TANZIA Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde afariki dunia. Azikwa makaburi ya Kinondoni,Dar es Salaam

Ngumu kupoa slim..yan naumwa hapa ila nahis nimezidi kuumwa

QUOTE="Slim5, post: 30655174, member: 196493"]Pole sana..... Kazi ya Mungu..... [/QUOTE]
 
Dstv wataubeba huu msiba ..dah ..Magu yuko wapi atangaze..maana huyu alikua shabiki kindaki ndaki wa ccm
 
Ephraim Kibonde amefariki usiku wa kuamkia Leo tarehe 7 machi 2019

Hatujapoa bado na msiba wa Ruge Leo Kibonde hatunae

Huzuni sana Mungu awape faraja watoto wake

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli duniani tunapita....ninakumbuka mwaka 2015 tulikutana Golden Tulip kwenye get together party ya Heineken...nikakukumbusha miaka ya 1981/2 Tambaza Secondary enzi za Mzee Kalumuna...nikakutajia majina ya mamates kama William Chiume,Jonathan Haule,John Peter,Godius Kahyarara wengine wakubwa kama Yahya Tuli...nikakuuliza ulikua darasa lipi...mm nilikua U...ukanijibu hapana sikusoma Tambaza ila Azania...japo story nyingi redioni zilikua za Tambaza miaka hiyo na ulizipata kutoka kwa marafiki...hasa za kupigana na maaskari polisi watunza foleni na mainspector wa UDA pamoja na migambo wao...pia ugomvi wa Kinondoni Muslim na Tambaza uliotokea Muhimbili Pri school...nitakukumbuka sana ulikuwa unanikumbusha mbaali sana na nikawa mpezi sana wa kipindi chako cha Jahazi....tangulia mate..ni njia yetu wote...mbele yako...nyuma yetu....Mungu aiweke roho yako mahali pema peponi Ephraim....so sad....
 
Kuna watu wanajiona hapa duniani wao ndio wao.....tukumbushane jamani, tutende mema, tuwandee mema wenzetu, tuondoe vinyongo kwa wenzetu, tunayoyafanya na kujivunia ni upepo tu! Mungu akisema rudi huna cha kujitetea
 
Pumzika Kibonde, poleni familia poleni clouds.
 
Mkuu haipendezi kupotosha, pia ulipaswa kuanzisha mada ya malalamiko inayojitegemea kwenye jukwaa husika na sio kwenye bandiko la taazia.

Mada yako umeanzisha dakika tatu baada ya mada hii kuanzishwa.

JF inatenda haki kwa wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eee Mungu wangu bora hata Ruge aliumwa muda mrefu jamani. Duu nilikuwa nasikiliza jahazi kwasababu yake. Nimesikitika sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…