Mtangazaji Adam Mchomvu amwomba radhi JPM kwa kutompigia Kura mwaka jana

Mtangazaji Adam Mchomvu amwomba radhi JPM kwa kutompigia Kura mwaka jana

Ni haki yake kusema hayo. Lowasa anawatesa sana, mzee wa watu katulia tuli.
 
haya Magufuli katwaa hekari 33 za waziri Sumaye ..wananchi wanajikatia maeneo
kama upo karibu na huna ardhi kachangamkie dili kuleeeee

Mi nipo mbali mdau, ila wananchi wake watakua wajinga kiasi gani mpaka 33 tu waitie wageni wakati hapo ilibidi wagawane watu angalau 6. Hao ni wazembe kabisa.
 
Jamaa anataka asikike kwa kiki ya kijinga. Mbona kuna waliompigia kura na sasa wanajuta ila hawasemi? Mwambieni huyo mchovu kwamba nafasi za u-DC na u-DED zimejaa.

Halafu inaonekani ni mmoja kati ya wanne kama usemavyo utafiti huu.

c52b3a838df63e2a2ce0ce6d1a2a0cef.jpg
 
Bangi mbaya sana,hata siku moja isihalalishwe nchini,huyo Adam nimemsikiliza anatoa pongezi bila kutaja ni yapi mkuu kafanya,anakalia hapa kazi tu, kwa ufupi kama kijana mwenzangu nimemwona kama 'Hopeless' vijana wenzie hawana ajira yeye anabwabwaja tu.
 
Akizungumza kwa ' huruma ' kabisa huku akikaribia ' kulia ' Mtangazaji ' maarufu ' wa Clouds fm Adam Mchomvu wakati akitoa salamu zake za mwaka wa kuzaliwa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amesema kuwa kiukweli mwaka jana hakuwa mmoja wa Watu waliompigia Kura ya Urais na kwamba Kura yake alimpa aliyekuwa Mgombea wa UKAWA Ndugu Edward Ngoyai Lowassa.

Mtangazaji huyo hakuishia tu hapo akaenda mbele na kusema kuwa ' anajuta ' ni kwanini hakumpigia Kura Rais Magufuli na kwamba anahisi pengine ' alirogwa ' na nguvu ya safari ya matumaini ambayo kimsingi imeshia tu katika ' kugoma ' na ' kuandamana '.

Mwisho kabisa Mtangazaji Adam Mchomvu akasema kuwa kwa Kipindi hiki tu cha mwaka mmoja ameona mambo makubwa ambayo ana uhakika kabisa kuwa aliyekuwa Mgombea wa UKAWA Ndugu Edward Lowassa asingethubutu na hata kuweza kufanya hasa kutokana rekodi yake ya ' wasiwasi ' dhidi ya rasilimali za nchi alizonazo.

Kama kawaida yake Mtangazaji Adam Mchomvu huwa hana ' Unafiki ' na akamalizia tu kwa kuwataka Watanzania wote wamuunge mkono Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwani alichokifanya tu kwa mwaka huu mmoja ni kikubwa na kwamba miaka minne ijayo Magufuli ataifikisha Tanzania kule inakotakiwa kufika hasa Kimaendeleo.

Binafsi kama GENTAMYCINE nichukuwe fursa hii kumpongeza kabisa Mtangazaji Adam Mchomvu kwanza kwa kuwa ' muwazi ' na ' mkweli ' na pia kuweza kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa Uongozi wake lakini na Watu wengine hasa wale Wana UKAWA hasa CHADEMA nanyi pia igeni hii busara na hekima aliyoionyesha mwenzenu mwana CHADEMA ' kindakindaki ' Adam Mchomvu na nyie mkubali ' Kazi ' za Rais wetu na ikiwezekana si vibaya hata mkizichana chana tu hizo Kadi zenu za CHADEMA na mrejee rasmi CCM kwani CCM ya sasa chini ya Rais Dkt. Magufuli ' imetakata ' na ' mwendo mdundo '.

Happy Birthday Rais wangu Mpendwa na Mkombozi wa Watanzania ' wanyonge ' na ' fimbo ' ya ' mafisadi ' na ' wavivu ' Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu, akulinde, akubariki na akupe afya njema.

Akhsante Adam Mchomvu kwa ' kuthubutu '.
HIVI NI NANI ALIYE WALOGA CCM MBONA HUWA MNAGA HOJA MAKINI NA NZITO ZAIDI YA KULETA THREADS GOIGOI???????????
SO WHAT THE PERSONAL COOKED INFO IS BENEFICIAL TO THE PUBLIC WISE???????????
HEBU ONDEENI UJINGA WENU NA HUYO MCHOVU,WHO IS MCHOVU TO US THAN IS NOTHING MAY BE SOMETHING TO YOU?
TUNATAKA KUSIKIA HABARI ZA MAENDELEO NA SIYO POLITICAL COMEDY TIME TO TIME THAT YOU BOYS OF CCM BRINGS TO US AS THE GREAT THINKERS.
 
Anatafuta kick.....angoje TU magu atamuita

OVA
 
Anadhan zali kama lililomuangukia Hudson Kamoga ndio na yeye ataukwaa!kwanza magufuli mwnyw anajua fika kuwa vita ya membe na lowassa ndio iliyosababisha yeye kuwa rais hata wana chato aliwaambia wamsamehee alikuwa anabeep tu kugombea
 
Hivi yule aliyekua mkuu wa mkoa wa morogoro Mzee wa nimekosa Mimi nimekosa sana alishasamehewa?
 
Back
Top Bottom