Poleni sana CMG kwa misiba miwili mikubwa....
JF naona siku hizi mnachagua nani anafaa kuweka uzi na nani hafai kuweka uzi...
Nikiwa mwanza kikazi,leo asubuhi napata habari za kifo cha Kibonde toka kwa Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa Mwanza...
Naingia kwenye page ya clouds ya IG wameshatoa taarifa za kifo cha staff wao...
Nami naandika thread hapa juu ya kifo cha Kibonde,naweka na supporting document toka page ya Clouds ya IG...
Nashangaa uzi wangu unafutwa... nakutupwa kwenye dustbin,ila aliyekuja nyuma yangu anaachwa na uzi wake...
Maswali yangu kwenu JF...
a) Hivi naweza toa taarifa za uongo kuhusu kifo cha mtu?? Kwa manufaa ya nani hasa. Hivi mlitaka muamini nini hasa kama nilichofanya mimi,ndicho alichofanya mleta mada nyuma yangu??
b) Je mnapenda watu.wapi wa namna gani watoe thread/uzi ndiyo uamini??
c) Nimepata taarifa toka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mwanza,pia Clouds wenyewe wakawa washatoa kabisa taarifa zao kwenye IG page yao... Ila mkaona hapana mkatoa uzi wangu.
Mnakera sana tena sana....Msipende kubagua nani anafaa na nani hafai kuweka uzi
Sent using
Jamii Forums mobile app