Mtangazaji Maulid Kitenge wa EFM unapata wapi uhalali wa Kukicheka Kiingereza hafifu cha Kocha wa Simba SC wakati Wewe ndiyo hukijui kabisa?

Kitenge mwenyewe huongea lugha mbovu maana hajui syntax , semantics au phonology zinakuaje kwenye lugha ya kiingereza anachotumia, na anatakiwa afahamu binadamu tuna fisrt language, second language, third language na kuendelea hivo mfano msukuma first language ni kisukuma, second language kiswahili na third language kiingereza kama cha Rais wetu Magufuli hivo sio kumcheka mtu kikubwa angalia general meaning kwenye kile alichoongea umeelewa?
 
Nyie ndo wale watu wanaoabudu makaratasi bila kuangalia uwezo binafsi wa mtu. Kitenge amebarikiwa na ni mweledi katika mambo mengi ndo sababu anabebeka. Wewe endelea na makaratasi yako, mwenzio anasonga mbele.[emoji3526][emoji3526]
Mweledi kwenye mambo mengi kama yapi ?
 
Ni Afrika tu ndio watu wanaona kujua kiingereza ni kuwa na akili, kwamba mtu anayejua kuongea kwa ufasaha basi ana akili. Huyo Kitenge kumbe bado hajastaarabika!

Ni ushamba na tabia hizo hufanywa na washamba, unajua kuna watu anahisi kusafiri kwenda USA au kwingineko tayari ni mjanja kumbe ushamba wake haujaisha na hana uelewa wa mambo mengi ya kidunia
 
acha kumsema nabi,wewe mlalamikie huyo kitenge,nabi kakukosea nini?
 
Kama hayo uyasemayo ni kweli usishangae kwa anayoyafanya kwa sababu ni bongolala
 
Hivi lugha kama hatumii mara kwa mara itakuwaje mbobeZi kuongea, unategemea mtanzania aongee kiingereza kama mtu anayeishi pale London, ni ngumu sana, hivyo hivyo mnyaturu alihemia Shinyanga haweza kuongea kisukuma fasaha kama mkazi wa kule, ni kannuni ndogo sana hiyo
 
Maisha haya [emoji23][emoji23]sasa wewe ulie faulu una nini?
Unajuaje hana kitu kweye hii anonymity? Hivi mbona huwa mnakua na akili za kijinga hivi? Yaani unaamini maisha yako magumu ni kwa kila mtu[emoji28].

Si ajabu hata huyo kitenge unaemuona ana maisha mazuri kuliko huyo jamaa nae akawa humu, ila kwakua ni fake I'ds unaweza kumtukana tu na kumtwisha huo umasikini wako.

Acha ushamba wa maisha.
 
Yaani kama hajui kiingereza, ni hakijui tu, hata kama anayemcheka naye hakijui..!!
 
Nyie ndo wale watu wanaoabudu makaratasi bila kuangalia uwezo binafsi wa mtu. Kitenge amebarikiwa na ni mweledi katika mambo mengi ndo sababu anabebeka. Wewe endelea na makaratasi yako, mwenzio anasonga mbele.[emoji3526][emoji3526]
Tukiachana na habari za makaratasi, Kitenge anauwezo gani?

Naomba tujadili vizuri tu.
 
Tukiachana na habari za makaratasi, Kitenge anauwezo gani?

Naomba tujadili vizuri tu.
Uwezo wake unapimwa na kazi anazozifanya. Kazi zote alizofanya kwenye taaluma yake ya uandishi wa habari na utangazaji ameifanya kwa weledi mkubwa hadi ameweza kuwavutia wasikilizaji na watazamaji wake ndani na nje ya nchi. Na kwa kuthibitisha hilo ni namna ambavyo amekuwa akipewa kazi mbalimbali nje ya ofisi yake na zote amezifanya kwa weledi mkubwa. Kijamii Maulid amekuwa kioo kwa kuishi vyema na wadau mbalimbali na hata kidini amekuwa muumini mzuri wa dini yake. Mengine utaongeza.
 
Hivi huyu kijora anapeleka biashara gani huko ughaibuni?
 
Co Afrika mkuu,ni bongo tu kuna huu ushamba
Ni Afrika tu ndio watu wanaona kujua kiingereza ni kuwa na akili, kwamba mtu anayejua kuongea kwa ufasaha basi ana akili. Huyo Kitenge kumbe bado hajastaarabika!
 
Moderator:ndio tumefika huku kujadili personal isssues za mt mu kisa mpira huu ni Upumbavu wa hali ya juu.

Direct linaonyesha jinsi gani Watanzania tumekosa kazi na kupenda kukalia majungu, mtima nyongo, wivu, tamaa...nk

Mtu mnayemjadili kawashinda kila kitu halafu mbaya zaidi Jumapili au ijumaa mtu upo kanisani/msikitini ukisali kumbe unanuka majungu tu acheni kuhukumu hiyo siyo kazi zenu.

Kwa unafiki Tanzania Duniani wa Kwanza
 
Kazi yake kuwaponda wasomi... Mara ukitoa elimu ya darasani unabaki na nini... Mimi nikamwambia unabaki na. Ujinga. So insecure na wasomi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…