Mtanzania adai kugundua dawa ya corona, ataka kuonana na Waziri wa Afya

Kuna sehemu nimesema hakuna umuhimu wa kuvaa barakao?
Sasa kuvaa barakoa na ugunduzi wa dawa vinahusianaje? Mpaka unamshangaa mgunduzi kuvaa mask kujikinga na virus vya Corona akiwa anahojiwa na waandishi wa habari??!! Yeye kasema amegundua dawa ya kutibu siyo kukinga, inakuaje unamshangaa kujikinga?!!!!

Fuatilia hata USA wamedai wameshapata tiba ya CORONA, lakini madaktari wagunduzi hawajaacha kuvaa BARAKOA

Sio eti kwasababu dawa ya vidonda vya tumbo imegunduliwa basi mgunduzi yuko huru kujipa msongo wa mawazo na kufanya mpangilio mbovu wa ulaji, akifanya hivo atapata tena vidonda vya tumbo[emoji15][emoji15]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna sehemu nimeonesha mshangao?
 
Waziri akufuate wewe wapi?
Kuna kitengo cha tiba mbadala pale Muhas nenda kaonane nao...peleka dawa yako ikafanyiwe utafiti wa kina...kama inaweza kutibu basi utapewa hati milki....

Said it well.
Unajua Kuna Wabongo wengi sana hawajui Mambo yanayohusiana na taratibu na sheria za nji.....!!
 
Eti "ameifanyia utafiti na kujiridhisha inaweza kutibu corona"
Huo utafiti amefanyia wagonjwa wangapi wa corona? Au alikuwa anaumwa yeye akatumia akapona?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti "ameifanyia utafiti na kujiridhisha inaweza kutibu corona"
Huo utafiti amefanyia wagonjwa wangapi wa corona? Au alikuwa anaumwa yeye akatumia akapona?

Sent using Jamii Forums mobile app

Watu lazima wajue kuwa Kati ya wanaoungua Covid-19 Kuna wale wanaopona kwa kuwa na (KINGA) IMMUNITY IMARA ya mwili, kuna wanaopona kwa kutumia dawa za kufukiza na kupona lakini pia kwa kutegemea Kinga imara ya mwili...!!!
Hivo kuthibitisha Kama dawa ya huyu jamaa inatakiwa uchunguzi wa kina haswa....!
 
View attachment 1437262

MKAZI wa Chanika jijini Dar es Salaam Seleman Mwamsumbwe (pichani kushoto) akiwa na dada yake(kulia) ameomba kukutana na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwa lengo la kumueleza habari njema ya kwamba amegundua dawa inayoweza kutibu ugonjwa wa COVID-19 unaotokana na virusi vya corona.

Akizungumza na waandishi wa habari leo nyumbani Chanika huku akiwa na furaha na tabasabu tele Mwamsumbwe amesema kuwa dawa hiyo ambayo ameigundua hawezi kuitaja hadharani kwa sasa hadi pale atakapoona na Waziri Ummy Mwalimu.
"Natambua changamoto kubwa Dunia inapitia kwa sasa na kusababisha mataifa mbalimbali kuhaha kutafuta tiba ya corona Dawa yangu ambayo tayari nimeifanyia utafiti wa kutosha nimjeridhisha ina uwezo wa kutibu ugonjwa huo bila tatizo lolote, naomba kukutana na Waziri wa Afya nizungumze naye na kisha nipate baraka ili kuokoa maisha ya watu ambayo yanaangamia kwa Corona,"amesema.

Akifafanua zaidi kuhusu dawa hiyo Mwamsumbwe amesema kwamba dawa hiyo inauwezo wa kutibu mfumo mzima wa mapafu, kuondoka mafua makali pamoja kikohozi.
."Namuomba Waziri wa aje tuonane ninahakika dawa hii itasaidia kuponya ugonjwa huu wa Corona au kupunguza makali ya gonjwa."amesisitiza na kuongeza anao uhakika wa asilimia 100 wa dawa hiyo kutibu Corona.

Mkazi wa Chanika Dar, Seleman Mwamsumbwe ambae anadai kugundua dawa ya kutibu Corona akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake kuhusu dawa hiyo ambapo ameomba kukutana na Waziri wa Afya ili kuzungumza nae kwa kina.

Swali kama ana dawa kwanini kavaa maski kubwa hivyo ?
hawa wakina "mwa" hawa tabu tuu watatutelezesha kama mwampo$@ 🤔😏
 
Mwamsumbwe si ndo wale wale akina Ambilikile Mwasapile ? Wanyakyusa bana!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu lazima wajue kuwa Kati ya wanaoungua Covid-19 Kuna wale wanaopona kwa kuwa na (KINGA) IMMUNITY IMARA ya mwili, kuna wanaopona kwa kutumia dawa za kufukiza na kupona lakini pia kwa kutegemea Kinga imara ya mwili...!!!
Hivo kuthibitisha Kama dawa ya huyu jamaa inatakiwa uchunguzi wa kina haswa....!
Nakubaliana na wewe 100%.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani tuache tabia ya kukejeli vya kwetu badala yake tuwape sapoti kwa kufanya uchunguzi. Wakati mwingine huwa nashangaa baadhi ya members humu sijui wanatumia akili kweli kufikiri?

Angekuwa mzungu mijinga yote ingeandika kusifia, "hii sasa ndio tiba halisi ya korona!!" Utumwa mbaya sana wakuu, unakabidhi akili yako kwa mtu mwingine afikiri kwa niaba yako. TUBADILIKE.

Mbona yako madawa mengi tu ya tiba mbadala ambayo yana uwezo kutiba magonjwa yaliyowashinda hao wataalamu mnaowategemea? Mdharau cha kwao ni mtumwa, hakuna ujinga unaopita kupinga kitu ambacho wala huna ABC zake. Yaani mtu hata hajaanza kuongea tayari umeshajua mawazo yake na kutoa najibu hapo hapo!! Sio tabia inayopendeza na humu jf inabidi tuanze kukanyana turejeze akili zetu sawa, tusiwe misukule ya mataifa ya magharibi.

ASANTE SANA

Sent from my SM-A720F using Tapatalk

Ni hivi, huu utapeli ndio ulichangia watu kwenda kwa babu kunywa maji machafu eti ni tiba! Ww utakuwa ni mshirikina lazima ndio maana unatoa povu.
 
Back
Top Bottom