Mtangazaji wa TBC 1 anasema meli ya MV Mwanza itapiga route ikiwa ziwa Victoria kwenda Sudani Kusini, Burundi, Zambia Congo na Malawi

Mtangazaji wa TBC 1 anasema meli ya MV Mwanza itapiga route ikiwa ziwa Victoria kwenda Sudani Kusini, Burundi, Zambia Congo na Malawi

Status
Not open for further replies.
Hakuna tasnia iliyojaa wajinga kama Uandishi wa habari fikiria media house zimejaza wajinga ambao hawajasomea kabisa mambo ya habari kuna akina Swebe, Zomboko, Mbwiga wa Mbwiguke akina Eddo Kumwembe hawa wanapewa vipaza sauti bula kujua maana ya umuhimu wa mambo ya habari akina Kitenge wote hao.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
TBC hivi sasa ina vilaza kupita maelezo! Kiswahili fasaha shida Jiografia ya nchi hii hawaijui, majina ya miji na mikoa wanachangaya mfano wanaita mkoa wa Songea badala ya Ruvuma nk!

Bila shaka ajira zao ni za kujuana!
 
Mleta uzi ni muongo hii ilitokea 2017 na barua ya kusimamishwa kazi ipo ilisainiwa 2017
 
View attachment 2948865

Sitaki niongee mengi nishasema watanzania wengi hasa kwenye kada ya uandishi wa habari miaka ya 2000+ ni hopeless na vilaza wa kutupwa sijui journalism gani hawajui hata Geography ya Primary na O level.

Kama mnauzinduzi wa MV Mwanza basi vilaza wenu washaropokwa huko.

Endeleeni na vilaza kwenye vyombo vya umma.

Ni hayo tu.

Wadiz.
Hiyo meli itakuwa na matairi usihofu.
 
Tanzania eeeehh!... Nchi yangu oooh!
Huyo ni mtangazaji wa Television ya Taifa! Ukweli na uwazi!

Taaluma ya habari imeingiliwa!
 
Hana hatia, yeye alimnukuu kiongozi mmoja kilaza mpenda sifa. Sasa wewe wasilisha taarifa uondoe midosho ya boss useme umehariri ufukuzwe kazi😅
 
TBC waliweza kutumia Bendera ya taifa kuziba mabonde yaliotwama maji barabarani katika msafara wa msiba wa Magufuli, hawashindwi jambo wanaweza ikokota meli na SGR mpaka Kote walikokusema wakubwa.
 
Kama tunadanganywa kwenye mamboo ya wazi namna hii vipi huko kwenye mafail maofisini
Hatari kaka. Jitu kama hili likiambiwa litangaze kuwa mikutano ya vyama vya siasa italeta vita linatangaza TU bila kuwaza mara mbili.
 
Sudani Kusin > Burundi > Zambia > Congo na Malawi, 🤒🤒🤒.

Huwezi jua labda Ramani imebadilika 😁😁.
Hahahaaa. Mkuu; au Ikifika mahali inatumia magurudumu au inaota mbawa na kuruka angani. Kazi tunayo aisee. Labda alitaka kusema kutakuwepo na bandari ya nchi kavu na abiria na mizigo yao watafikia/watashukia hapo kwa kupelekwa kwa magari?
 
😀😀😀, kama waandishi wenyewe ndo Hawa, Sishangai sana siku ile saa100 akiwa live kutangaza kifo cha mzee mwinyi.
 
Mleta uzi ni muongo hii ilitokea 2017 na barua ya kusimamishwa kazi ipo ilisainiwa 2017
Ile ya 2017 ilikuwa inahusu "Trump kumpongeza Magufuli" mkuu. Wewe ndiye muongo.
 
Kama tunadanganywa kwenye mamboo ya wazi namna hii vipi huko kwenye mafail maofisini
Huyo mtangazaji hajadanganya hata kidogo, ameonyesha tu uwezo wake duni kulingana na kazi aliyopewa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom