Mtangazaji na DJ wa East Africa Radio, Baba T atimiza miaka 81

Mtangazaji na DJ wa East Africa Radio, Baba T atimiza miaka 81

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Kutoka EATV facebook wall,

Kwa mara nyingine tumebarikiwa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mfanyakazi mwenzetu mwenye umri mrefu zaidi hapa ofisini. Jina lake halisi ni Emsly Smith maarufu kama Baba T.

Baba T ni Dj wa muziki wa Reggae na pia ni mtangazaji wa kipindi cha 'Lovers Rock' cha East Africa Radio. Leo ametimiza miaka 81 na bado ana nguvu kama unavyomuona kwenye picha.

Baba T ni mtu mwenye upendo kwa kila mmoja, kila siku asubuhi anapofika ofisini huwagawia wafanyakazi wa kike wote biskuti za chocolate, na wanaume huwa anawapa vipande vya nazi.

Happy Birthday Baba T. Live long Rasta Man.

42A772A8-10C2-4BC9-A26A-5A7A8FB885CB.jpeg

My take:


Kiukweli nimemfahamu Baba T miaka mingi kidogo nikiwa mfatiliaji wa vipindi vya burudani enzi hizo lakini sikuwahi ku note his age. Nimeshtuka mno kama kwenye media, tasnia ya utangazaji, na kama DJ wa muziki wa raggae Baba T anatimiza miaka 81 akiwa bado active kwenye industry alafu ni kama wadau wa media na entertainment wanachukulia poa mno. Hata hii birthday yake inapita kirahisi mno

Watanzania tujifunze kukubali vyetu! Tunahitaji kuonesha heshima na appreciation kwa huyu mzee akiwa hai. Wadau wa media na burudani kama mnapita hapa ...please tumuenzi huyu mzee

Happy birthday Baba T
 
Asee hili kweli ni jambo kubwa. 81years huyu ni lulu akitumika vizuri.
Moja ya vitu vinavyo inspire wengine ni appreciation kwa watu kama hawa. Ukiangalia MTV au BET jinsi wenzetu wanavyothamini legendary kama hawa ni baraka tosha na inspiration kwa wengine. How kitu kikubwa hivi kinapita kirahisi hivi tena kwa mtu wa media? Hivi hawa watu wa media wasipokumbukana nani awakumbuke kwanza?

CC pasco na wadau wengine ...
 
Baba T ni vegetarian toka enzi za ujana wake tangu alipoanza kujihusisha na imani ya ki-rastafarian.

ni kawaida kwa vegetarians kuzeeka huku wakiwa bado na utimamu wa kimwili na akili.

kuna uhusiano mkubwa sana kati ya vyakula tunavyokula na utimamu wa kimwili.
 
Baba T ni vegetarian toka enzi za ujana wake tangu alipoanza kujihusisja na imani ya ki-rastafarian.

ni kawaida kwa vegetarians kuzeeka huku wakiwa bado na utamamu wa kimwili na akili.

kuna uhusuano mkubwa sana kati ya vyakula tunavyokula na utimamu wa kimwili.
Still spinning na yuko vizuri kweli ...imagine a DJ at that age? Lovers rock kitambo sana ....
 
Back
Top Bottom