Mtangazaji na DJ wa East Africa Radio, Baba T atimiza miaka 81

Mtangazaji na DJ wa East Africa Radio, Baba T atimiza miaka 81

Kutoka EATV facebook wall,

[HASHTAG]#KUMBUKUMBU[/HASHTAG] Kwa mara nyingine tumebarikiwa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mfanyakazi mwenzetu mwenye umri mrefu zaidi hapa ofisini. Jina lake halisi ni Emsly Smith maarufu kama Baba T. Baba T ni Dj wa muziki wa Reggae na pia ni mtangazaji wa kipindi cha 'Lovers Rock' cha East Africa Radio. Leo ametimiza miaka 81 na bado ana nguvu kama unavyomuona kwenye picha.

Baba T ni mtu mwenye upendo kwa kila mmoja, kila siku asubuhi anapofika ofisini huwagawia wafanyakazi wa kike wote biskuti za chocolate, na wanaume huwa anawapa vipande vya nazi.

Happy Birthday Baba T. Live long Rasta Man.

My take;

Kiukweli nimemfahamu Baba T miaka mingi kidogo nikiwa mfatiliaji wa vipindi vya burudani enzi hizo lakini sikuwahi ku note his age. Nimeshtuka mno kama kwenye media, tasnia ya utangazaji, na kama DJ wa muziki wa raggae Baba T anatimiza miaka 81 akiwa bado active kwenye industry alafu ni kama wadau wa media na entertainment wanachukulia poa mno!!! Hata hii birthday yake inapita kirahisi mno!!! Watanzania tujifunze kukubali vyetu! Tunahitaji kuonesha heshima na appreciation kwa huyu mzee akiwa hai. Wadau wa media na burudani kama mnapita hapa ...please tumuenzi huyu mzee!!!

Happy birthday Baba T
Mara nyingi BabaT anatembea na miguu kutoka kwake Mbezi Africana nadra sana kupanda basi,si ajabu ndio maana ana umri mkubwa lakini ukimuona utadhani yupo miaka kati ya 55 na 60
 
Yule prof wa UDSM walikutana na Nyerere huko ndo akamuomba aje afundishe chuo kikuu cha mlimani. Kupitia yeye marastafatiani wakapewa eneo kubwa sana huko kigoma na dsm....ambapo sasa eneo la dar limefikia thamani ya bilion kadhaa hii imefanya baadhi ya marasta wenye tamaa kuanza kuwashawishi wenzao wauze hilo eneo la dar
Mwalimu Nyerere aliwaalika hata Wamarekani weusi na wengi wapo Kigamboni wengine wana mashamba ya kahawa Mbozi na wapo hadi leo,pale Kimara Mwisho kulikuwa na bucha moja maarufu na kisasa ilikuwa ikiitwa Little John ,hiyo bucha ilikuwa ya Mmarekani mweusi na washwahili washirika walimfanyia hila na akaamuriwa aondoke nchini,bucha ,ardhi na mali nyingine zikakombwa na waliokuwa washirika zake ambao walishindwa kuindesha bucha hiyo akina Sunday ,Rich Mlowo,
 
Hongera sana umejitunza vyema Mwenyezi Mungu akubariki sana
 
Inawezekana Tegeta ilikuwa ngome ya Rastafarian kwa mwendo huu ...
Yeah kila Jumamosi wanakutana kule Tegeta.

Yule Prof kwa sasa Marehemu.

Nadhani alikuja enzi za akina Prof. Walter Rodney.

Pale UDSM ukisoma mambo ya Development Studuies lazima usome kitabu cha Walter Rodney kinaitwa "How Europe Underdeveloped Africa".
Jamaa alikuwa na akili sana alipata PHD akiwa na miaka 24. Kazi yake iliyompa PHD ni hicho kitabu nilichokitaja hapo juu.

Mwalimu Nyerere aliwaalika hata Wamarekani weusi na wengi wapo Kigamboni wengine wana mashamba ya kahawa Mbozi na wapo hadi leo,pale Kimara Mwisho kulikuwa na bucha moja maarufu na kisasa ilikuwa ikiitwa Little John ,hiyo bucha ilikuwa ya Mmarekani mweusi na washwahili washirika walimfanyia hila na akaamuriwa aondoke nchini,bucha ,ardhi na mali nyingine zikakombwa na waliokuwa washirika zake ambao walishindwa kuindesha bucha hiyo akina Sunday ,Rich Mlowo,
Waswahili hawaja anza majungu siku hizi!!
Hiyo dhambi itawatafuna tu.
 
Hbd rasta, Baba T anaheshimika sana huko kwao Jamaica, bday yake mwaka juzi konshen alimuimbia wimbo

Mbona nasikia Baba T ni Mchagga aisee....au nililishwa tango pori?Hebu tupeni verification..huyu ni mtu muhimu sana TZ hii.
 
Mbona nasikia Baba T ni Mchagga aisee....au nililishwa tango pori?Hebu tupeni verification..huyu ni mtu muhimu sana TZ hii.
Mkuu Baba T ni mjamaica alikuja na wenzie miaka ya 80 kuna wengine walisettle morogoro na wengine walienda kigoma, mwalimu aliwapa ardhi kubwa wafanyie shughuri zao, baadhi walirudi kwao baadae, hivi karibuni nilipata taarifa kuwa lile eneo lao la kigoma lilitaifishwa.
 
Mara ya mwisho naonana naye alikuwa anatimiza 80. Lakini nikijilinganisha naye najiona tayari nimeshajichokea wakati yeye ni mkubwa kuliko father wangu.
Baba T ni vegetarian toka enzi za ujana wake tangu alipoanza kujihusisha na imani ya ki-rastafarian.

ni kawaida kwa vegetarians kuzeeka huku wakiwa bado na utimamu wa kimwili na akili.

kuna uhusiano mkubwa sana kati ya vyakula tunavyokula na utimamu wa kimwili.
 
Mkuu Baba T ni mjamaica alikuja na wenzie miaka ya 80 kuna wengine walisettle morogoro na wengine walienda kigoma, mwalimu aliwapa ardhi kubwa wafanyie shughuri zao, baadhi walirudi kwao baadae, hivi karibuni nilipata taarifa kuwa lile eneo lao la kigoma lilitaifishwa.

Duh..basi kuna kilaza mmoja aliniaminisha Baba T ni pure Mchagga....Hiyo story ya Wajamaica kuja TZ miaka hiyo naifahamu,kumbe na Baba T alikua mmoja wapo.Very interesting story!
 
Baba T ni vegetarian toka enzi za ujana wake tangu alipoanza kujihusisha na imani ya ki-rastafarian.

ni kawaida kwa vegetarians kuzeeka huku wakiwa bado na utimamu wa kimwili na akili.

kuna uhusiano mkubwa sana kati ya vyakula tunavyokula na utimamu wa kimwili.
Hivi nifanyeje kuwa vegetarian maana kuna wakati huwa nasiki mwili unataka ka nyama japo sipendi nyama ila samaki napenda sana
 
ulaji wa nyama sana na ngono za mara kwa mara zinachosha sana,mwili unatumia calories nyingi sana ku digest nyama mpaka iwe rahisi kuwa absorbable kuliko samaki na mbogamboga
Basi hapa nitaondoa nyama ila samaki nitaendelea nayo
 
Hahaha hiyo ya vipande vya nazi na chocolate itakuwa kuna kitu ameking'amua ndani ya eneo la kazi labda vijana wamekuwa hawako makini kwenda na wakati
 
Hii ya kuwagawia wanawake biskuti za chocolate na wanaume vipande vya nazi imekaaje hii? Mmeshawahi kumuuliza maana ya jambo hili? Au anamaanisha wanawake wakila hizo biskuti ndio wanakuwa watamu zaidi?
Mkuu huyu rasta anajua vyakula ambavyo ni dawa.

Nazi inaongeza libido kwa wanaume huna haja ya kula miti shamba mingi au dawa za hospital kuongeza nguvu za kiume.

Chocolate pia inatokana na nuts huongeza libido, sema hii ukila yenye sukari nyingi huongeza mwili kitu ambacho sio kizuri kwa mwanaume.
 
Moja ya vitu vinavyo inspire wengine ni appreciation kwa watu kama hawa. Ukiangalia MTV au BET jinsi wenzetu wanavyothamini legendary kama hawa ni baraka tosha na inspiration kwa wengine. How kitu kikubwa hivi kinapita kirahisi hivi tena kwa mtu wa media? Hivi hawa watu wa media wasipokumbukana nani awakumbuke kwanza?

CC pasco na wadau wengine ...
Mkuu

Media zetu zinashangaza sana
 
Baba T ni vegetarian toka enzi za ujana wake tangu alipoanza kujihusisha na imani ya ki-rastafarian.

ni kawaida kwa vegetarians kuzeeka huku wakiwa bado na utimamu wa kimwili na akili.

kuna uhusiano mkubwa sana kati ya vyakula tunavyokula na utimamu wa kimwili.
Mkuu

Acha nichume mlenda,kwanza nyama vyuma vimekaza
 
Back
Top Bottom