View attachment 1437262
MKAZI wa Chanika jijini Dar es Salaam Seleman Mwamsumbwe (pichani kushoto) akiwa na dada yake(kulia) ameomba kukutana na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwa lengo la kumueleza habari njema ya kwamba amegundua dawa inayoweza kutibu ugonjwa wa COVID-19 unaotokana na virusi vya corona.
Akizungumza na waandishi wa habari leo nyumbani Chanika huku akiwa na furaha na tabasabu tele Mwamsumbwe amesema kuwa dawa hiyo ambayo ameigundua hawezi kuitaja hadharani kwa sasa hadi pale atakapoona na Waziri Ummy Mwalimu.
"
Natambua changamoto kubwa Dunia inapitia kwa sasa na kusababisha mataifa mbalimbali kuhaha kutafuta tiba ya corona Dawa yangu ambayo tayari nimeifanyia utafiti wa kutosha nimjeridhisha ina uwezo wa kutibu ugonjwa huo bila tatizo lolote, naomba kukutana na Waziri wa Afya nizungumze naye na kisha nipate baraka ili kuokoa maisha ya watu ambayo yanaangamia kwa Corona,"amesema.
Akifafanua zaidi kuhusu dawa hiyo Mwamsumbwe amesema kwamba dawa hiyo inauwezo wa kutibu mfumo mzima wa mapafu, kuondoka mafua makali pamoja kikohozi.
."
Namuomba Waziri wa aje tuonane ninahakika dawa hii itasaidia kuponya ugonjwa huu wa Corona au kupunguza makali ya gonjwa."amesisitiza na kuongeza anao uhakika wa asilimia 100 wa dawa hiyo kutibu Corona.
Mkazi wa Chanika Dar, Seleman Mwamsumbwe ambae anadai kugundua dawa ya kutibu Corona akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake kuhusu dawa hiyo ambapo ameomba kukutana na Waziri wa Afya ili kuzungumza nae kwa kina.
Swali kama ana dawa kwanini kavaa maski kubwa hivyo ?
Mleta mada sijuwi kama ulikutana na huyu muhusika?
Mtu huyu si wa kupuuzwa kamwe,haraka sana mpeni chanel za kukutana na Mh.Waziri ili aeleze alicho nacho.
Huenda Bw. Seleman Mwamsumbwe amesha fanya tafiti chini kwa chini na kutibu wagonjwa wa aina hiyo huko mitaani,sasa anataka kupata kibali cha serikali ili aruhusiwe kuwatibu wagonjwa kule Luganzila ,na pengine anataka akutane na wataalamu wa kitengo cha dawa za kijadi pale muhimbili ili atowe mchango wake.
Mimi nina Kisa kidogo cha Mtu wa famila yangu .
Mama huyu aliugua Mafua yanayo tiririka kama maji bila kuzuia.Kila alipokwenda hospitali hakupata tiba.
Alipelekwa India na kukaa huko wiki tatu hivi kwa matibabu ,na wao hawakufanikiwa,kwa vile alikuwa na uwezo na misaada ya watoto wake walioko nje ,wakampeleka Ujerumani alikaa huko siku 14 nako pia hakufanikiwa Ila wao walipendekezwa apsuliwe kichwa afanyiwe uchunguzi kwenye ubongo,akakataa.wakamshauri aache baadhi ya vyakula vya Unga ,huenda walidhania ni alergy, kweli alipata nafuu tuu lakini hali haikupona .
Alirudi TZ na kuendelea kuishi na ugonjwa huo wa kuvuja mafua mepesi.
Siku moja alipata kikohozi, akashauriwa na House girl wake atumie MANJANO MBICHI ACHEMSHE NA MAZIWA anywe kikombe kimoja kwa siku tatu asubuhi na jioni kwa ajili ya kutibu 'symptoms' za kikohozi.
Naam Alimuandalia dawa hiyo na kutumia usiku ,Ajabu kuamka asubuhi tatizo la mafua kutiririka limekoma, baada ya siku tatu na kikohozi nacho kikakoma.
Funzo:
Usidharau Tiba za asili.
Usimdharau mtu kwa muonekano wake.
Waliloshindwa Wahindi na Wazungu aliliweza Hose Girl wa Kitanzania.
Nathibitisha ,kuwa Maneno haya ni kweli, na Mungu Yu mwema kwa watu wake.