Mtangazaji Paul James 'PJ' arejea Clouds FM

Dah... wangekuwa na akili ya kujitambua wangeanzisha radio yao
Division of labour...sio lazima Ronaldo, Messi, Thiery Henry au Pele waanzishe timu zao ndio tutukuze mchango wao kwenye tasnia ya Soka.
 
kama wamerudi itakuwa poa mile kipindi kilipwaya sana Masood hana uelewa mpana Sizya mleta magazenga anamfunika
Ni dhambi kumlinganisha KP na yule dogo...KP yupo njema ingawa kwangu Hando yupo njema zaidi ya KP.

Huyo Dogo siza kuongea kwenyewe ni shida, R na L, Za na Dha zinamsumbua, na sauti yake si ya redioni kabisa...huwa natamani awe anaandika pointi zake wenzake wasome.
 
Habari ndugu zangu,

Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia watangazaji ambao awali waliikimbia clouds au hata walifukuzwa, sasa wanarudi. Mfano mkubwa ni Kepten Gadner habash na poul james a.k.a PJ.

Pia tumeshuhudia mtangazaji mashuhuri wa singeli Kicheko mtata akiihama E FM na kwenda Clouds.

Sasa swali langu mimi ni kwamba, je huu ni mchezo mchafu wa clouds kuuwa E Fm, au ni kwamba E FM hakuna maslahi mazuri au hasa ni nini tatizo?



 
Kila mtu ana sababu yake na kubwa zaidi ni mambo ya kibiashara tuu.
Sema nahisi Clouds wameona Efm wanavo kuja juu ndio na wenyewe wanapambana
*lipumba mwenyewe karud CUF sembuse hao watangazaji tu jamani! Hata si shda hiyo
 
Wakati huyu PJ kahamia E fm , nilikuwa namkuta maeneo ya nyuma ya clouds anakunywa pombe pale mchana huku akiwa kazungukwa na majamaa kibao wa clouds. Nikawa najiuliza huku ndio kuhama gani? Kwenda kuka E fm na kuja kushinda ckouds
 
Ni wachache sana wenye ujuzi wa habari wengi wao ni wasema chochote kama mc hata kama hawana uakika na habari utasikia anaiachia tu bila kujali effects zinazoweza kutokea kwake,kwa mwajiri wake na jamii kwa ujumla kwa kutoa taarifa zisizo sahihi. Sijaelewa ila vituo vingine vmekuwa kibiashara zaidi taaruma wameweka pembeni,na watangazaji wao wakishapata majina wanazani wamepata kila kitu. yaani most of them wako empty juu ya mambo yanayendelea kwenye jamii zaidi zaidi wanategemea sana mitandao,unakuta kitu kimepostiwa JF wao ndo wanakitangaza kama ndo wamekitafuta. Yaani hawako tayari kujifunza wamelewa umaarufu tu.Dah ukiangalia vyombo vya habari vya nchi nyingine hasa zilizoendelea ndo utangundua tofauti yatu na wao yaani ni aibu tupu.
 
Wakati huyu PJ kahamia E fm , nilikuwa namkuta maeneo ya nyuma ya clouds anakunywa pombe pale mchana huku akiwa kazungukwa na majamaa kibao wa clouds. Nikawa najiuliza huku ndio kuhama gani? Kwenda kuka E fm na kuja kushinda ckouds
Kwani waligombana?
 
Kwenye hii Tasnia, tumwache tu mzee Mengu Ntuyabaliwe afanye yake...
 
Huyu jamaa anakipi kipya zaidi ya kusoma magazeti?
Tusimalize kusema yote. Hatufahamu nyuma ya pazia...... Japo kweli PJ sauti yake ina mvuto... Sio tu kwenye magazeti hata kwenye kipindi cha michezo zamani alivyokua akitangaza..... Tushaambiwa huo mchezo hauitaji hasira.
 
Kama uongozi wa Clouds unaendeshwa sijui kwa kujuana au kifamilia bila ujuzi na hata kuweka vichwa vingine wawaletee mazuri, wataendelea kutapa tapa tu na kutumia wa enzi. Naona EFM inaelekea kupata wasikilizaji wengi zaidi
Tatizo hawajasamba Tanzania nzima
 
redio mpya inabidi zije na watangazaji wapya sio kwa kuchukua wale wa redio zenye mashabiki wengi na kutembea kwenye nyota ile ile ya wenzao mfano efm hawakuwa na haja ya kumchukua pj kusoma yale yale magazeti aliyokuwa anasoma clouds then unaita creativity hiyo cio creativity bali ni copy and paste
 
Naona vinyago walivyovichonga wao wenyewe vinawatisha. Ila mfa maji haachi kutapatapa.
 
Point
 
Clouds
Leo Tena
XXL
Jahazi
Makele matupu tangu mwanzo mpaka mwisho,hakuna content yoyote
Iyo leo tena naonaga wanapiga story zao tu....i love power breakfast
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…