Mtanzania adai kugundua dawa ya corona, ataka kuonana na Waziri wa Afya

Mtanzania adai kugundua dawa ya corona, ataka kuonana na Waziri wa Afya

Swali ni je, anajuaje kuwa dawa yake inatibu corona?Kama anayo maelezo ya kutosheleza kuthibitisha kujua kwake huko, apewe ushirikiano..Lakini kama anaamini tu kuwa inatibu apuuzwe.Mambo ya kujua kwa sababu ya kuamini ni mambo yasiyoweza kutuondosha kwenye janga LA corona...Hawezi tu kutwambia anajua kwa asilimia mia dawa yake inatibu kwakuwa tu yeye anaamini hivyo!!

Tukifanya jambo ambalo kila mtu anaamini tutakuwa ni taifa LA machizi.Mimi nikisema ninaamini kisamvu kinatibu corona kwa asilimia mia pia nitataka nikutane na Ummy?Pengine nimependa shingo yake tu nataka niione mubashara halafu ninazuga nina dawa ya corona..Na hapo ndipo wazungu wanapotuacha kwenye haya mambo ya gunduzi muhimu..Sisi tunatoa maelezo ya kuamini,wao wanatoa maelezo ya kisayansi kutushawishi kwa nini wanajua.Wanafanya mpaka majaribio kuonesha wanachotueleza..Sisi tunataka tuaminiwe tu basi..
 
Mwamsumbwe!!!!!

Bila Shaka atakuwa ni mtu wa mbeya huyo,Babu wa loliondo mpya
 
Laki
Angeeleza hiyo research kafanya vipi, test kafanya vipi, na mafanikio ni asilimia ngapi, sio kuja na maneno ya juu juu tu. Huyu mtu ni stupid akifikiri maisha ni mepesi mepesi hivyo.
Lakini hana haja ya kueleza details zake zote hapa Jf, hii ndio siri ya uvumbuzi.
Atakapofika kwa waziri na kuunganishwa na wahusika ,huko atajieleza kwa kina.
We vipi yakhe?
 
Kila mtu anayedai kuvumbua dawa akitaka kuonana na waziri si itakuwa tabu. Cha msingi kama hoja zake ni timamu aende kitengo cha tiba asili pale Muhimbili aonane na watafiti wa hizo mambo. Hivi hata yule wa kujiita Mashimo si naye alidai ana dawa? Aliishia wapi?
Mtu akihitaji kuonana na waziri ,anakusudia Mamlaka ya nchi,watu wengine huwa hawajuwigi wapi waanzie mambo yao ndo maana yeye kamtaja waziri,hayo mengine yatajiseti huko huko baada ya kufika wizarani.

Pengine akienda mwenyewe tuu pale kwenye kitengo ,wanaweza wakampuuza,si unajuwa Watu wetu nchi hii?
Lakini akienda kwa kibali cha waziri anaweza pewa uzito fulani na kulisaidia Taifa.
 
Laki

Lakini hana haja ya kueleza details zake zote hapa Jf, hii ndio siri ya uvumbuzi.
Atakapofika kwa waziri na kuunganishwa na wahusika ,huko atajieleza kwa kina.
We vipi yakhe?

Akifika kwa waziri nitashangaa waziri gani kilaza anapokea watu ovyo. Ninafahamu vizuri scientific procedure za mambo kama haya, kusema ametest vipi kuprove kua inatibu korona haiwezi kua siri wala haiwezi kuelezea alivyotengeneza.

Mfano anaweza sema amechukua damu au kohozi la mtu mwenye korona akaweka kwenye microscope akachukua dawa yake akaweka akaona kua dawa yake inaneutralize kirusi cha korona. Kuelezea kitu kama hicho kinatoa vipi siri ya dawa yake?

Hajatest vyovyote vile, sio kwa mtu wala mnyama, amekaa tu anasema ana dawa, hivi utasemaje una dawa huku hujijaribu?, hahaha akaongee na wajinga hakuna chochote akae ndani tu ajilinde na korona sio kutupotezea muda. Ningekua waziri huyu asingenikaribia hata kidogo. Waste of time
 
Kila mtu anayedai kuvumbua dawa akitaka kuonana na waziri si itakuwa tabu. Cha msingi kama hoja zake ni timamu aende kitengo cha tiba asili pale Muhimbili aonane na watafiti wa hizo mambo. Hivi hata yule wa kujiita Mashimo si naye alidai ana dawa? Aliishia wapi?
Sio lazima kwa waziri.. serikali iwaelekeze sehemu au kitengo husika wapeleke huko. Na itangazwe baada ya kuthibitishwa inafaa! Yoyote atakaetangaza bila kupitia kwenye kitengo husika achukuliwe hatua kali za kisheria!
 
View attachment 1437262

MKAZI wa Chanika jijini Dar es Salaam Seleman Mwamsumbwe (pichani kushoto) akiwa na dada yake(kulia) ameomba kukutana na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwa lengo la kumueleza habari njema ya kwamba amegundua dawa inayoweza kutibu ugonjwa wa COVID-19 unaotokana na virusi vya corona.

Akizungumza na waandishi wa habari leo nyumbani Chanika huku akiwa na furaha na tabasabu tele Mwamsumbwe amesema kuwa dawa hiyo ambayo ameigundua hawezi kuitaja hadharani kwa sasa hadi pale atakapoona na Waziri Ummy Mwalimu.
"Natambua changamoto kubwa Dunia inapitia kwa sasa na kusababisha mataifa mbalimbali kuhaha kutafuta tiba ya corona Dawa yangu ambayo tayari nimeifanyia utafiti wa kutosha nimjeridhisha ina uwezo wa kutibu ugonjwa huo bila tatizo lolote, naomba kukutana na Waziri wa Afya nizungumze naye na kisha nipate baraka ili kuokoa maisha ya watu ambayo yanaangamia kwa Corona,"amesema.

Akifafanua zaidi kuhusu dawa hiyo Mwamsumbwe amesema kwamba dawa hiyo inauwezo wa kutibu mfumo mzima wa mapafu, kuondoka mafua makali pamoja kikohozi.
."Namuomba Waziri wa aje tuonane ninahakika dawa hii itasaidia kuponya ugonjwa huu wa Corona au kupunguza makali ya gonjwa."amesisitiza na kuongeza anao uhakika wa asilimia 100 wa dawa hiyo kutibu Corona.

Mkazi wa Chanika Dar, Seleman Mwamsumbwe ambae anadai kugundua dawa ya kutibu Corona akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake kuhusu dawa hiyo ambapo ameomba kukutana na Waziri wa Afya ili kuzungumza nae kwa kina.

Swali kama ana dawa kwanini kavaa maski kubwa hivyo ?
da nmecheka sana kwenye huu.mstari wa mwisho.kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu bila Shaka Ni kigagula fulani anataka ku-take advantage ya Covid-19 kujipatia umaarufu na kipato kwa watakaoingia kwenye 18 zake.
Is like BABU WA LOLIONDO COMEDIAN.,....!!
Watz be careful Vinginevo mtaliwa!!!🤣🤣
 
Kiki za kijinga tu. Kila mtu ana dawa ya Corona tukitaka kuonana na Waziri tutaleta mikusanyiko.

Barakoa yake ni kwaajili ya kuzuia mende wasiingie puani.?
Ahaaaa ahaaaa, eti kama ana dawa kwanini kavaa barakoa kubwa hivyo? Huyu atakuwa ni tapeli la ccm.
mbona hata malimao na tangawizi yanatibu, sasa si kila mtu angeomba kuonana na waziri wa afya?
Nimefurahia swali ulilomtwangwa!
Nadhani tuache tabia ya kukejeli vya kwetu badala yake tuwape sapoti kwa kufanya uchunguzi. Wakati mwingine huwa nashangaa baadhi ya members humu sijui wanatumia akili kweli kufikiri?

Angekuwa mzungu mijinga yote ingeandika kusifia, "hii sasa ndio tiba halisi ya korona!!" Utumwa mbaya sana wakuu, unakabidhi akili yako kwa mtu mwingine afikiri kwa niaba yako. TUBADILIKE.

Mbona yako madawa mengi tu ya tiba mbadala ambayo yana uwezo kutiba magonjwa yaliyowashinda hao wataalamu mnaowategemea? Mdharau cha kwao ni mtumwa, hakuna ujinga unaopita kupinga kitu ambacho wala huna ABC zake. Yaani mtu hata hajaanza kuongea tayari umeshajua mawazo yake na kutoa najibu hapo hapo!! Sio tabia inayopendeza na humu jf inabidi tuanze kukanyana turejeze akili zetu sawa, tusiwe misukule ya mataifa ya magharibi.

ASANTE SANA

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
 
Nimefurahia swali ulilomtwangwa!
Swali la kijinga mno, kugundua dawa hakuondoi taratibu zilizowekwa. Pia amekwambia amegundua TIBA kwa maana kwamba inatibu MGONJWA. Sasa unatoka atoe mask, kwani amesema KAGUNDUA CHANJO????

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
 
Hili ndilo haswa anapaswa kulifanya, kisha hao watakaopona watawajulisha wengine nae atatafutwa kama tabibu wa COVID-19 na mengineyo!!
Nijuavo Mimi Kuna Chama Cha Wagangs wa TIBA ASILI WANAOSHIRIKI na Kitengo Maalumu cha Tiba Asili pale Muhimbili National Hospital. Alipaswa aanzie pale kama kweli ana tiba ya Covid-19.

From there anaweza pewa wajonjwa 5 au 10 confirmed kuwa wana Covid-19 halafu awape dozi yake kwa muda fulani then Tiba yake ioneshe itakavyo respond na Covid-19........wangapi watapona na Wangapi hawatapona!

Nje ya hapo new utapeli na ubabaishaji tu....!!!
Watz lazima wajue kuwa hili ni Janga but at the same time is an opportunity for Conmen to make a flourishing business...!!!
 
Waziri akufuate wewe wapi?
Kuna kitengo cha tiba mbadala pale Muhas nenda kaonane nao...peleka dawa yako ikafanyiwe utafiti wa kina...kama inaweza kutibu basi utapewa hati milki....
 
Back
Top Bottom