Mtanzania Afungua Kesi Mahakamani kuhusu kuzimwa kwa mitandao 2020, Aiomba Mahakama ichukue hatua kali

Mtanzania Afungua Kesi Mahakamani kuhusu kuzimwa kwa mitandao 2020, Aiomba Mahakama ichukue hatua kali

Hiyo kesi wataomba declaratory orders tu ambazo haziko enforceable.

Hivi nchi ingechafuka 2020 hata hiyo kesi wangeenda kuifungua? Panapokuja maslahi ya kiusalama, dola itafanya lolote kuilinda nchi. Gharama za kuilinda amani ni ndogo kuliko za kuirejesha...
Mwenda...wazimu wewe Uchaguzi ni tukio la kuhatarisha usalama wa nchi????,Kivipi...
 
Huyo sio mzalendo labda ni mwoga kama dem mwenye bikra yake nimuona mzalendo kama angeshitaki serikali ya jiwe kipindi hicho
Serikali ni serikali, hakuna serikali ya jiwe au ya Samiah. Ndio maana Deni la serikali analipa rais aliyepo madarakani. Halafu jifunze kuwakubali watu hata kwa kidogo wanachofanya.
 
Huyo sio mzalendo labda ni mwoga kama dem mwenye bikra yake nimuona mzalendo kama angeshitaki serikali ya jiwe kipindi hicho
Wewe ndio muoga wa kwanza, uliyejificha kwa jina bandia. Kwakweli nyani haoni kundule.
 
Hiyo kesi wataomba declaratory orders tu ambazo haziko enforceable.

Hivi nchi ingechafuka 2020 hata hiyo kesi wangeenda kuifungua? Panapokuja maslahi ya kiusalama, dola itafanya lolote kuilinda nchi. Gharama za kuilinda amani ni ndogo kuliko za kuirejesha...
Tanzania bado sana, kama ina watu dizain yako basi tuna safari ndefu sana
 
Ukitafakari vizuri Ni kama vile onyo Fulani , Kama vile Msirudie tena.
Tukioa la kuzima internet Nchi nzima lina hatarisha Usalama wa Taifa.

Ikiwemo Magaidi na watu wasio wema wanaweza kuingilia Mifumo ya Nchi na kufanya uharifu Mkubwa.

Wakatu huo huo wanaweza kupoteza ushahidi wa uharifu wao...sio jambo dogo la kuliacha lipite...
 
Hiyo kesi wataomba declaratory orders tu ambazo haziko enforceable.

Hivi nchi ingechafuka 2020 hata hiyo kesi wangeenda kuifungua? Panapokuja maslahi ya kiusalama, dola itafanya lolote kuilinda nchi. Gharama za kuilinda amani ni ndogo kuliko za kuirejesha...
Machafuko ingeleta wewe chawa. Kama hujui kitu Kaa kimya. Eti Usalama wa nchi, wakati mpaka Leo watu wanatekwa na kupotezwa bila kujulikana.
 
Hiyo kesi wataomba declaratory orders tu ambazo haziko enforceable.

Hivi nchi ingechafuka 2020 hata hiyo kesi wangeenda kuifungua? Panapokuja maslahi ya kiusalama, dola itafanya lolote kuilinda nchi. Gharama za kuilinda amani ni ndogo kuliko za kuirejesha.

Pia wajipange kuthibitisha kwamba ilikuwa ni serikali inahusika, na sio technical problems za mtandao

Sasa hapo Magoti na Dawson wamekosa fursa ya kuangalia picha za ngono mtandaoni mwaka 2020, kimewauma mpaka leo
Chawa anayejali tumbo pekee. Kizazi Cha kijinga Sana.
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshitakiwa kikatiba katika Mahakama Kuu ya Tanzania iliyopo Dar es Salaam kuhusu tukio la kuzima mtandao (internet shutdown) wakati wa uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba, 2020.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wakili Tito Elia Magoti anayemwakilisha mdai, shauri hilo la kikatiba limefunguliwa na Kumbusho Dawson Kagine, mtumiaji wa mitandao ya kijamii ambaye pia Katibu Mtendaji wa Reach Out Tanzania, asasi isiyokuwa ya kiserikali yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam ikifanya kazi ya kuhamasisha umma kuhusu athari za kuzimwa kwa mtandao.

Tito akiwa na Wakili Mwenza Alphonce Lusako wameeeleza kuwa shauri hilo limefunguliwa kwa maelekezo ya mteja wao ambaye ni Kumbusho dhidi ya Waziri Wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

“Ni madai ya mteja wetu kwamba mtandao ulizimwa kwa makusudi, na kwamba tukio hilo lilivunja haki kadhaa zinazolindwa na Katiba ya JMT. Mathalani, haki ya kupata, kutoa na kusambaza taarifa (Ib 18), uhuru wa kukutanika na kushirikiana na wegine (lb 20(1)), na uhuru wa kushiriki shughuli za umma (Ib 21(1, 2)), na wajibu wa serikali kuheshimu katiba na sheria za nchi (Ib 26)” Ameeleza Tito.

Aidha ameeleza kuwa haki hizo zimekiukwa katika Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu, Mkataba wa Kimataifa unaohusu Haki za Raia na Siasa na Mkataba wa Afrika wa Demokrasia Uchaguzi na Utawala, pamoja na matamko mbalimbali kama Azimio la Baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu Kuendeleza, Kulinda na Kufurahia Haki ya Mtandao, Tamko la Afrika Kuhusu Haki ya na wa Uhuru Mtandao la mwaka 2017 na Kanuni za Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu Uhuru wa Kujieleza Afrika.

Kumbusho baada ya kufungua shauri hilo, ameitaka mahakama itamke kwamba kuzimwa mtandao kulivunja sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mikataba ya Kimataifa na hivyo kulivunja haki za binadamu, serikali izuiwe na ihakikishe hairudii, kuzima mtandao ikiwamo katika chaguzi zijazo za Serikali za Mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025. Pia ameitaka Mahakama itamke kuwa hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wote walioshiriki kuzima mtandao.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wakili Tito, Shauri hili litatajwa kwa mara ya kwanza mbele ya Jaji David Ngunyale tarehe 17 Julai 2024 Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam.
 
Unafunguaje kesi uchwara hivo unaacha kufungua kesi dhidi ya uuzwaji wa maliasili za Tanzania Kwa waarabu?.Huyu ni wakili uchwara kabisa na ni chawa na lengo lake ni kumchafua mzalendo wa wakati ule
 
Unafunguaje kesi uchwara hivo unaacha kufungua kesi dhidi ya uuzwaji wa maliasili za Tanzania Kwa waarabu?.Huyu ni wakili uchwara kabisa na ni chawa na lengo lake ni kumchafua mzalendo wa wakati ule
Uzalendo una wigo mpana,kipaumbele cha mfungua shitaki ni ukiukwaji wa makusudi ambao Serikali imekuwa ikiutumia ili kupora ushindi kwenye uchaguzi na kama kesi itatendewa haki basi tutakuwa salama kuanzia sasa na chaguzi zote zitakazofuata.
 
Back
Top Bottom