TANZIA Mtangazaji wa Clouds, Master Tindwa aliyepigwa risasi azikwa leo (Novemba 3, 2025)

TANZIA Mtangazaji wa Clouds, Master Tindwa aliyepigwa risasi azikwa leo (Novemba 3, 2025)

Makumbele

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2009
Posts
312
Reaction score
1,433
8660ecce-7be8-4a4f-aba3-3a27d0c7768a.jpeg


Mtangazaji huyo wa Michezo alikuwa kibarazani kwake alipokumbwa na shambulizi hili.

Marehemu hakuwa akiandamana lakini kama ilivyoripotiwa awali, alipigwa risasi.

Leo mwili wake umepumzishwa katika “nyumba yake ya milele”.

Aliwahi kufanya kazi Radio One na ITV

Pumzika salama ndugu yetu
============
CLOUDS MEDIA GROUP inasikitika kutangaza kifo cha aliyekua mfanyakazi wake Master Tindwa Mtopa, kilichotokea Oktoba 30, 2025 na kuzikwa Novemba 3, 2025 kwenye Makaburi ya Mama Kibonge yaliyopo Buza Jijini Dar es salaam.

Clouds Media Group inatoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote walioguswa na msiba huu na tunamuomba mwenyenzi Mungu ailaze roho ya Master Tindwa mahali pema peponi 🙏.

Screenshot 2025-11-03 195137.png
 
View attachment 3496747

Mtangazaji huyo wa Michezo alikuwa kibarazani kwake alipokumbwa na shambulizi hili.

Marehemu hakuwa akiandamana lakini kama ilivyoripotiwa awali, alipigwa risasi.

Leo mwili wake umepumzishwa katika “nyumba yake ya milele”.

Pumzika salama ndugu yetu
Madhara ya uminywaji wa haki,yanaweza kumuathiri Kila mmoja wetu.
Watu wema wanaweza kuuwawa kwa kisingizio cha kutafuta amani
 
Mtoto wake akija kuwa "Hamza wa baadae" watu wanaanza kumlaumu.
Please watoto wake watoe kwenye hili, Please. Usiwatakie mabaya. Tutatue changamoto yoyote ya Sasa tulimalize tusirithishe kwa vizazi vijavyo.
 
Aloo jamani Kuna watu walikuwa wanapiga risasi kila mtu mtaan

Wengi sana wamepoteza maisha siku ya tarehe 30
Mtaani kwetu kijana alienda kununua mboga akiambatana na mdogo wake asubuhi ya tarehe 30 Oct 2025 .
Ghafla akapigwa risasi ya kichwani ubongo ukamwagika.
Mdogo wake akakimbia akafika salama nyumbani na kutoa taarifa.
Huyu dogo maisha yake yote picha ya namna alivyouwawa Kaka yake itabaki kichwani. Atakuwa na hasira na kuwaza kiasasi maisha yake yote.
Upo mwaka tutashuhudia vurugu kubwa kuliko za sasa zitakuwa za kulipa kisasi.
 
Back
Top Bottom