Mtanganyika wenzangu usiwe mwoga! Hizi zote ni fursa zinazokusubiria

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Najua wengine watakimbilia kusema "motivational speaker", lakini hata kama wote watakejeli, kejeli zao hazitaubadili ukweli ninaoenda kuuwasilisha!

Kenya ndiyo nchi inayoongoza Afrika Mashariki kwa kusafirisha nje mboga na matunda. Lakini wakati huo huo, Tanzania ina eneo kubwa linalofaa kwa kilimo ukilinganisha na Kenya.

Katika ardhi yote inayofaa kwa kilimo Tanzania, inayotumika ni chini ya asilimia thelathini na tano. Hiyo ni nini kama si isharq kuwa kuna fursa ya "kutoboa " kupitia kilimo nchini?

Mazao yanayoongoza kwa kuwaingizia Wakenya mamilioni mengi ya fedha ni MISHOKISHOKI (dragon) ikifuatiwa na parachichi za HASS. Ni wazi kuwa mazao yanayostawi Kenya yanaweza pia kustawi Tanganyika.

Nataka kusemaje?

Unaweza kuwa bilionea kwa kufanya kilimo cha kisasa. Lima:
1. Dragon fruits
2. Hass avocado
3. Apple
4. Nyanya
N.k., lakini hakikisha hali ya hewa ya eneo husika inaruhusu hicho kilimo.

Nasisitiza, lima kisasa, hata kama utaanza kwa kulima eneo dogo sana.

Na kama unaona huna maarifa yanayohitajika kwenye mazao husika, mtafute mjasiriamali wa kilimo mwenye uzoefu akupe semina, au uhudhurie kozi fupi ya Kilimo SUA.

Usiseme huna ardhi!
Usiseme huna mtaji!
Usiseme huna maarifa!
Usiseme huna nafasi!
Usiseme huwezi!

Penye nia pana njia! Ukishaamua kuwa bilionea kupitia kilimo cha kisasa, utakuwa umeshashinda kwa zaidi ya asilimia hamsini.

Inuka sasa uufukuzie ubilionea wako!
 
Attachments

  • Mr.Beatus_Malema_s_sentiments_on_a_Dragon_fruit_from_SJS_Organic_Farm_Kwanyange.(360p).mp4
    23.2 MB
  • CHINESE_FARMERS_IN_KENYA_REAP_PROFIT_FROM_DRAGON_FRUITS(720p).mp4
    32.7 MB
  • CHINESE_FARMERS_IN_KENYA_REAP_PROFIT_FROM_DRAGON_FRUITS(144p).mp4
    4.5 MB
  • Msichana_Mjasiriamali_Tanzania_kupitia_kilimo(240p).mp4
    6.8 MB
  • How_Asia_Harvesting_Million_of_Dragon_Fruits_-_Awesome_Asia_Agriculture_Tradition_Processing_F...mp4
    12.6 MB
  • Mbona_tunda_la_dragon-fruit_ni_ghali_zaidi_(240p).mp4
    19.7 MB
  • Kenyan_making_a_name_in_agribusiness_in_Rwanda(240p).mp4
    17.9 MB
  • HlSTORIA_..MJUE_KIJANA_ANAETENGEZA_MILIONI_120_KWA_MIEZI_3_ATOBOA_SIRI_NZITO(240p).mp4
    33.4 MB
  • MTANZANIA_MILIONEA_MWENYE_MASHAMBA_MAKUBWA_YA_PARACHICHI,_ASIMULIA_ANAVYOPIGA_MAMILIONI(144p).mp4
    14.8 MB
  • MKULIMA_WA_NYANYA_TAJIRI_WILAYA_YA_KARATU-MALELA(144p).mp4
    8.7 MB
  • MKOJO_WAMVURUGA_HUSSEIN_BASHE,_MAAJABU_YA_MKULIMA_IRINGA(144p).mp4
    10.1 MB
  • Tajiri_wa_parachichi_aliyemkosha_Waziri_Mkuu__Nilianza_na_mtaji_wa_elfu20,_sasa_navuna_mamilio...mp4
    13.5 MB
  • EXCLUSIVE___NILIITWA_KICHAA_KWA_KUOKOTA_MBEGU_ZA_PARACHICHI__-_ERASTO_NGOLE(144p).mp4
    30.2 MB
  • NEMESI_ATEMBELEWA_NA_UJUMBE_KUTOKA_CHUO_CHA_ULINZI_CHA_TAIFA(144p).mp4
    11.9 MB
  • NEMES;Apokea_Ugeni_Mzito_Kutoka_Chuo_cha_Ulinzi_Nchini_Wajifunza_Kilimo_cha_Parachichi_Nimefar...mp4
    29.1 MB
Najua wengine watakimbilia kusema "motivational speaker", lakini hata kama wote watakejeli, kejeli zao hazitaubadili ukweli ninaoenda kuuwasilisha!

Kenya ndiyo nchi inayoongoza Afrika Mashariki kwa kusafirisha nje mboga na matunda. Lakini wakati huo huo, Tanzania ina eneo kubwa linalofaa kwa kilimo ukilinganisha na Kenya.

Katika ardhi yote inayofaa kwa kilimo Tanzania, inayotumika ni chini ya asilimia thelathini na tano. Hiyo ni nini kama si isharq kuwa kuna fursa ya "kutoboa " kupitia kilimo nchini?

Mazao yanayoongoza kwa kuwaingizia Wakenya mamilioni mengi ya fedha ni MISHOKISHOKI (dragon) ikifuatiwa na parachichi za HASS. Ni wazi kuwa mazao yanayostawi Kenya yanaweza pia kustawi Tanganyika.

Nataka kusemaje?

Unaweza kuwa bilionea kwa kufanya kilimo cha kisasa. Lima:
1. Dragon fruits
2. Hass avocado
3. Apple
4. Nyanya
N.k., lakini hakikisha hali ya hewa ya eneo husika inaruhusu hicho kilimo.

Nasisitiza, lima kisasa, hata kama utaanza kwa kulima eneo dogo sana.

Na kama unaona huna maarifa yanayohitajika kwenye mazao husika, mtafute mjasiriamali wa kilimo mwenye uzoefu akupe semina, au uhudhurie kozi fupi ya Kilimo SUA.

Usiseme huna ardhi!
Usiseme huna mtaji!
Usiseme huna maarifa!
Usiseme huna nafasi!
Usiseme huwezi!

Penye nia pana njia! Ukishaamua kuwa bilionea kupitia kilimo cha kisasa, utakuwa umeshashinda kwa zaidi ya asilimia hamsini.

Inuka sasa uufukuzie ubilionea wako!
Yes, Motivational Speaker!
 
Asante sana kwa uzi mzuri, bahati mbaya sana vijana wa kitanzania wengi wanataka kazi za maofisini, private au serikalini na kukaa mjini kununua Samsung na iphone. Na kwenye thread kama hizi huwaoni hata wachache watakaokuja kuchangia ushaanza kuwaona wa kukubatiza majina. Ila ukweli utabakia palepale kilimo kinalipa kwa mtu asiyekata tamaa na kujituma. Mifano ipo mingi sana, ila kilimo kinataka uvumilivu maana unasubiria miezi kadhaa ndo uone matunda, wakati mwingine hasara. Wakati watu wanataka wa bet asubuhi jioni wapate matokeo kama mkeka umekubali au umechanika.😅
 
Nimelima sana miaka kadhaa.....JIBU....KILIMO SI KITU CHA KUFANYWA NA KILA MTU.....kwa wengine ni kamari....kwa wengine ni KARAMA.
 
Kuanzia babu yangu, baba yangu mpaka mimi sote tumelima lakini hatujawahi kutoboa kwa uhakika.
Kwa Tanzania, Kilimo ni shughuli ya kubahatisha kwa mkulima lakini ni shughuli ya uhakika kwa mlanguzi na dalali.

Nyinyi wengine limeni tu, mimi nitakuja kununua mazao yenu kwa bei ya chini ili nikauze kwenye soko la uhakika kwa bei ya juu.
 
✅🙏🙏🙏
 
Kilimo cha kienyeji kitakuletea matokeo ya kienyeji.

Kama unataka matokeo yenye tija, fanya kilimo cha kisasa.
 
Kama hujajipanga USIINGIE KWENYE KILIMO. Bora uendelee kufanya uchuuzi wa mazao kuliko kujiingiza kwenye kamari ya kilimo. Binafsi kwa sasa najipanga taratibu. Tayari nina ardhi na ninaendelea kuweka miundombinu yote muhimu kwanza. Kufika 2026 nitaweza kufanya kilimo cha kisasa kwa uhakika.
 
Kuanzia babu yangu, baba yangu mpaka mimi sote tumelima lakini hatujawahi kutoboa kwa uhakika.
Kwa Tanzania, Kilimo ni shughuli ya kubahatisha kwa mkulima lakini ni shughuli ya uhakika kwa mlanguzi na dalali.

Nyinyi wengine limeni tu, mimi nitakuja kununua mazao yenu kwa bei ya chini ili nikauze kwenye soko la uhakika kwa bei ya juu.
Naweza kukisia kilichotokea
1. Babu yako alilima kama alivyofundishwa na wazazi wake
2. Baba yako akafanya kama Babu yako
3. Wewe nawe ukafuata nyayo za baba yako.

Kwa kufanya kama alivyofanya baba yako ambaye naye aliiga kwa baba yake, hakukuwepo na namna ila kupata matokeo yale yale aliyoyapata babu yake baba yako.

Njia pekee ambayo ingekusaidia kupata matokeo tofauti ni kufanya kwa namna tofauti na walivyofanya wao:
~ Ungechagua mazao yenye uhakika wa soko ndani au nje ya nchi

~ Ungetafuta maarifa kwa kuhudhuria semina au kozi fupi zinazohusiana na na kilimo cha hayo mazao

~ Ungeweka mpango wa uendeshaji wa shughuli husika kuanzia hatua za awali mpaka bidhaa ifikapo sokoni. Kwa maana hiyo, ungeweza kuamua kulima mwenyewe, kusafirisha mwenyewe, na kuuza mwenyewe.
 
Unaongea sana theories.
 
Back
Top Bottom