Mtangazaji wa Clouds alalamikia kutishiwa na Haji Manara

P R I S C A - K I S H A M B A !
- Mwandishi / Mtangazaji wa clouds fm ametishiwa kudhalilishwa na msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara.

"KOSA LANGU NINI? Leo nilikuwa sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa klabu ya Simba SC na waandishi wa habari za michezo mkutano ambao uliongozwa na Haji Manara"

"Baada ya mkutano kumalizikiza Haji aliporuhusu maswali kwa waandishi waliokuwepo miongoni mwao waliouliza maswali ni mwandishi wa habari ABDUL DUNIA"

"Alimuuliza Haji 'Rekodi za michezo (3) ya mwisho kati ya Simba na Yanga ya ligi kuu inaonesha Yanga ilikuwa na wastani mzuri wa kupata matokeo mazuri dhidi ya Simba, huoni kwamba kwa rekodi hii ubora wenu uko kwa timu zingine na sio kwa YANGA ?"

"Haji Manara aliwaka sana na kumshushia maneno mwandishi yule na kumtuhumu kuwa yeye ni shabiki wa Yanga na ametumwa na Yanga, akamwambia siku zingine akienda kwenye PRESS awe na maswali ya kueleweka na sio maswali UCHWARA"

"Baada ya Haji kuwaka nikanyoosha mkono kumuuliza Haji kuwa, ni vyema kwa kuwa umetoa nafasi kwa watu kukuuliza maswali ujibu kwa kuwa swali hilo lilikuwa na lengo zuri tu"

"Kama kawaida Haji Manara alitumia mkutano huo uliokuwa live kwenye television na blogs mbalimbali kuniambia maneno ya VITISHO akiahidi KUNIDHALILISHA kwani anadai ana SMS zangu nyingi ambazo sio nzuri alisema..."

"Kaa kimya wewe, tena wewe ndio nilikuwa NAKUTAFUTA kwa muda mrefu, NITAKUDHALILISHA, hapa nina SMS zako huna adabu unanivunjia heshima kwenye press zangu kama nani?! Alisema Manara dhidi yangu"

"Mkutano ulipoisha Manara alipita na kunifuata nilipokuwa nimesimama akarudia tena akiahidi KUNIDHALILISHA siku moja huku akininyooshea kidole usoni"

"Nilijisikia vibaya kama binadamu, wakati huo alikuwa anatoka nje akiwa ameambatana na watu kadhaa, nilitoka nje ya ukumbi kumfuata na kumuita, nikamwambia 'Haji naomba usimame, nikamwambia kwa nini kila kunapokuwa na hadhara ya watu huwa unatishia KUNIDHALILISHA ?! Ni wapi nilikukosea?

"Nikamwambia naomba tumia fursa hii kuwaonesha waandishi hizo SMS zangu unazosema ni mbaya"

"Haji alinisogelea na kutaka KUNIKUNJA mbele ya UMMA wa Waandishi wa habari, waandishi kadhaa waliokuwepo wakawahi kumshika nami akanishika kaka anaitwa JACKSON kutoka NCARD kitengo cha mauzo aliyekuwa sehemu ya mkutano ule pamoja na MUSSA MWKISU na wengine waliokuwepo"

"Hii sio mara ya kwanza Haji kutumia jukwaa la watu KUNIDHALILISHA, ameshafanya hivyo kwenye group moja la WHATSAPP la Taifa stars kwa kuniita majina yasiyofaa"

"Nitafikisha ombi hili kwenye ofisi ya muajiri wangu kuandika barua kwenda uongozi wa SIMBA SC. Haji amenitishia mara kadhaa nikiwa kwenye majukumu yangu, ametishia KUNIDHALILISHA hata kupitia mitandao ya kijamii"

"Manara asitumie umaarufu wake, asitumie kivuli cha klabu yake ya Simba kutaka kuwadhalilisha watoto wa kike"

[emoji368] Prisca Kishamba
View attachment 1836334
Haji Manara kuwa msemaji wa klabu kubwa kama Simba ni udhalilishaji. Huyu na Jerry Muro ni Waropokaji siyo Wasemaji.
 
Hadithi za mikia haziko objective. Issue ni udhalilishaji tena wa mtoto wa kike, embu tutumie akili zetu vizuri, na tarehe 3 lazima tutafune myama. Simba kwao porini.
Kila mtoto wa kike akielezwa ukweli inageuzwa kadhalilishwa.At the same time mnadai usawa. Huyo mwanamme aliyejibiwa hajadhalilishwa Bali Prisca.

Hizi ni dabo standadi za kijinga,jinsia fulani kuona hawawezi kukaripiwa.
 
Manara ni mkosefu, hafai kuwa simba uswahili umemjaa pomoni.
Anajikweza sana, mafanikio ya simba yanahitaji hela za MO, sio kelele za manara wanamvumilia tu.
Japo huyo dada naye yupo kwenye payroll ya GSM ni mchonganishi na mzushi, ila njia iliyotumiwa na haji sio sahihi.
Kama kweli huyo dada ni mchonganishi basi alistahili kujibiwa vile.
 
Uwenda Prisca kweli akawa na makosa,sina hakika kama kweli huyo dada anamakosa kwasababu sijayajua japo wadau wanasema yapo ila alichofanya Haji sio.
Haji anajazba za haraka sana pia ana madeko flani hivi yanayomfanya aongee chochote kinachomjia baada ya jazba zake kupanda.
Natamani Haji aombe radhi yeye ni msemaji wa Simba na press yake ilihusu kuelekea Kariakoo darby kwanini ameingiza personal issue na vitisho kwa wanahabari!.
 
Prisca na yule bishoo wa kiume tunajua walikua wanaitaka nafasi ya Haji pale msimbazi ndio bifu lilipoanzia..
 
Ukweli Manara ukiwa unawakilisha team kubwa ni lazima ujicontrol ni kweli alimtishia na alikuwa anaendesha press kama kijiwe cha kahawa sio lazima kila mtu akupende swali jibu bila jazba wala matusi na mbaya zaidi alikuwa anatumia lugha chafu katika press ya team kama Simba neno Kudadadeki hii sio sawa haya mambo uneweza kuongea off sio live na zaidi lazima uwaheshimu wenzako hata kama unajuwa wana njaa ila heshima muhimu. Alitamka tena wewe nakutafuta sana kaingiza personal issues katika club ya Simba. Kazi ya mwandishi kukuliza maswali ya kukuudhi ufunguke sasa angeenda Hardtalk si angerusha ngumi huyu.
Manara ana madhaifu mengi sana, inabidi afahamu anawakilisha Simba brand kubwa, mambo ya kwenye kahawa ayaache uko uko
 
Kakudhalilisha vipi ama kakuambia kuwa una sura mbaya na ngumu. Haukuona cha kufanya mpaka umekimbilia kuandika habari za soka! Vumilia huko ni pagumu sana kupigwa nje nje acha matusi. Muulize marehemu James Nnende alivyopigwa ndoga na Mogela. Ukiandika Siasa ujue pia utauliwa tu. Kila kazi ni ngumu hata ukienda kulima panya na nyani watakula mazao yako. Tuachie Lunyasi yetu. Ndio una sura mbaya hali ubishi..na waandishi nyie mna njaa sana uenda uliomba hela kwa Haji.
Haji kakosea lazima aambiwe ukwelii!
Asijione yupo juu ya wote
Busara na weledi vitumike!
Nani anajiumba au anachagua awe na sura soft!
Yeue mwenyewe mlemavu wa ngozi hana adabu
 
Sikutegemea mwalimu wa Madras anaweza kuwa na mapungufu ya kinidhamu kiasi hiki Sasa watoto wanajifunza nini kwake!!!
 
👇
Manara akimchamba Prisca kwenye Press leo_laughing__laughing_ ( 640 X 640 ).jpg
 
Ukiona kiongozi (public figure) anatumia lugha mbaya kwenye press conference huyo hafai, anaweza kuwa ana over-confidence", kitu ambacho ni hatari!

Kuna siku nilipata concept kutoka kwa mwandishi wa habari miaka hiyo, ambapo vyombo vya habari vilikuwa hot.

Alisema hivi "Unakuta unampigia mtu fulani kumuuliza tuhuma fulani ili akupe habari lakini hapokei simu au anatukana"

Kitendo cha kutopokea simu au kutukana hizo ni habari pia. Zitaandikwa hivo hivo, kwamba, "alipopigiwa simu, simu yake iliita bila kupokelewa" au "Alipigiwa simu, lakini hakutoa ushirikiano kwa mwandishi".

Maana yangu ni kwamba, unapokuwa msemaji wa timu, kazima utaulizwa maswali ya kuudhi, hivyo ni lazima uwe mpole na ku-relax. Hakuna haja ya kukimbia maswali wala kupanic.
 
P R I S C A - K I S H A M B A !
- Mwandishi / Mtangazaji wa clouds fm ametishiwa kudhalilishwa na msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara.

"KOSA LANGU NINI? Leo nilikuwa sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa klabu ya Simba SC na waandishi wa habari za michezo mkutano ambao uliongozwa na Haji Manara"

"Baada ya mkutano kumalizikiza Haji aliporuhusu maswali kwa waandishi waliokuwepo miongoni mwao waliouliza maswali ni mwandishi wa habari ABDUL DUNIA"

"Alimuuliza Haji 'Rekodi za michezo (3) ya mwisho kati ya Simba na Yanga ya ligi kuu inaonesha Yanga ilikuwa na wastani mzuri wa kupata matokeo mazuri dhidi ya Simba, huoni kwamba kwa rekodi hii ubora wenu uko kwa timu zingine na sio kwa YANGA ?"

"Haji Manara aliwaka sana na kumshushia maneno mwandishi yule na kumtuhumu kuwa yeye ni shabiki wa Yanga na ametumwa na Yanga, akamwambia siku zingine akienda kwenye PRESS awe na maswali ya kueleweka na sio maswali UCHWARA"

"Baada ya Haji kuwaka nikanyoosha mkono kumuuliza Haji kuwa, ni vyema kwa kuwa umetoa nafasi kwa watu kukuuliza maswali ujibu kwa kuwa swali hilo lilikuwa na lengo zuri tu"

"Kama kawaida Haji Manara alitumia mkutano huo uliokuwa live kwenye television na blogs mbalimbali kuniambia maneno ya VITISHO akiahidi KUNIDHALILISHA kwani anadai ana SMS zangu nyingi ambazo sio nzuri alisema..."

"Kaa kimya wewe, tena wewe ndio nilikuwa NAKUTAFUTA kwa muda mrefu, NITAKUDHALILISHA, hapa nina SMS zako huna adabu unanivunjia heshima kwenye press zangu kama nani?! Alisema Manara dhidi yangu"

"Mkutano ulipoisha Manara alipita na kunifuata nilipokuwa nimesimama akarudia tena akiahidi KUNIDHALILISHA siku moja huku akininyooshea kidole usoni"

"Nilijisikia vibaya kama binadamu, wakati huo alikuwa anatoka nje akiwa ameambatana na watu kadhaa, nilitoka nje ya ukumbi kumfuata na kumuita, nikamwambia 'Haji naomba usimame, nikamwambia kwa nini kila kunapokuwa na hadhara ya watu huwa unatishia KUNIDHALILISHA ?! Ni wapi nilikukosea?

"Nikamwambia naomba tumia fursa hii kuwaonesha waandishi hizo SMS zangu unazosema ni mbaya"

"Haji alinisogelea na kutaka KUNIKUNJA mbele ya UMMA wa Waandishi wa habari, waandishi kadhaa waliokuwepo wakawahi kumshika nami akanishika kaka anaitwa JACKSON kutoka NCARD kitengo cha mauzo aliyekuwa sehemu ya mkutano ule pamoja na MUSSA MWKISU na wengine waliokuwepo"

"Hii sio mara ya kwanza Haji kutumia jukwaa la watu KUNIDHALILISHA, ameshafanya hivyo kwenye group moja la WHATSAPP la Taifa stars kwa kuniita majina yasiyofaa"

"Nitafikisha ombi hili kwenye ofisi ya muajiri wangu kuandika barua kwenda uongozi wa SIMBA SC. Haji amenitishia mara kadhaa nikiwa kwenye majukumu yangu, ametishia KUNIDHALILISHA hata kupitia mitandao ya kijamii"

"Manara asitumie umaarufu wake, asitumie kivuli cha klabu yake ya Simba kutaka kuwadhalilisha watoto wa kike"

🔍 Prisca Kishamba
View attachment 1836334
Lisemaji leye UWELEDI.
 
Ukiona kiongozi (public figure) anatumia lugha mbaya kwenye press conference huyo hafai, anaweza kuwa ana over-confidence", kitu ambacho ni hatari!

Kuna siku nilipata concept kutoka kwa mwandishi wa habari miaka hiyo, ambapo vyombo vya habari vilikuwa hot.

Alisema hivi "Unakuta unampigia mtu fulani kumuuliza tuhuma fulani ili akupe habari lakini hapokei simu au anatukana"

Kitendo cha kutopokea simu au kutukana hizo ni habari pia. Zitaandikwa hivo hivo, kwamba, "alipopigiwa simu, simu yake iliita bila kupokelewa" au "Alipigiwa simu, lakini hakutoa ushirikiano kwa mwandishi".

Maana yangu ni kwamba, unapokuwa msemaji wa timu, kazima utaulizwa maswali ya kuudhi, hivyo ni lazima uwe mpole na ku-relax. Hakuna haja ya kukimbia maswali wala kupanic.
indeed.
 
Prisca Kishamba ni mpuuzi sana huyu dada hasa linapokuja suala la Simba.

Ni moja ya wachambuzi wanaokuza ujinga ujinga na ili kuua brand ya Simba.
Ana ushabiki wa kiutopolo sana.
 
Back
Top Bottom