Mtangazaji wa Clouds alalamikia kutishiwa na Haji Manara

Mtangazaji wa Clouds alalamikia kutishiwa na Haji Manara

Acheni kushabikia mambo ya kijinga,nje ya Simba na Yanga sote ni Watanzania,sote ni binadamu.Alichokifanya Haji si cha kiungwana. Michezo ni furaha na Upendo si uadui.
Safi sana. Umeongea kama great thinker na aina ya mtu sahihi kuwepo JF. Bahati mbaya JF inabeba kila aina ya taka. Kuna comments mpaka unashangaa.
 
Kwani angejibu ni kweli Yanga wamekuwa na matokeo mazuri kidogo katika mechi 3 za mwisho lakini sisi tunajuwa ni bora kuliko Yanga kwa kuwa tunategemea kuwa mabingwa mara 4 mfululizo hata JKT Ruvu wamekuwa wanatusumbua kidogo lakini haiwafanyi wao kuwa bora na sisi tumejipanga kuwaonesha nani bora Jumamosi kuwafunga na kuifanya sherehe ya ubingwa kunoga zaidi kwa kwa kuwafunga Yanga. Mechi zilizopita hazina ushawishi tena ni wiki hii kuwafunga na kuwaweka sehemu wanayostahili. Haya majibu tosha kabisa..
Ukiwa msemaji hautakiwi kuwa na hasira.

Kwani jamaa (Manara) ana taaluma ya uandishi wa habari au taaluma yoyote inayohusiana na mawasaliano ya umma?
 
Manara hana professionalism..... Huwezi ku-attack mwandishi tena ukisema nilikuwa nakutafuta wewe na nitakudhalilisha. Huwezi kuleta mambo personal kwenye press conference ya taasisi. In short anaikosea adabu Simba.
 
Acheni kushabikia mambo ya kijinga,nje ya Simba na Yanga sote ni Watanzania,sote ni binadamu.Alichokifanya Haji si cha kiungwana. Michezo ni furaha na Upendo si uadui.
Mkuu hivi umesoma vyema kweli maelezo tokea mwanzo mpaka mwisho? Haji kaanza kupanic kabla hata ya kuongea huyo Prisca. Lilipoulizwa swali juu ya wastani mzuri wa Yanga kupata matokeo kwa kuangalia mechi tatu za mwisho ndipo Haji akachafukwa
 
Ukiwa msemaji hautakiwi kuwa na hasira.

Kwani jamaa (Manara) ana taaluma ya uandishi wa habari au taaluma yoyote inayohusiana na mawasaliano ya umma?
Mimi sijui taaluma yake hilo swali wangeulizwa waliomuajiri vigezo vyao, mimi nasema haijalishi wewe umesomea nini lakini unapowakilisha taasisi kubwa basi ni lazima ujiheshimu na uheshimu wengine ni simple logic wala haihitaji degree.
 
P R I S C A - K I S H A M B A !
- Mwandishi / Mtangazaji wa clouds fm ametishiwa kudhalilishwa na msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara.

"KOSA LANGU NINI ? Leo nilikuwa sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa klabu ya Simba SC na waandishi wa habari za michezo mkutano ambao uliongozwa na Haji Manara"

"Baada ya mkutano kumalizikiza Haji aliporuhusu maswali kwa waandishi waliokuwepo miongoni mwao waliouliza maswali ni mwandishi wa habari ABDUL DUNIA"

"Alimuuliza Haji 'Rekodi za michezo (3) ya mwisho kati ya Simba na Yanga ya ligi kuu inaonesha Yanga ilikuwa na wastani mzuri wa kupata matokeo mazuri dhidi ya Simba, huoni kwamba kwa rekodi hii ubora wenu uko kwa timu zingine na sio kwa YANGA ?"

"Haji Manara aliwaka sana na kumshushia maneno mwandishi yule na kumtuhumu kuwa yeye ni shabiki wa Yanga na ametumwa na Yanga,, akamwambia siku zingine akienda kwenye PRESS awe na maswali ya kueleweka na sio maswali UCHWALA"

"Baada ya Haji kuwaka nikanyoosha mkono kumuuliza Haji kuwa, ni vyema kwa kuwa umetoa nafasi kwa watu kukuuliza maswali ujibu kwa kuwa swali hilo lilikuwa na lengo zuri tu"

"Kama kawaida Haji Manara alitumia mkutano huo uliokuwa live kwenye television na blogs mbalimbali kuniambia maneno ya VITISHO akiahidi KUNIDHALILISHA kwani anadai ana SMS zangu nyingi ambazo sio nzuri alisema..."

"Kaa kimya wewe, tena wewe ndio nilikuwa NAKUTAFUTA kwa muda mrefu, NITAKUDHALILISHA, hapa nina SMS zako huna adabu unanivunjia heshima kwenye press zangu kama nani ?! Alisema Manara dhidi yangu"

"Mkutano ulipoisha Manara alipita na kunifuata nilipokuwa nimesimama akarudia tena akiahidi KUNIDHALILISHA siku moja huku akininyooshea kidole usoni"

"Nilijisikia vibaya kama binadamu, wakati huo alikuwa anatoka nje akiwa ameambatana na watu kadhaa, nilitoka nje ya ukumbi kumfuata na kumuita, nikamwambia 'Haji naomba usimame,, nikamwambia kwa nini kila kunapokuwa na hadhara ya watu huwa unatishia KUNIDHALILISHA ?! Niwapi nilikukosea ?

"Nikamwambia naomba tumia fursa hii kuwaonesha waandishi hizo SMS zangu unazosema ni mbaya"

"Haji alinisogelea na kutaka KUNIKUNJA mbele ya UMMA wa Waandishi wa habari, waandishi kadhaa waliokuwepo wakawahi kumshika nami akanishika kaka anaitwa JACKSON kutoka NCARD kitengo cha mauzo aliyekuwa sehemu ya mkutano ule pamoja na MUSSA MWKISU na wengine waliokuwepo"

"Hii sio mara ya kwanza Haji kutumia jukwaa la watu KUNIDHALILISHA, ameshafanya hivyo kwenye group moja la WHATSAPP la Taifastars kwa kuniita majina yasiyofaa"

"Nitafikisha ombi hili kwenye ofisi ya muajiri wangu kuandika barua kwenda uongozi wa SIMBA SC. Haji amenitishia mara kadhaa nikiwa kwenye majukumu yangu, ametishia KUNIDHALILISHA hata kupitia mitandao ya kijamii"

"Manara asitumie umaarufu wake, asitumie kivuli cha klabu yake ya Simba kutaka kuwadhalilisha watoto wa kike"

🔍 Prisca Kishamba
View attachment 1836334
Ipo shida hapa hii nafasi ya Hajji inahitaji hekima, busara, ukomavu na ustahimilivu, angeweza kujibu hilo sijibu ni swali la uchokozi, sipo tayari kukuudhi kwenye hadhara. Kama mwana Simba this has been outright thoughts. Japo nyuma ya pazia kama kuna namna ni maadui wa Simba angewachana nyie ni chawa wa Utopolo bora nisijibu nikikujibu utaudhika. #Hajji_Manara_Reform_Behave_Professionally_with_Perseverence.
 
Manara ni kielelezo kuwa kuna watu wasio sahihi kwenye nafasi muhimu.

Pia uongozi wa Simba kushindwa kuchukua hatua yoyote kwa Manara muda wote inaonyesha wao ni wa ovyo pia.

Madhaifu ya ki-uongozi ya hizi timu zetu yanafichwa sana na matokeo ya uwanjani zaidi ya hapo hakuna jipya wanafanya.
 
Leo Haji Yupo EFM Radio live kwenye kipindi cha Sports HQ
 
Ukiwa msemaji hautakiwi kuwa na hasira.

Kwani jamaa (Manara) ana taaluma ya uandishi wa habari au taaluma yoyote inayohusiana na mawasaliano ya umma?
Mawasilianao ya madrasa
 
Kwani angejibu ni kweli Yanga wamekuwa na matokeo mazuri kidogo katika mechi 3 za mwisho lakini sisi tunajuwa ni bora kuliko Yanga kwa kuwa tunategemea kuwa mabingwa mara 4 mfululizo hata JKT Ruvu wamekuwa wanatusumbua kidogo lakini haiwafanyi wao kuwa bora na sisi tumejipanga kuwaonesha nani bora Jumamosi kuwafunga na kuifanya sherehe ya ubingwa kunoga zaidi kwa kwa kuwafunga Yanga. Mechi zilizopita hazina ushawishi tena ni wiki hii kuwafunga na kuwaweka sehemu wanayostahili. Haya majibu tosha kabisa..
Hivi ni kweli mechi tatu za ligi za mwisho yanga aliibuka kinara?.
 
Back
Top Bottom