Mtangazaji Paul James 'PJ' arejea Clouds FM

Dindilimunyo

Senior Member
Joined
Sep 12, 2016
Posts
108
Reaction score
206


Wakuu salamu.

Inasemekana PJ wamerudi tena Clouds fm. Waliondoka kwa mbwembwe sana kwenda Efm japo kwa maoni yangu hawakufanikiwa kufanya kile nilichotarajia! Lakini leo asubihi katika nyapia nyapia zangu pale Efm inasemekana PJ amekabidhi barua ya kuacha kazi na leo asubuhi ameonekana Clouds fm.

Hoja yangu ya msingi: Je, Radio za Tanzania zimekosa kabisa kutengeneza damu mpyaa hadi kugombania watangazaji wale wale ambao kimsingi hawana jipya?

Niliona usajili wa Gadner pale Clouds kutoka Efm nao haukuleta jambo jipya sana kwenye jahazi! Ukiangalia kitakwimu bado Ubaoni ya Efm ndio yenye wasikilizaji wengi kwa mujibu GO nyakati za jioni. Ilitosha kwa Clouds kujifunza hilo kwamba sasa wanapaswa kuamini damu mpya.

Kingine cha kusikitisha kwenye radio hizi zimebakia kugombania watu maarufu na huku wenye taaluma hii wakiwa mtaani hawana kazi mfano mtu kama Gigy Money anakuwa mtangazaji kwa elimu ipi na kwa taaluma ipi?

Radio zetu hizi kubwa za Dar zinapaswa kuwaamini na kuwapandisha madaraja watangazaji wa Mikoani ambao ni wazuri kuliko hawa mjini wanao wasumbuaa.

Nimejiuliza sana mikataba ya hawa watu ipoje kama PJ ameweza rudi Clouds kijanja janja hivi na hata miaka miwili haijaisha.
=============

USAHIHI: NI PAUL JAMES 'PJ' PEKEE NDIYE ALIYETHIBITISHA KURUDI CLOUDS MEDIA GROUP MPAKA SASA. GERALD HANDO BADO YUPO E-FM RADIO.
 
Yawezekana ni ushamba wangu au umri, binafsi baadhi ya vipindi vingi vya Clouds FM sioni maudhui yake na faida chanya za kuijenga jamii yetu na kwa maendeleo ya taifa. Nadhani wangepewa nafasi ya kupromoti sanaa tuu, vingine waachie wengine
 
Ubaoni e fm wapo vzuri ila jahazi ni matangazo tu kama bango ya tbc
 
Reactions: Lee
Niliwahi kumsikia Joseph Kusaga anasema yeye kwenye Ajira zake za Utangazaji huwa haangalii suala la Elimu anachokiangalia ni kipaji chako hata kama umeishi la Saba.

Naamini ndio ukweli wenyewe na wengi wameamua kufuata mtindo huo wa kuangalia vipaji zaidi na sio Elimu, ndio maana tunawasikia Wakina Mpoki, Zembwela, Gigy money japo sijui huyu waliangalia kigezo gani n.k

Wameona kwa wenzao wakenya na wao wanaangalia Kipaji zaidi kuliko elimu ndio maana Redio zao nyingi zimejaa wachekeshaji.


Ubaya wetu tumebaki kuwaangalia wale wale tu na hivyo tunakuwa kama tunawagombania badala ya kuibua hawa ambao wana elimu lakini pia wana kipaji ambao wamekosa watu wa kuwashika mkono.
 
Zembwela anajua anachokifanya ni moja kati ya watangazaj wanaojitambua huwez kumweka level za kina gigy
Zembwela sio mtangazaji, ni muongeaji kwenye radio, nikama hao kina gigy money sijui na kida Idrisa na wengine wanao fanania hivyo, utangazaji ni fani lazima ukasomee. utangazaji ni fani kama udakitari na ualimu, kuna ethics zake, kufanya kazi kwenye kituo cha habari hakikufanyi kuwa mwanahabari. Kama kuna mtu ameingia kwenye field ya habari kutokana na umashuhuri wake au namna yoyote kisha akaona kuna future ndani ya habari, inabidin afanye maarifa ili aingie darasani kusomea hiyo kazi.
 
Kama uongozi wa Clouds unaendeshwa sijui kwa kujuana au kifamilia bila ujuzi na hata kuweka vichwa vingine wawaletee mazuri, wataendelea kutapa tapa tu na kutumia wa enzi. Naona EFM inaelekea kupata wasikilizaji wengi zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…