Mtangazaji wa Clouds alalamikia kutishiwa na Haji Manara

Ukweli Manara ukiwa unawakilisha team kubwa ni lazima ujicontrol ni kweli alimtishia na alikuwa anaendesha press kama kijiwe cha kahawa sio lazima kila mtu akupende swali jibu bila jazba wala matusi na mbaya zaidi alikuwa anatumia lugha chafu katika press ya team kama Simba neno Kudadadeki hii sio sawa haya mambo uneweza kuongea off sio live na zaidi lazima uwaheshimu wenzako hata kama unajuwa wana njaa ila heshima muhimu. Alitamka tena wewe nakutafuta sana kaingiza personal issues katika club ya Simba. Kazi ya mwandishi kukuliza maswali ya kukuudhi ufunguke sasa angeenda Hardtalk si angerusha ngumi huyu.
 
Kama huna doa juu yake fuata taratibu za kusuluhishana naye sio mbele ya watu wengi.
Watumie wanaomtumia kumpa jeuri.
 
Kwani angejibu ni kweli Yanga wamekuwa na matokeo mazuri kidogo katika mechi 3 za mwisho lakini sisi tunajuwa ni bora kuliko Yanga kwa kuwa tunategemea kuwa mabingwa mara 4 mfululizo hata JKT Ruvu wamekuwa wanatusumbua kidogo lakini haiwafanyi wao kuwa bora na sisi tumejipanga kuwaonesha nani bora Jumamosi kuwafunga na kuifanya sherehe ya ubingwa kunoga zaidi kwa kwa kuwafunga Yanga. Mechi zilizopita hazina ushawishi tena ni wiki hii kuwafunga na kuwaweka sehemu wanayostahili. Haya majibu tosha kabisa..
 
Manara ana matatizo!

Alipaswa aambatane na Mkude kwenye vipimo vya afya ya akili.

Kwa Nini asingesema mapema press conference yake anawaalika waandishi mashabiki wa Simba pekee?

Kila mwandishi anayeandika kisichompendeza Manara anakuwa adui.

Waandishi wangepotezea tu hizo press zake kumshusha mabega.
 
Hardtalk hiki kipindi ni noma! Jakaya alishawahi hojiwa aiseeee! Alipigwa maswali hadi akawa na kigugumizi!

Sent using Jamii Forums mobile app
Wazungu kimtaani kusema https://jamii.app/JFUserGuide sio tusi ni kama neno la kawaida lakini wakiwa kwenye media live ikitokea mtu katumia neno hilo kwa bahati mbaya basi wanaomba radhi au wanakata matangazo sio kwamba neno lile hawatumii nje wanatumia sana ila huyu Manara katumia neno KUDADADEKI zaidi ya mara moja lakini anaona sawa tu hata kuomba msamaha hili neno sio mahala pake.
 
Mkuu kama shida ni huyu dada ni bora umzuie asiingie kwenye ukumbi. Au pia Simba na Yanga ziwe zinaita waandishi ambao ni mashabiki wao tu.
Hakika Mkuu na Hapa Tuangalie Bad reputation aliyoifanya Haji Kwa Huyo Dada ingawa Huyo Dada Nae Ni kimbelembele sana kutoa habari za Simba na Kuwasifia
....
Unadhani Angekuwa Msemaji Wa Yanga au Msemaji Wa Azam Angeweza Kujibu Majibu Kama Ya Haji? Hata Kama Umeulizwa swali Ambalo haulipendi ww Ungemjibu Tu.
....
Mkuu Kama ulivyosema Hapo Juu, kama shida ni waandishi Wa Hii bad ni bora haji na SSC wawazuie wasiingie kwenye ukumbi.
....
Au pia Simba na Yanga ziwe zinaita waandishi ambao ni mashabiki wao tu.
 
Kinachoshangaza ni hao waandishi wengine wanaocheka.

Hata hawajui kama kuna shida kwa hicho anachofanya Manara.

Swali aliloulizwa hua tunaona makocha wa ligi za Ulaya wakiulizwa na hua wanajibu. Kocha hata kama amekasirishwa na swali kuna namna atajibu na wengi husema "Timu hiyo inategemea bahati" " Marefa hua hawako fair kwenye maamuzi ya 50/50"

Kimsingi ni kwamba hua linajibiwa swali la hivyo. Bado naamini hizi timu za Tz kua na wasemaji kwa ishu za kiufundi kama hizi ni upuuzi.
 
We acha upumbavu hamws nhende yupo hai sio marehwmu,anaishi mwanza
 
Ukileta umalaya wako lazima uwakiwe tu
 
Acha yawakumbe,alishaonya Shaffii Dauda akapuuzwa,Manara ni wa kudhibitiwa,anatumia kivuli cha mapungufu yake (albinism) na kivuli cha Simba kutenda anayotenda(kero,kauli chafu,kuchafua brand za watu,utoto na matatizo lukuki,jamii elevu ya wapenda soka nchini tunajua haya masuala ),kisaikolojia ku_behave hivi kwa mapungufu aliyonayo inamsaidia kutoonekana dhaifu ktk jamii,ila mbali na yote hayuko sawa kwa %[emoji817],ukimezwa na mahaba ya U_simba huwezi elewa nazungumzia nn,Simba SC mpelekeni Manara alipopelekwa Mkude haraka akapimwe...
 
Waandishi wamemlea sana huyo jamaa kila siku anawatukana kuna kipindi alimtukana Shafih, akawatukana E-Fm walifanya interview na Manura , akawatukana Wasafi juzi kati kawatukata wachambuzi akawaita taka taka, kipindi kile cha visit kidimbwi alishambulia Jemedari Said cha ajabu bado wana cheka nae tu
 
Naona mnamtetea huyo Prisca, inaonekana kuna shida kweli hawezi kuwakiwa bure tu kulikuwa na wangapi wasiwakiwe awe yeye tu. Japo kumuwakia mbele ya hadhara haikuwa poa.
 
Uchaguzi wa TFF umeingiliwa na Siasa, JIWE ndiye alipandikiza wanasiasa na sasa tunakula wa chuya.
1. Karia ni SIMBA.
2. Clouds ina U-YANGA kupita maelezo na ipo wazi.
3. Mwanamke wa clouds ni mwandishi wa gazeti la michezo la Yanga na alikuwa ametumwa kutibua mkutano na taarifa zilikuwa zishamfikia Manara mapema kabisa.
 
Tuache ushabiki. Manara ni mpuuzi. Huo ni udhalilishaji.
Matokeo ya yote haya ni kukosa standards na professionalism kwenye nchi yetu. Tunafanya mambo kienyeji kwenye mambo nyeti. Tunamuhitaji sana Manara kama klabu kutokana na uwezo wake wa kuhamasisha mashabiki, lakini ni muda sasa viongozi ndani ya klabu kumkanya, kumpa muongozo na ikiwezekana msaada wa kisaikolojia wa namna ya kudhibiti jazba pindi anapoulizwa maswali na waandishi wa habari ambayo hayampendezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…