Uchaguzi 2020 Mtani wangu Tundu Lissu pokea huu 'Ukweli' wangu japo najua hujaambiwa na unaweza ukawauma Wakupendao

Uchaguzi 2020 Mtani wangu Tundu Lissu pokea huu 'Ukweli' wangu japo najua hujaambiwa na unaweza ukawauma Wakupendao

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
UTANGULIZI
Sijawahi hata Siku moja kuficha Hisia zangu za 'Kukukubali' sana hasa kwa aina ya 'Misimamo' yako thabiti, uwezo wa Kufikiri ( Akili ) na pia Kuchambua mambo 'Kiumakini' kabisa. Na hapa nisikufiche si Mimi tu ambaye ni mwana CCM nakiri na kulisema hili ila nina uhakika hata wana CCM wengi tu nao wapo kama Mimi juu yako sema tu hawakuonyeshi Kiuwazi japo Mioyoni mwao upo sana tu.

MTAZAMO
Sina shaka kabisa na Wewe Kutia Nia na hatimaye Chama chako cha CHADEMA Kukuamini na Kukuteua kuwa Mgombea wao kwani Kisheria na Kikatiba hii ni Haki ya Kila Mtanzania mwenye Sifa Kamili kufanya hivyo. Wasiwasi wangu Kwako upo sehemu ndogo tu kwamba umewahi kufanya 'Timing' Kipindi hiki kibaya Kwako Kisiasa na badala yake kwa mwaka 2025 ndiyo ulikuwa muda Muafaka.

USICHOKIJUA
Mtani wangu kutoka Singida Tundu Lissu najua unaweza 'usiamini' ila kwakuwa GENTAMYCINE 'nakupenda' ngoja nikuambie tu ukweli kuwa pamoja na kwamba unaona una Watu (Wafuasi) wengi wakiwa nawe kila uendako ila ukweli ni kwamba 'Kitakwimu' ni 25% tu hao unaowaona ndiyo 'Wamejiandikisha' Kupiga 'Kura' mwaka huu na 'Wamehakiki' vyema kabisa Majina yao Vituoni.

ULILOLISAHAU WEWE NA CHADEMA YAKO
Hapa sitokulaumu Wewe sana Mtani wangu Tundu Lissu kwakuwa muda mwingi ulikuwa katika 'Matibabu' yako huko 'Ughaibuni' ila lawama zangu nyingi nazipeleka kwa CHADEMA kwa 'Kujisahau' Kwao muda mwingi 'Kuwahimiza' Wanachama wao waende 'Kujiandikisha' Vituoni na badala yake wao muda Wao mwingi walitumia 'Kuwekeza' katika 'Kupambana' tu na Serikali ( Dola )

UMAKINI WA CCM UPO HAPA
Tayari CCM walishafanya 'Utafiti' wao wa ndani tena 'Kiumakini' kabisa na 'Kujiridhisha' kuwa wana uhakika wa Kura 8,000,000 ( Milioni Nane ) kutokana na 'Wanachama' wao nchi nzima hivyo wakaendelea katika Kuwatafuta wengine ili kuongeza hiyo idadi huku 'wakiwahimiza' sana Wanachama wao hao 'Kujiandikisha' na hata 'Kuhakiki' Majina yao Jambo ambalo wamefanikiwa 100%.

MKAKATI WA KISIASA ULIOIMALIZA KABISA CHADEMA
Wakati CHADEMA yako muda mwingi 'ikiwekeza' katika 'Kulaumu' na 'Kupambana' na Mamlaka ( Dola ) hasimu walisahau kuwa Siasa zote duniani pia huwa zina 'Umafia' ndani yake na mliosoma 'Political Science' mtanielewa hivyo baada ya 'Kuhisiwa' kuwa mtaendelea kuwa 'Tishio' mkatafutiwa 'Adui Rafiki' wa huko huko 'Upinzani' asaidiwe na wa Kwao ili 'Kuzigawa' Kura zenu nyingi.

FAIDA PEKEE AMBAYO TUTAIPATA KUTOKA KWAKO
Mtani wangu Tundu Lissu wala 'usidanganyike' na 'wasikudanganye' uwezo wa Wewe Kushinda na kuwa Rais wetu haupo na huna hasa kutokana na 'Mikakati' iliyoko na pia kwa 'Mpinzani' wako kufukia karibia 90% ya yale 'Mashimo' yote ya 'Kimapungufu' katika 'Utawala' wake. Kitu pekee utakachofanikiwa nacho ni 'Kuwajaza' tu Watanzania wachache Imani za Chuki na Majungu pia.

USHAURI WANGU KWAKO
Kwakuwa nina uhakika kuwa hutoweza 'Kutoboa' hata iweje ( japo utajitutumua ) ningependa tumia sasa uwezo wako huu mkubwa wa 'Ushawishi' ulionao katika 'Kuwahimiza' Watanzania wanaokuamini na Wafuasi wako 'Wawachague' Wabunge wengi wa CHADEMA ili angalau wakiwa wengi basi muweze kuwa na 'Nguvu' Bungeni ambayo inaweza 'Kukujenga' kwa 2025 Ukigombea.

UWEPO WAKO NI TIJA KUBWA KWA CCM KUENDELEA KUJIJENGA ZAIDI
Nakujua na ni matuamini yangu makubwa kuwa hata katika Mikutano yako ya Kampeni zilizoanza utakuwa unatumia muda mwing sana 'Kuinanga' ile mbaya CCM na Mwenyekiti wake ila usisahau tu kuwa kwa kadri utakavyokuwa 'unawasema' CCM na Rais wao ndiyo utakuwa 'unawafunua' na 'kuwajenga' zaidi ili wazidi 'Kujikita' na 'Kujidhatiti' kabisa Madarakani na Kiutawala.

HITIMISHO
Nakutakia tu Kampeni njema Mtani wangu Tundu Lissu Wewe pamoja na Vyama vingine vyote vya Upinzani nchini Tanzania ila niwaombeni tu tumieni 'Muhula' huu wa mwisho wa Rais Dkt. Magufuli kuwepo 'Madarakani' kwa nyie 'Wapinzani' Kwanza Kujitathmini na Kujijenga zaidi huku mkiwa 'Wamoja' na muache 'Unafiki' ili basi Chaguzi zijazo muingie mkiwa ni Wamoja kabisa.

Wako Mtani wako

GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE ( Majina yangu Kamili ni Kalemera Rwigyema Mazimpaka Kadogoo )
 
Nchi hii bana kwa kweli Ina Mambo mengi sana na watu wa aina yake. NEC wanatuambia Kuna wapiga kura 29 milioni waliojiandikisha kupiga kura mwaka huu. CCM kwa mujibu wa pole pole inawanachama Kama 14 milioni, Je, hao 15 milioni ni akina nani?
 
Nchi hii bana kwa kweli Ina Mambo mengi sana na watu wa aina yake.NEC wanatuambia Kuna wapiga kura 29milioni waliojiandikisha kupiga kura mwaka huu.Ccm kwa mujibu wa pole pole inawanachama Kama 14 milioni,Je hao 15 milioni ni akina nani?

Bora umemwambia, maana 29m+ ni nusu ya watanzania wote, kwa maneno marahisi ni watu wazima wote wenye miaka 18 na kuendelea.
 
Nchi hii bana kwa kweli Ina Mambo mengi sana na watu wa aina yake. NEC wanatuambia Kuna wapiga kura 29milioni waliojiandikisha kupiga kura mwaka huu.Ccm kwa mujibu wa pole pole inawanachama Kama 14 milioni,Je hao 15 milioni ni akina nani?

Hivi niliposema kuwa CCM tayari walikuwa na Wanachama wao 8,000,000 (Milioni Nane) 'Kibindoni' na kwamba waliendelea tena 'Kuwatafuta' wengine hivyo ni 'obvious' kuwa kwa 'Mikakati' yao watakuwa 'wameongezeka' ulinielewa?

Kuna Watu hapa kutokana na 'Upumbavu' wenu na Kupenda 'Kukurupuka' katika Kusoma 'Threads' zangu huwa mnanilazimisha niwe nawajibuni 'hovyo' tu. Kama huna 'Akili' usifungue 'Uzi' wangu.
 
You, hypocrite shut up your mouth.

Leo hii GENTAMYCINE kwakuwa nimesema 'Ukweli' ambao unawauma CHADEMA naitwa 'Mnafiki' ila nikiwa nakisema Chama changu 'pendwa' cha CCM na hadi Mwenyekiti wangu Taifa Rais Dkt. Magufuli huwa mnaniona Mtu sahihi Kwenu.

Sasa hapa kati yangu Mimi Mkweli na Wewe usiyependa Kuambiwa Uwazi kama huu niliouweka hapa ni nani 'Mnafiki' zaidi? Najua huu ni 'Ukweli Mchungu' Kwenu ila 'muupokee' tu sawa?
 
Bora umemwambia, maana 29m+ ni nusu ya watanzania wote, kwa maneno marahisi ni watu wazima wote wenye miaka 18 na kuendelea.

Na Wewe kumbe umeshindwa 'Kunielewa' kama huyo 'Mpumbavu' Mkuu?
 
Umenikumbusha jambo zuri,wakati wa kujiandikisha,kuna watu walihamasisha watu wasijiandikishe kuikomoa Gavamenti,na saizi kampeni zimeanza watu wengine hawakujiandikisha.....itaishia kuwa kelele tu ila vitendo zero......kuna siredi humu nyingi tu......sasa nani atapiga kura?

Anyway,ngoja sisi wapenzi watazamaji tuendelee kula mchuzi....nyama tutazikuta chini
 
Nchi hii bana kwa kweli Ina Mambo mengi sana na watu wa aina yake.NEC wanatuambia Kuna wapiga kura 29milioni waliojiandikisha kupiga kura mwaka huu.Ccm kwa mujibu wa pole pole inawanachama Kama 14 milioni,Je hao 15 milioni ni akina nani?
Milioni 8 ni costant! Piga ua hiyo ipo ya wanachama kindakindaki,sasa chadema hawawezi kuipita hiyo hata wafanyaje.watabaki wanachama mil 6 kati ya 14,hao tutapata nusu,nusu watakuwa na vinyongo vya kuenguliwa.jumla mil 11.zitabaki kura 18 za wananchi kati ya milioni 29 za wapiga kura wote.hapo sasa ccm watavuna 90% ya wapiga kura mil18 ambayo ni kama mil16 na laki 2, ukijumlisha ccm watapata kura milion 27 .2.[emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji112][emoji112][emoji112]
 
Leo wanafungua kampeni zao lakini wameshindwa kabisa kusema watafanya nini wakichaguliwa. Muda wote wanalaumu tu
Hili la msingi sana. Kulaumu tuuu na kulialia kwamba alipigwa risasi 85% ya speech ni wastage ya time.

Watu wana kiu kubwa kusikia kitu tofauti CHADEMA itafanya tofauti na CCM ya JPM. Muda wa kurekebisha bado upo though
 
Watakaompigia kura Lisu ni wafuatao-
1.Wafanyakazi waliokosa nyongeza ya mishahara kwa miaka 5 ilihali gharama za maisha zineongezeka maradufu.

2.Wafanyakazi waliotumbuliwa kwa uhakiki wa vyeti na kunyinwa haki zao za msingi.

3.Vijana waliorundikana mitaani wasijue nini cha kufanya kwa ukosefu wa ajira kwa miaka mingi.

3.wafanyabiashara waliofilisiwa biashara zao,waliobambikiziwa kodi zisizo na mfano.

4.Wafanyakazi walioongezewa makato ya HESLB bila kuongeza mishahara.

5.Watu waliokerwa na kukosa furaha ndani ya nchi yao kwa kukosa uhuru wa kujieleza,uminywaji wa demokrasia na ukandamizaji wa haki za kiraia na kibinadamu.

kwa ufupi,watu niliowataja hapo juu ni wanachama wa CCM,CHADEMA,ACT, na wengine hawana vyama kama mimi.

Msingi wa kukubalika ni HAKI,Haki huinua taifa.
 
GENTAMYCINE wengi naona mnamuattack kwa huu Uzi wake,ila tusipende kusikia mazuri tu,hata kukosolewa ni njia mojawapo ya kujenga.....WaTz huwa hatupendi kuambiwa ukweli......iwe chama tawala au opozisheni.......yaani kila mtu akiweka siredi inayokosoa upande fulani anaonekana wa upande fulani,sikweli.....tumpimge kwa hoja na fakti
 
Back
Top Bottom