Mtangazaji kumsifia mchezaji muda wote ni sahihi?

Mtangazaji kumsifia mchezaji muda wote ni sahihi?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Mtangazi mmoja wa mechi ya leo kati ya Argentina na Australia, anaonekana kuwa ni shabiki wa Messi na Argentina kwa jumla. Muda mwingi anatumia kumsifia Messi hasa katika kipindi cha kwanza. Kweli Messi ni mchezaji maarufu ila kumsifia kupita kiasi wewe kama mtangazji ni sahihi?

Mchezaji akifanya vitu adimu kumsifia ni sahihi na kawaida, ila kutumia muda mwingi kumsifia mchezaji hata kama hana mpira sio kuwakera washabiki wa timu pinzani?

Messi kweli ni staa, lakini wazungu wanasema, "too much of everything is harmful".

Mtu maarufu akifanya au kusema jambo la kawaida tu, basi jambo hilo linaweza kugeuka kuwa ni jambo kubwa. Halikadhalika, mchezaji Maarufu (Star) akifunga bao la kawaida tu, basi bao hilo litasifiwa utadhani yeye ndio wa kwanza kufunga.

Usisahau wachambuzi wa soka nao ni watu wa kwenda na upepo wa soka.

Hongera Messi, ila mtangazai tambua unasikilizwa na mashabiki wa timu zote mbili, hivyo watendee haki (usiwe bias).

Mtangazi hupaswi kuwa mshabiki ingawa kuchagiza ni muhimu (ficha mahaba yako).
 
We jamaa bana hivi upo serious kweli? Usiseme mtangazaji kumsifia mchezaji mmoja sema mtangazaji kumsifia Messi,
Messi ni lazima asifiwe unachotakiwa ni kufurahia anacho fanya Messi maana huenda usione tena
Mambo yakibadilika, utashangaa wanavyobadilisha lugha na hapa ndio huwa nashindwa kuwaelewa baadhi ya watangazi na wanaojiita wachambuzi wa soka.
 
Mtangazi mmoja wa Mechi ya leo kati ya Argentina na Australia, anaonekana kuwa ni shabiki wa Messi na Argentina kwa ujumla. kweli Messi ni mchezaji maarufu ila kumsifia kupita kiasi wewe kama mtangazji ni sahihi?

Mchezaji akifanya vitu adimu kumsifia ni sahihi na kawaida, ila kutumia muda mwingi kumsifia mchezaji hata kama hana mpira sio kuwakera washabiki wa timu pinzani?

Messi kweli ni star, lakini wazungu wanasema, "too much of everything is harmful".

Mtu maarufu akifanya au kusema jambo la kawaida tu, basi jambo hilo linaweza kugeuka kuwa ni jambo kubwa. Halikadhalika, Mchezaji Maarufu(Star) akifunga bao la kawaida tu, basi bao hilo litasifiwa utadhani yeye ndio wa kwanza kufunga.

Usisahau wachambuzi wa soka nao ni watu wa kwenda na upepo wa soka.

Hongera Messi, ila Mtangazi tambua unasikilizwa na mashabiki wa timu zote mbili, hivyo watendee haki(usiwe bias).
👆
Nakadori mjibu huyu jamaa...
 
Saivi australia ndo wanaonekana sasa!!sikia wanavyo tajwa!?!
 
We jamaa bana hivi upo serious kweli? Usiseme mtangazaji kumsifia mchezaji mmoja sema mtangazaji kumsifia Messi,
Messi ni lazima asifiwe unachotakiwa ni kufurahia anacho fanya Messi maana huenda usione tena
Wajukuu wetu watakuwa wanatuonea wivu kumshuhudia messi live.
Maana hajawahi tokea na kwa soka hili la kisasa huenda asije kutokea tena mchezaji kama Messi kwenye hii dunia.
 
Back
Top Bottom