Mtanzania Afungua Kesi Mahakamani kuhusu kuzimwa kwa mitandao 2020, Aiomba Mahakama ichukue hatua kali

Mtanzania Afungua Kesi Mahakamani kuhusu kuzimwa kwa mitandao 2020, Aiomba Mahakama ichukue hatua kali

Umeme ulivyokuwa ukikatika katika miaka hiyo anamshitaki nani hasa Tanesco au mitandao?

Sababu mitandao kufanya kazi hutegemea uwepo wa umeme kwenye minara yao

Hii kesi sijaielewa vizuri

Kila la heri kwa mshtaki mitandao
 
Issue nii nani alifanya mtandao usipatikane ni Tanesco supplier wa umeme kwenye milimgoti ya mawasiliano kwa sababu ya maji ya kuendesha mitambo kuwa chini au ni milingoti ya kurusha network?

Kesi nyepesi sana hii hata mimi sio wakili ningeweza kuwa wakili wa kampuni za mitandao bure bila kulipwa hata mia anieleze vizuri mahaanadhani kitaalamu nini kilisababisha mbona angenikoma huyo
 
Tukioa la kuzima internet Nchi nzima lina hatarisha Usalama wa Taifa.

Ikiwemo Magaidi na watu wasio wema wanaweza kuingilia Mifumo ya Nchi na kufanya uharifu Mkubwa.

Wakatu huo huo wanaweza kupoteza ushahidi wa uharifu wao...sio jambo dogo la kuliacha lipite...
Kabisa mkuu , kuna watu wanaona mbali
 
Uneme ulivyokuwa ukikatika katika miaka hiyo anamshitaki nani hasa Tanesco au mitandao?

Sababu mitandao kufanya kazi hutegemea uwepo wa umeme kwenye minara yao

Hii kesi sijaielewa vizuri

Kila la heri kwa mshtaki mitandao
Karibu mahakamani kwa utetezi upande wa Jamhuri
 
Mbona wakati wa aliyetowa hiyo amri hamjafunguwa kesi?

Unafik huo.
Wanatafuta umaarufu tu wa kijinga

Mtandao kuzima kuna factors nyingi mojawapo hali ya hewa angani kiasi kuwa satellite Ray haiwezi fika kwenye dish undergroundi kurusha kwenye minara underground signal ya pili ni tatizo la Tanesco umeme kuzimika zimika kiasi kufanya minara mitumia umeme kutofanya kazi hadi hitilafu Tanesco imalizwe ,tatizo
La tatu ni huko kwa Internet providers kupata tatizo la kiufundi kwenye satellite yao iliyoko angani au tatizo la kiufundi la receiving information centre undergroundi on earth na ku distribute Mb nk kwenye simu kuwa accessible kwenye Internet

Anamshitaki nani sasa kwenye hiyo sheet ya mashtaka? Ataishia kulipa mamilioni ya legal costs kama hajielewi anatafuta umaarufu wa kijinga
.hiyo kesi sio rahisi kama anavyodhani
 
Wanatafuta umaarufu tu wa kijinga

Mtandao kuzima kuna factors nyingi mojawapi hali ya hewa angani kiasi kuwa satellite Ray haiwezi fika kwenye dish undergroundi kurusha kwenye minara underground signal ya pili ni tatizo la Tanesco umeme kuzimika zimika kiasi kufanya minara mitumia umeme kutofanya kazi hadi hitilafu Tanesco imalizwe ,tatizo
La tatu ni huko kwa Internet providers kupata tatizo la kiufundi kwenye satellite yao iliyoko angani au tatizo la kiufundi la receiving information centre undergroundi on earth na ku distribute Mb nk kwenye simu kuwa accessible kwenye Internet

Anamshitaki nani sasa kwenye hiyo sheet ya mashtaka? Ataushia kulipa mamilioni ya legal costs kama hajielew8 anafuta umaarufu wa kijinga
.hiyo kesi sio rahisi kama anavyodhani
Kijana usinifundishe mambo ya telecommunications.

Kwa kukujuza tu, mitandao ya Tanzania haitegemei satellites, kuna marine cables, miaka mingi sana.
 
Kwa nini mkuu?
Ili uwe na akili unatakiwa uunge mkono hoja yake. Ukiwa tofauti naye tu basi ujue lazima akuone mjinga.
Hiyo ndio kanuni ya baadhi ya watu humu.
 
Karibu mahakamani kwa utetezi upande wa Jamhuri
Yaani hapo sijaingia kwa undani niko juu juu tu

Siri ya uwakili hatakiwi kuonyesha hoja zake zote nzito zingine unabakiza utatoa mahakamani unabakiza kidogo kumtahadharisha wakili huyo mpeleka kesi mahakamani kuwa kuna issues


Check and take into consideration these preliminary issues before taking this case as the advocate of this case
Ni red flag kwa wakili aki go ahead sio big issue tukutane mahakamani
 
Nadhani wote ni mashuhuda na wahanga kwa namna mtandao unavyozimwaga hasa kipindi cha uchaguzi, zitakumbukwa zaidi zile nyakati za uchaguzi wa 2020.

Sasa wakili na Mwanaharakati wa haki za binadamu Adv. Tito Magoti akimuwakilisha Bwn. Kumbusho Dawson Kagine, wamefungua kesi dhidi ya waziri wa Mawasiliano, Habari na teknolojia, Mamlaka ya udhibiti wa mawasiliano Tanzania pamoja na mwanasheria mkuu wa serikali.

Ni madai ya shauri hili kwamba mtandao ulizimwa kwa makusudi, na kwamba tukio hilo lilivunja haki kadhaa zinazolindwa na Katiba ya JMT. Mathalani, haki ya kupata, kutoa na kusambaza taarifa (Ib 18), uhuru wa kukutanika na kushirikiana na wegine (Ib 20(1)), na uhuru wa kushiriki shughuli za umma (Ib 21(1, 2)), na wajibu wa serikali kuheshimu katiba na sheria za nchi (Ib 26).

Vilevile wanadai kwamba, haki hizo zimekiukwa katika Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu; Mkataba wa Kimataifa unaohusu Haki za Raia na Siasa; na Mkataba wa Afrika wa Demokrasia, Uchaguzi na Utawala. Pia, Azimio la Baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu Kuendeleza, Kulinda na Kufurahia Haki ya Mtandao, Tamko la Afrika Kuhusu Haki ya na wa Uhuru Mtandao la mwaka 2017 na Kanuni za Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu Uhuru wa Kujieleza Afrika yamekiukwa.

Wanaiomba Mahakama itamke yakwamba:​
  1. kuzimwa mtandao kulivunja sheria na Katiba ya JMT na mikataba ya Kimataifa. Na hivyo, kulivunja haki za binadamu kama zilivyoainishwa hapo juu.​
  2. hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wote walioshiriki kuzima mtandao.​
  3. serikali izuiwe na ihakikishe hairudii, kuzima mtandao ikiwemo katika chaguzi zijazo: serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025.​
Shauri hili litatajwa kwa mara ya kwanza mbele ya Mhe. David Ngunyale tarehe 17.07.2024 Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam.​
View attachment 3043144
Ukienda kusoma andiko langu la “SAUTI YA KESHO: Safari ya Uhuru Katika Vyombo vya Habari na Mtandao Tanzania” utagundua niligusia hili suala katika safari ya kuelekea #TanzaniaTuitakayo 👇🏼.

IMG_5040.jpeg
 
Kama wanaingiza chochote kitu kwa kufungua hiyo kesi naona ni sawa tu. Tunaita ujasiriamali. Washinde au wasishinde kwenye hiyo kesi hakutakuwa na madhara yoyote kwa serikali ya awamu ya 6 chini ya Dr Mama Samia. Wananchi wasiwe na hofu.
Sijakuelewa hofu ya nn kuna vita? Na wananchi ni akina nani hao ambao hawatakiwi kuwa na wasiwasi? Kwamba walivyozima mtandao ilikuwa sahihi? Yaani unaona sawa! Kwahiyo mtu asidai haki au?
 
Kijana usinifundishe mambo ya telecommunications.

Kwa kukujuza tu, mitandao ya Tanzania haitegemei satellites, kuna marine cables, miaka mingi sana.
Marine cable ndio inarusha hewani? Ili kuwafikia watumiaji popote Tanzania? Mijini na vijijini?
 
Hii ndio Taarifa mpya inayozunguka Duniani kwa sasa, Kwamba Mtanzania huyo Mzalendo na mwenye uthubutu, Bwana Kumbusho Dawson, ameifungulia kesi Serikali ya Tanzania Pamoja na Mamlaka za mawasiliano kwa jambo lile la kishamba la mwaka 2020 ili Mahakama ichukue hatua na itamke kwamba jambo kama lile lisirudiwe tena kwenye Nchi hii .


Nachukua nafasi hii kumpongeza kijana huyu kwa ujasiri huu, tena bila kuogopa kutekwa, badala ya kunyamaza na kuishia kulalamika kama Kinana na Warioba, yeye ameamua kuchukua hatua

Nakala: Nape Nnauye
Ule ulikuwa ni ushamba jazz band! Shwaini wakubwa!
 
Back
Top Bottom