku majuzi natizama deni naona sidaiwi nilicheka sana .hii yote walinikorofisha kitu kidogo sana
 
mimi leo nimelazimika kuandika uzi sababu nimeibiwa salio langu la tsh 300
Yaan 300 unalialia wakati ukitumia M-PESA 15000 unarudishiwa 3000 ukitumia 1000 unarudishiwa 150 ukitumia 500 unarudishiwa 50, hivi unataka Vodacom wakuoende vipi mkuu ?
 
Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu huu mtandao kuibia watumiaji wake lakini hatuoni maboresho yoyote mimi leo nimelazimika kuandika uzi sababu nimeibiwa salio langu la tsh 300 na huu mtandao baada ya kujaza vocha wananitumia sms umekatwa sh 300 baada ya kujiunga na huduma ya "chekecha mkwanja "

Ni huduma ambayo sijawahi kujiunga wala sihijui lakini natumia sms kuwa umekatwa Tsh 300 kutokana na kujiunga huduma hii ni utapeli mkubwa sana voda wanaufanya nilazima serikali itoe jicho kufuatilia hii mitandao kwa hichi kinachoendelea naona watakuwa wanavuna pesa nyingi kuibia watumiaji

View attachment 2640680
Hadi MB,yaaani unajiunga TU ndani ya dakika kumi hata internet haijafunguka unatumia meseji kuwa kifurushi kimeisha.
 
Kampuni ikiibia wateja 100k mara 300 tu piga hesabu ? Hivi wewe unaiona 300 ni ndogo?
Yaan 300 unalialia wakati ukitumia M-PESA 15000 unarudishiwa 3000 ukitumia 1000 unarudishiwa 150 ukitumia 500 unarudishiwa 50, hivi unataka Vodacom wakuoende vipi mkuu ?
 
Mtoa uzi ni kama umeniwahi, binafsi Voda com wamekuwa wakinifanyia mambo ya kipuuzi toka mwaka jana, nakumbuka mwaka jana siku ya kwanza kuweka buku wakanikata mia mbili mara mbili nikabakiwa na mia sita, nilipo wapigia simu wakasema wamenitoa kwenye huduma nilizo jiunga.
Baada ya mwezi mmoja kupita wakanikata tena mia mbili na nilipo wawashia moto mwaka jana ukawa umepita. Mwaka huu mwezi huu wa tano wamenikata tena mia mbili, kiukweli nilikerekwa sana na kujiuliza vp ambaye hana muda wa kufuatilia pesa zake na ndugu zetu wa polini bila kusahau watu wazima si ndio kila siku wanalia bila kujua.
Kiukweli serikali isipokuwa makini ipo siku hali itakuwa mbaya sana.
 
Mimi tangu wagawe namba yangu kwa mtu mwingine nimeamua kuachana nao mazima, ipo hivi, kuna kipindi nilisafiri takribani kama miezi miwili hivi, hiyo sehemu ilikuwa Ina changamoto ya mawasoliano kwa upande wa Vodacom, ikabidi niwe natumia Halotel kwa kupiga na kutuma ujumbe wa kawaida, lakini kwa upande wa WhatsApp nikawa natumia Vodacom.

Cha ajabu wakagawa namba yangu kwa mtu mwingine, nikawapigia simu huduma kwa Wateja wakaniambia eti namba isipotumika miezi mitatu wanagawa kwa mtu mwingine, hivyo eti niongee na waliompa namba yangu ili afute usajili, baada ya jitihada zangu kugonga mwamba nikaamua kuachana na huduma yao.

Binafsi sioni sababu ya hii mitandao kugawa namba ambayo imesajiliwa kwa mtu mwingine kwa kigezo eti haikatumika kwa muda mrefu, kwa nini wasitoe namba mpya kwa mteja mpya!
 
Mitandao yote ipo hivyo siku 90 zikiisha line haipo hewani wanapitanayo!
 
ikiwa na deni hawagawi mkuu.! Mm niliwahi kukaa miezi minne bila kuwa hewani, nilikuwa nadaiwa 42,000 lakini hawakugawa[emoji23]
 
Back
Top Bottom