TANZIA Mtangazaji Swedy Mwinyi wa TBC afariki Dunia

TANZIA Mtangazaji Swedy Mwinyi wa TBC afariki Dunia

Ahmed Jongo
Ezekiel Malongo
Halima Mchuka
Sued Mwinyi

Mlifanya matangazo ya mpira na kioinfi cha michezo RTD kuwa moto sana!!
Nazeeka sasa

Pumzikeni kwa amani Ma-Legend
Hawa miamba wameitumikia Tasinia ya Habari ipasavyo.
 
Pana Mtangazaji mmoja alikua anatangaza Mwanza nae alifariki Mbeya simkubuki jina alikua anaweza kutangaza kikosi cha Tipso wa lindanda akiwa anawaona wanatroti tu wenyewe walikua wanasema naona Wachezaji wanapasha misuri joto pale au wanapiga njalamba pale...
Dominic Chilambo.

Alifariki akiwa anatangaza mpira kati ya Tukuyu Star vs Yanga/Simba.
Kipindi cha michezo saa moja na nusu RTD Halima Mchuka akatangaza kifo chake kwa masikitiko makubwa sana akiwa ameweka wimbo flani hivi na kisha kuweka sauti ya mwisho ya Chilambo akiwa anatangaza hiyo match.
 
Dominic Chilambo.

Alifariki akiwa anatangaza mpira kati ya Tukuyu Star vs Yanga/Simba.
Kipindi cha michezo saa moja na nusu RTD Halima Mchuka akatangaza kifo chake kwa masikitiko makubwa sana akiwa ameweka wimbo flani hivi na kisha kuweka sauti ya mwisho ya Chilambo akiwa anatangaza hiyo match.
Yap ni Mzee Chilambo ila alifariki siku chache mbele baada ya kutangaza mechi ya Yanga vs Simba zilichezea Mbeya na ni kweli kipindi cha michezo tulisikiliza sauti yake kwa mara ya mwisho kwa mechi hiyo na nakumbuka maana nilikuwepo Uwanja wa Sokoine pale...kabla haya maandishi ya Mwalimu JK hawajafuta..
"NCHI MASIKINI HAIWEZI KUENDELEA KWA KUTEGEMEA MISAADA KUTOKA NCHI ZA NJE"
JULIUS NYERERE.
wahuni wamefuta hayo wameweka ya kwao...
 
Taarifa inayosambaa mitandaoni inaeleza kwamba, Mtangazaji wa TBC, Sued Mwinyi amefikwa na Umauti leo, kwenye Hospitali ya Mloganzila ambako alilazwa kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua.

Apumzike kwa Amani

View attachment 2988858
asante kwa taarifa hii

Moja ya simulizi za maisha yetu na Sued Mwinyi.

Tukiwa ndiyo mwanzo mwanzo tumejiunga na rtd mimi, Sued Mwinyi na Pascal Mayala baada ya kumaliza mafunzo yetu ya utangazaji pale mjengoni tukapelekwa idhaa ya biashara, mkuu wa idhaa akiwa Mikidadi Mahamoud na wasaidizi wake Sekione Kitojo, Salama Mfamao(Rip)na Siwatu Luanda(Rip).

Pascal akapewa kipindi cha Karibu Vijana kinatoka saa 10.45-11.00 jioni. Sued akapewa Salam Mkulima na mimi nikapewa kipindi cha Pole kwa Kazi(11.05-12.00 jioni).

Wakati ule vipindi hivyo vyote ni recorded yaani vinatayarishwa mapema na kuja kurushwa baadaye.

Sued alikuwa shabiki mkubwa wa muziki wa Reggae, Pascal yeye ngoma za kizungu za kuruka majoka na mimi nikihusudu sana mabolingo.

Basi katika vipindi vile vyetu ambavyo nilikuwa vya salaam, Sued akawapigia wakulima Reggae tupu, Pascal yeye kwa vijana alibakia Marekani na mimi katika pole kwa kazi nikawapa pole wafanyakazi kwa mabolingo mtindo mmoja.

Vipindi vilivyomalizika kwenda hewani siku ya pili yake wakuu katika kikao chao chini Mkurugenzi David Wakati(Rip) wakatufanyia tathmini na kuona kuwa tulikuwa hatuna utaifa na uzalendo kwa utamaduni wetu.

Basi tukahamishwa haraka sana.Mimi nikapelekwa idhaa ya taifa chini ya Fauziyat Ismail Aboud, Sued nadhani akarudishwa External Service( sote watatu tulianzia huko) na Pascal akapelekwa kitendo cha ngoma zetu akapewa kipindi cha tuimbe sote na ngoma zetu bosi wake akiwa Khalid Ponera na Msaidizi wake Michael Katembo.

Hapo kwangu ndiyo ukawa mwanzo wa kuzijua na kuzipenda nyimbo za bendi zetu kwa sababu nilipewa kuandaa kipindi cha mchana mwema, Jambo na jioni njema.

Pascal Mayala mpaka leo anazijua sana ngoma za makabila yetu pamoja na kwaya za shule ya msingi ya Khana Tanga.

KWAHERI SUED MWINYI
C&P
Abubakar Liongo

Ni ngumu sana kusimulia maisha ya mwenziyo mliyoanza pamoja maisha na sasa ametangulia mbele ya haki.
Sued Ramadhan Mwinyi tuliajiriwa siku moja pale RTD June 1989. Mwengine ni Pascal Mayalla. Baadaye tukaanza kozi ya utangazaji hapo hapo RTD tukijumuika na Bakari Msulwa, Eshe Muhiddin,Nyambona Masamba, Shida Wazir,Kassim Mikongolo(rip) kwa uchache niliyowakumbuka.
Lakini ilitokea sisi watatu, Sued,Pascal na mimi tukawa maswahiba sana. Kuna mengi sana ya kusimulia kuhusu ndugu yangu huyu. Nakumbuka siku ya harusi yangu 1996 Sued alivaa suti akisema ni mara yake ya kwanza kuvaa suti pale Pool Side Kilimanjaro Hotel(now Kempiski).
Nyambona Massamba kwa niaba ya mwenzangu Pascal Mayalla tunakupa asante na hongera sana kwa kusimamia matibabu ya mwenzetu(utatu wetu) hadi umauti ulipomfika.
Sued umetangulia sehemu ambako swahiba wetu aliyetupokea External Service Mohamed Dahman atakupokea tena japo mara hii ukiwa peke yako bila ya Pascal Mayalla na Aboubakary Liongo.
Utapokelewa pia na Nadhir Mayoka, Salama Mfamao, Siwatu Luanda, Sara Dumba,Kassim Mikongolo,Hassan Mkumba, Hendrik Libuda, Ahmed Jongo,Khalid Ponera, Tumbo Risasi, Julius Nyaisanga na wengine.
Mwenyezimungu akuondolee adhabu ya kabri, akusamehe makosa yako.
IKO SIKU ISIYO NA JINA TUTAONANA HUKO ULIKOTANGULIA
C&P About
Abubakar Liongo
Pole sana Chief @⁨Abou Liongo⁩ , na asante sana kwa kumbukumbu hii ya enzi zetu. Batch yetu ya Watangazaji 10, wanaume 5 na wanawake watano. Swedy Mwinyi, Abubakar Liongo, Bakari Msulwa, Kassim Mikongolo na mimi Pascal Mayalla. Wanawake ni Eshe Muhidin, Shida Waziri, Nyambona Masamba, Jane Rutaserwa na Rose Japhet. Batch yetu ndio iliyokuwa batch ya mwisho ya watangazaji kuajiriwa enzi za Mkurugenzi David Wakati. Abou Liongo na Swedy Mwinyi ndio watangazaji wa kwanza wa umri mdogo kusoma habari RTD. Ikatoea Mimi, Swedy na Abou, kuwa marafiki wa karibu na kuanza kutembeleana home. Swedy alipofiwa na mama yake, tulisindikiza Morogoro kuzika, Swedy alipofiwa na baba yake, tulishiriki bega kwa bega kuzika, sasa leo tunakutana tena kumsindikiza mwenzetu tuliyeanza naye kazi siku moja. Ni huzuni kubwa!. Innalillah wa inna illah Raajiun!.

Pascal Mayalla
 
Back
Top Bottom