Njaa Mbaya
JF-Expert Member
- Jul 4, 2012
- 666
- 175
Nimemsikiliza asubuhi hii mtangazaji wa kipindi cha power breakfast Gerald Hando kwenye jicho la ng'ombe anataka katibu mkuu wa baraza la mitihani aueleze umma wa watanzania kwa nini wanafunzi wamefeli. Nikajiuliza hivi anajua kazi ya hili baraza si kuwaandaa wanafunzi kwa mujibu wa mitahala hili wafanye mitihani yao na kufaulu bali ni kutunga mitihani, kusahihisha, kutoa majibu na kutoa vyeti.
Sasa katibu mkuu atajuaje kama wanafunzi wameandaliwa vizuri kwa kuwa hii ni kazi ya taasisi nyingine yaani shule ndizo zenye wajibu wa kazi ya kuwandaa wanafunzi. Shule nazo zina mambo mengi walimu vifaa, miundombinu maslahi ya walimu, maabara nk. Sasa mwenye jukumu la kuhakikisha haya yote yanapatikana ni serikali ili mwanafunzi pate maandalizi mazuri afaulu mtihani uliondaliwa na NECTA.
Unakaa kwenye redio untaka mwenye jukumu la kutunga aeleze matatizo ya maandalizi ya wanafunzi kufanya mitihani. Nina wasiwasi na uwezo na uelewa na pia elimu ya huyu jamaa anaropoka bila kufikiri