Mtanzania afukuzwa China kwa kushindwa kuheshimu taratibu za kujinga na ugonjwa wa covid-19

Mtanzania afukuzwa China kwa kushindwa kuheshimu taratibu za kujinga na ugonjwa wa covid-19

Maelezo ya mmoja wetu kuhusu hilo yako hivi:-

“Naomba kushare na ninyi jambo moja linasikitisha kidogo. Jana kwenye mitandao ya kijamii hapa China kumeibuka habari ya kuchafua jina letu Tanzania. Kuna mtanzania mwenzetu ameripotiwa kufanya mambo ambayo ni kinyume kabisa na maelekezo tunayopewa na Balozi wetu ya kutii maagizo ya mamlaka za hapa, na kufuata sheria. Inatajwa kuwa mtanzania mkazi wa Beijing anayefanya kazi kwa miaka mingi hapa China.

Huyu jamaa anatajwa kuwa alikuwa anaenda Tanzania lakini safari haikuendelea kwa kuwa Dubai hakuna ndege ya kwenda Tanzania akalazimika kurudi Beijing, lakini baada ya kurudi Beijing alikataa kuvaa mask (huku china kuvaa mask kwa mtu yeyote ni lazima), alitoa lugha ya kifedhuli kwa mamlaka husika, na baada ya kuambiwa awe kwenye karantini aliikuka agizo na alivuinja camera ya usalama kwenye eneo analokaa na kutoka nje”

Nyongeza ya taarifa.

“Order ya deportation mtanzania mwenzetu niliyewaambia asubuhi imetolewa”
View attachment 1406758View attachment 1406763
Kwa hiyo atatafutiwa usafiri maalum kumrudisha Tz au ni mpaka janga liishe ndio atarudishwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
safi kabisa..pumbavu...ujeuri aje afanye huku kwetu ambapo mambo shwari business as usual , na sio nchi strict kama china linapokuja suala la its people's health in line

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ubishi + ujuaji wakatu upo ugenini vya nini?
 
Hao wachina ni wastaarabu sana angekuwa North Korea tayari ndugu zake wangekuwa wanaanua matanga.
Analeta uchoko kwenye nchi za watu.?
Kule Philippines raising ameamuru polisi na jeshi kumtwanga risasi raia yeyote anayekaidi amri ya 'lockdown'. Dah! Sijasikia wale watetezi wa haki za binadamu wakitoa neno, na sijui wamevurugwa?
 
kama serikali imepata taarifa zake inabidi akifika tu airport asipewe hata ruhusa kuongea ni karantini tena yenye ulinzi wa police
 
amelikoroga

na akitua tu airport bongo ni direct kwenye quarantine kwa lazima...tena kwa garama zake binafsi.

Mkataa Pema Pabaya Panamwita





Sent using Jamii Forums mobile app
Hatuangalii yeye ni nani. Kama wasemavyo wenzetu "hakuna kwa nini wala kya nani", huyu jamaa ni moja kwa moja karantini ya siku 14 na akitoka huko ni safari ya kurudi kijijini kwao.
 
Sema ukwel pia baadh ya immigration officer huwa wanaboa sana hasa wanapokuona ngoz nyeus au unatokea nchi fulan maskin..

Tunaosafir safiri tunaelewa haya mambo,
ukikutwa una hasira za karibu unaweza hata ukaachia haja ndogo ofisi zao..
 
Back
Top Bottom