Ndg gentamycine mbona sijaona sehemu jamaa kasifia chama chetu pendwa cha ccm? Yeye kamsifia mheshimiwa rais kwa utendaji wake which is not bad and he is not the first opposition's fun to declare the same. Jamaa yuko sawa kwa baadhi ya mambo ni kweli Mheshimiwa rais ndani ya mwaka moja kafanya Mengi mazuri na mengine si mazuri (kama ni kwa asilimia mazuri yanaweza kulingana na asilia alizoshinda nazo urais kwa mtizamo wangu). lakini kusema ndg EDO asingefanya hivyo ni upotoshaji mkubwa na usiokubalika, maana naye angefanya mazuri kwa upande anaoona unafaa kwa mtizamo wake maana kama nchi hatuna sera na dira za kudumu za maendeleo . Mwingine anazungumza viwanda mwingine Elimu, sasa kama edo angeweza kusomesha vijana wote bure akasitisha ajira kwa muda na kununua ndege wenye mtizamo wake wangeona kafanya makubwa zaidi na wangesema Magu asingeweza kufanya hayo.
MIMI Nampongeza Rais kwa hatua za kuthibiti rushwa, utumishi holela na safari zisizo na tija kwa nchi , ila kama angeruhusu uhuru wa mawazo, akakubali kukosolewa, bunge kuwa huru kama enzi za mkwere na wapinzani kuwa huru kufanya siasa popote BILA KUVUNJA SHERIA ZA NCHI basi Magu angekuwa The best President after the late JKN.