Mtanzania Afungua Kesi Mahakamani kuhusu kuzimwa kwa mitandao 2020, Aiomba Mahakama ichukue hatua kali

Mtanzania Afungua Kesi Mahakamani kuhusu kuzimwa kwa mitandao 2020, Aiomba Mahakama ichukue hatua kali

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hii ndio Taarifa mpya inayozunguka Duniani kwa sasa, Kwamba Mtanzania huyo Mzalendo na mwenye uthubutu, Bwana Kumbusho Dawson, ameifungulia kesi Serikali ya Tanzania Pamoja na Mamlaka za mawasiliano kwa jambo lile la kishamba la mwaka 2020 ili Mahakama ichukue hatua na itamke kwamba jambo kama lile lisirudiwe tena kwenye Nchi hii .

Screenshot_2024-07-15-16-12-40-1.png
Screenshot_2024-07-15-16-11-58-1.png

Nachukua nafasi hii kumpongeza kijana huyu kwa ujasiri huu, tena bila kuogopa kutekwa, badala ya kunyamaza na kuishia kulalamika kama Kinana na Warioba, yeye ameamua kuchukua hatua

Nakala: Nape Nnauye

Pia soma>> Watanzania wamefungiwa internet
 
Hiyo kesi wataomba declaratory orders tu ambazo haziko enforceable.

Hivi nchi ingechafuka 2020 hata hiyo kesi wangeenda kuifungua? Panapokuja maslahi ya kiusalama, dola itafanya lolote kuilinda nchi. Gharama za kuilinda amani ni ndogo kuliko za kuirejesha.

Pia wajipange kuthibitisha kwamba ilikuwa ni serikali inahusika, na sio technical problems za mtandao

Sasa hapo Magoti na Dawson wamekosa fursa ya kuangalia picha za ngono mtandaoni mwaka 2020, kimewauma mpaka leo
 
Hiyo kesi wataomba declaratory orders tu ambazo haziko enforceable.

Hivi nchi ingechafuka 2020 hata hiyo kesi wangeenda kuifungua? Panapokuja maslahi ya kiusalama, dola itafanya lolote luilinda nchi. Gharama za kuilinda amani ni ndogo kuliko za kuirejesha...
Wee jamaa una kiwango kidogo sana kichwani
 
Nadhani wote ni mashuhuda na wahanga kwa namna mtandao unavyozimwaga hasa kipindi cha uchaguzi, zitakumbukwa zaidi zile nyakati za uchaguzi wa 2020.

Sasa wakili na Mwanaharakati wa haki za binadamu Adv. Tito Magoti akimuwakilisha Bwn. Kumbusho Dawson Kagine, wamefungua kesi dhidi ya waziri wa Mawasiliano, Habari na teknolojia, Mamlaka ya udhibiti wa mawasiliano Tanzania pamoja na mwanasheria mkuu wa serikali.

Ni madai ya shauri hili kwamba mtandao ulizimwa kwa makusudi, na kwamba tukio hilo lilivunja haki kadhaa zinazolindwa na Katiba ya JMT. Mathalani, haki ya kupata, kutoa na kusambaza taarifa (Ib 18), uhuru wa kukutanika na kushirikiana na wegine (Ib 20(1)), na uhuru wa kushiriki shughuli za umma (Ib 21(1, 2)), na wajibu wa serikali kuheshimu katiba na sheria za nchi (Ib 26).

Vilevile wanadai kwamba, haki hizo zimekiukwa katika Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu; Mkataba wa Kimataifa unaohusu Haki za Raia na Siasa; na Mkataba wa Afrika wa Demokrasia, Uchaguzi na Utawala. Pia, Azimio la Baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu Kuendeleza, Kulinda na Kufurahia Haki ya Mtandao, Tamko la Afrika Kuhusu Haki ya na wa Uhuru Mtandao la mwaka 2017 na Kanuni za Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu Uhuru wa Kujieleza Afrika yamekiukwa.

Wanaiomba Mahakama itamke yakwamba:​
  1. kuzimwa mtandao kulivunja sheria na Katiba ya JMT na mikataba ya Kimataifa. Na hivyo, kulivunja haki za binadamu kama zilivyoainishwa hapo juu.​
  2. hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wote walioshiriki kuzima mtandao.​
  3. serikali izuiwe na ihakikishe hairudii, kuzima mtandao ikiwemo katika chaguzi zijazo: serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025.​
Shauri hili litatajwa kwa mara ya kwanza mbele ya Mhe. David Ngunyale tarehe 17.07.2024 Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam.​
IMG_5037.jpeg


Pia soma=> Gerson Msigwa: Tozo kwenye Miamala ya kutoa pesa bado ipo
 
Back
Top Bottom