TANZIA Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde afariki dunia. Azikwa makaburi ya Kinondoni,Dar es Salaam

TANZIA Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde afariki dunia. Azikwa makaburi ya Kinondoni,Dar es Salaam

Aisee. Kwenye msiba wa Ruge nilimuona akiwa na afya njema kabisa.

Hakika hakuna ajuaye siku ya Kufa.

Apumzike kwa amani.
 
R.I.P kibonde, nakumbuka kukuona ukiwa MC wakati mwili wa boss Ruge unateremshwa kaburini, tena ulikuwa unatembea na kuchungulia ndani mwa kaburi wakati mtumishi wa Bwana anamwagia maji ya baraka na kuombea shughuli hiyo. kumbe ulichokuwa hukifahamu ni kwammba nawe ulikuwa njiani... Aisee kifo ni fumbo kubwa sana katika maisha ya binadamu.
 
Ni msiba mzito kwa Clouds hasa hasa familia na wapendwa wake wote. Pole yao alazwe anapostahili. Yaani clouds mwaka 2019 hawatausahau na ndo kwanza march .

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
View attachment 1039947

Habari za hivi punde ni kuwa mtangazaji maarufu wa Clouds FM, Ndugu Ephraim Kibonde amefariki dunia alfajiri ya leo tarehe 7 Machi 2019.

Kibonde alianza kusumbuliwa na presha akiwa katika msiba wa marehebu Ruge Mutahaba huko Bukoba mkoani Kagera na kuhamishiwa hospitali ya Bugando jijini Mwanza ambapo mauti yamemkuta.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM, Sebastian Maganga wamethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa
Dah! Kibonde...R.I.P Mzee wa Jahazi
 
poleni sana familia ya marehemu, clouds fm na tanzinia yote ya habari
 
Back
Top Bottom