Chini ya uzi huu, JF imeniletea uzi mwingine.
Mtu kaandika kichwa cha uzi "Teknolojia hatari inayoogopwa na waharifu huko China".
Huyu ni mtu asiyejua tofauti ya "wahalifu" na "waharifu".
Zamani tulichekana kwa kutojua Kiingereza.
Tukaja kugundua ni vibaya kuchekana hivyo, kwa sababu Kiingereza si lugha yetu. Wote bado tunajifunza tu. Wengine kwa bado kwa sana, wengine tunajifunza bado hata kama tunakijua kuliko Waingereza wengi.
Rais Mwinyi alisema Kiingereza ni Kiswahili cha dunia.
Akimaanisha kwamba, kama Kiswahili kilivyo "lingua franca", lugha ya biashara, ya Tanzania na Afrika ya Mashariki, Kiingereza ni kugha ya biashara ya dunia.
Nchi yetu inaongeza watu kwa kasi kubwa kuliko inavyoongeza usomi.
Hivyo ni wazi kunaongezeka watu wengi sana wasiojua mambo ya msingi kabisa, hata matamshi, sarufi, herufi, nomino, nyambulisho, fasihi, hata kusima tu kwa ufasaha.
Hata hapa JF tu, napata tabu karibu kila siku, kwa sababu nakutana na watu wengi ambao inaonekana wazi kwamba hawajui kusoma kwa ufasaha na kufuatilia matiki ya lugha.
Hawajui. Ama hawafundishwi au hawafuatilii wao ni suala tofauti, lakini, inainekana tunazidisha idadi ya wajunga nchini. Sikusudii kuwatusi, lakini nakusudia kueleza ujunga kama ukisefu wa ujuzi wa jambo.
Hao waajiri oengine wanaoenda hao wasiojua mambo sana, kwa sababu hao ndio wasiojua kudai haki na mishahara, wanaojua mengi wanadai mengi.
Kwa hivyo, licha ya kwamba kuna wengi wenye kujua mengi, inawezekana wasiojua mengi wakachagukiwa jwa sababu ndio wanaokwenda na bajeti ya kubana matumizi.
Tunapenda zaidi kubana matumizi kuliko kufanya kitu vizuri hqlafu kikaleta ufanisi zaidi na kujenga biashara zaidi.
Mwishowe tunabana matumizi kijinga.
Unaajiri mtu asiyejua lugha, makampuni ya kutangaza biashara yanaona hufai kuoata matangazo. Unakosa biashara kwa kuonekana unabangaiza.
Wakati tofauti ya hela kidogo tu ya kumuajiri mtu anayejua kazi, ingekupeleka ufanye biashara za matangazo mpaka ya kimataifa.
Tunajifunga wenyewe kwa kukisa vision.
Halafu tunatafuta mchawi aliyeturoga na kutuweka kwenye umasikini.