Mtandao wa WhatsApp haupatikani hewani kwa muda

Mtandao wa WhatsApp haupatikani hewani kwa muda

Watumiaji wengi wa mtandao wa WhatsApp wameripoti kushindwa kutuma wala kupokea ujumbe wowote asubuhi hii.

View attachment 2397216
Kwa mujibu wa Downdetector, zaidi ya watu 12000 wameripoti uwepo wa tatizo hili hadi kufikia mida ya saa 4:30 asubuhi.

Hata hivyo, hakuna taarifa yoyote rasmi iliyotolewa na Kampuni ya Meta yenye kuthibitisha au kukanusha kuhusu uwepo wa changamoto hii.

Kwako hali ipoje?
Freemason wanafanya maintenance
 
Nimehangaika si kidogo, nikahisi nimeishiwa bundle, zima simu washa hola!
Asanteni kwa taarifa.
 
.
JamiiForums94319067.gif
 
India ina watu bilioni 1.3 kuelekea point 4 na wana sikukuu yao ya Diwali. Na bado jana Rishi Sunak Mhindi kawa Waziri Mkuu wa Uingereza. Ilitarajiwa leo WhatsApp itakuwa chini, wazoefu wa internet traffic walisema nami kuna sehemu nilisoma jana
Ndo maana usiku nilisikia baruti🤭
 
India ina watu bilioni 1.3 kuelekea point 4 na wana sikukuu yao ya Diwali. Na bado jana Rishi Sunak Mhindi kawa Waziri Mkuu wa Uingereza. Ilitarajiwa leo WhatsApp itakuwa chini, wazoefu wa internet traffic walisema nami kuna sehemu nilisoma jana
Kwa hiyo Rish Sunak kaleta mafuriko ya wahindi kwenye wasap, bila shaka wahindi wataenda kujazana uingereza maana sasa wanatawala nchi mbili.
 
Back
Top Bottom