Dindilimunyo
Senior Member
- Sep 12, 2016
- 108
- 206
Wakuu salamu.
Inasemekana PJ wamerudi tena Clouds fm. Waliondoka kwa mbwembwe sana kwenda Efm japo kwa maoni yangu hawakufanikiwa kufanya kile nilichotarajia! Lakini leo asubihi katika nyapia nyapia zangu pale Efm inasemekana PJ amekabidhi barua ya kuacha kazi na leo asubuhi ameonekana Clouds fm.
Hoja yangu ya msingi: Je, Radio za Tanzania zimekosa kabisa kutengeneza damu mpyaa hadi kugombania watangazaji wale wale ambao kimsingi hawana jipya?
Niliona usajili wa Gadner pale Clouds kutoka Efm nao haukuleta jambo jipya sana kwenye jahazi! Ukiangalia kitakwimu bado Ubaoni ya Efm ndio yenye wasikilizaji wengi kwa mujibu GO nyakati za jioni. Ilitosha kwa Clouds kujifunza hilo kwamba sasa wanapaswa kuamini damu mpya.
Kingine cha kusikitisha kwenye radio hizi zimebakia kugombania watu maarufu na huku wenye taaluma hii wakiwa mtaani hawana kazi mfano mtu kama Gigy Money anakuwa mtangazaji kwa elimu ipi na kwa taaluma ipi?
Radio zetu hizi kubwa za Dar zinapaswa kuwaamini na kuwapandisha madaraja watangazaji wa Mikoani ambao ni wazuri kuliko hawa mjini wanao wasumbuaa.
Nimejiuliza sana mikataba ya hawa watu ipoje kama PJ ameweza rudi Clouds kijanja janja hivi na hata miaka miwili haijaisha.
=============
USAHIHI: NI PAUL JAMES 'PJ' PEKEE NDIYE ALIYETHIBITISHA KURUDI CLOUDS MEDIA GROUP MPAKA SASA. GERALD HANDO BADO YUPO E-FM RADIO.