Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kabisa mkuu , kuna watu wanaona mbaliTukioa la kuzima internet Nchi nzima lina hatarisha Usalama wa Taifa.
Ikiwemo Magaidi na watu wasio wema wanaweza kuingilia Mifumo ya Nchi na kufanya uharifu Mkubwa.
Wakatu huo huo wanaweza kupoteza ushahidi wa uharifu wao...sio jambo dogo la kuliacha lipite...
Karibu mahakamani kwa utetezi upande wa JamhuriUneme ulivyokuwa ukikatika katika miaka hiyo anamshitaki nani hasa Tanesco au mitandao?
Sababu mitandao kufanya kazi hutegemea uwepo wa umeme kwenye minara yao
Hii kesi sijaielewa vizuri
Kila la heri kwa mshtaki mitandao
Wanatafuta umaarufu tu wa kijingaMbona wakati wa aliyetowa hiyo amri hamjafunguwa kesi?
Unafik huo.
Kijana usinifundishe mambo ya telecommunications.Wanatafuta umaarufu tu wa kijinga
Mtandao kuzima kuna factors nyingi mojawapi hali ya hewa angani kiasi kuwa satellite Ray haiwezi fika kwenye dish undergroundi kurusha kwenye minara underground signal ya pili ni tatizo la Tanesco umeme kuzimika zimika kiasi kufanya minara mitumia umeme kutofanya kazi hadi hitilafu Tanesco imalizwe ,tatizo
La tatu ni huko kwa Internet providers kupata tatizo la kiufundi kwenye satellite yao iliyoko angani au tatizo la kiufundi la receiving information centre undergroundi on earth na ku distribute Mb nk kwenye simu kuwa accessible kwenye Internet
Anamshitaki nani sasa kwenye hiyo sheet ya mashtaka? Ataushia kulipa mamilioni ya legal costs kama hajielew8 anafuta umaarufu wa kijinga
.hiyo kesi sio rahisi kama anavyodhani
Ili uwe na akili unatakiwa uunge mkono hoja yake. Ukiwa tofauti naye tu basi ujue lazima akuone mjinga.Kwa nini mkuu?
Yaani hapo sijaingia kwa undani niko juu juu tuKaribu mahakamani kwa utetezi upande wa Jamhuri
Pascal Mayalla inabidi ufanye kitu wana JF waamini wewe ni wakili msomi mwenye manufaa kwa jamii. Siyo kwa kuandamwa huku😂😂😂Pascal Mayalla yeye anaona sawa tu
Sure pasco ukimgusa penyewe akujibu analike na kutembeaJF raha...Atakuja hapa ku like basi
Aiseeehhh
Yule jamaa wa Chato alitamani malaika wazime mitandao sijui alikuwa ana matatizo gani.
Nadhani wote ni mashuhuda na wahanga kwa namna mtandao unavyozimwaga hasa kipindi cha uchaguzi, zitakumbukwa zaidi zile nyakati za uchaguzi wa 2020.
Sasa wakili na Mwanaharakati wa haki za binadamu Adv. Tito Magoti akimuwakilisha Bwn. Kumbusho Dawson Kagine, wamefungua kesi dhidi ya waziri wa Mawasiliano, Habari na teknolojia, Mamlaka ya udhibiti wa mawasiliano Tanzania pamoja na mwanasheria mkuu wa serikali.
Ni madai ya shauri hili kwamba mtandao ulizimwa kwa makusudi, na kwamba tukio hilo lilivunja haki kadhaa zinazolindwa na Katiba ya JMT. Mathalani, haki ya kupata, kutoa na kusambaza taarifa (Ib 18), uhuru wa kukutanika na kushirikiana na wegine (Ib 20(1)), na uhuru wa kushiriki shughuli za umma (Ib 21(1, 2)), na wajibu wa serikali kuheshimu katiba na sheria za nchi (Ib 26).
Vilevile wanadai kwamba, haki hizo zimekiukwa katika Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu; Mkataba wa Kimataifa unaohusu Haki za Raia na Siasa; na Mkataba wa Afrika wa Demokrasia, Uchaguzi na Utawala. Pia, Azimio la Baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu Kuendeleza, Kulinda na Kufurahia Haki ya Mtandao, Tamko la Afrika Kuhusu Haki ya na wa Uhuru Mtandao la mwaka 2017 na Kanuni za Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu Uhuru wa Kujieleza Afrika yamekiukwa.
Wanaiomba Mahakama itamke yakwamba:
kuzimwa mtandao kulivunja sheria na Katiba ya JMT na mikataba ya Kimataifa. Na hivyo, kulivunja haki za binadamu kama zilivyoainishwa hapo juu. hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wote walioshiriki kuzima mtandao. serikali izuiwe na ihakikishe hairudii, kuzima mtandao ikiwemo katika chaguzi zijazo: serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025.Shauri hili litatajwa kwa mara ya kwanza mbele ya Mhe. David Ngunyale tarehe 17.07.2024 Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam.View attachment 3043144
Sijakuelewa hofu ya nn kuna vita? Na wananchi ni akina nani hao ambao hawatakiwi kuwa na wasiwasi? Kwamba walivyozima mtandao ilikuwa sahihi? Yaani unaona sawa! Kwahiyo mtu asidai haki au?Kama wanaingiza chochote kitu kwa kufungua hiyo kesi naona ni sawa tu. Tunaita ujasiriamali. Washinde au wasishinde kwenye hiyo kesi hakutakuwa na madhara yoyote kwa serikali ya awamu ya 6 chini ya Dr Mama Samia. Wananchi wasiwe na hofu.
Marine cable ndio inarusha hewani? Ili kuwafikia watumiaji popote Tanzania? Mijini na vijijini?Kijana usinifundishe mambo ya telecommunications.
Kwa kukujuza tu, mitandao ya Tanzania haitegemei satellites, kuna marine cables, miaka mingi sana.
Profession yake na siyo professional yakeAngalau anaonyesha ujasiri na kuitendea haki professional yake..
Ule ulikuwa ni ushamba jazz band! Shwaini wakubwa!Hii ndio Taarifa mpya inayozunguka Duniani kwa sasa, Kwamba Mtanzania huyo Mzalendo na mwenye uthubutu, Bwana Kumbusho Dawson, ameifungulia kesi Serikali ya Tanzania Pamoja na Mamlaka za mawasiliano kwa jambo lile la kishamba la mwaka 2020 ili Mahakama ichukue hatua na itamke kwamba jambo kama lile lisirudiwe tena kwenye Nchi hii .
Nachukua nafasi hii kumpongeza kijana huyu kwa ujasiri huu, tena bila kuogopa kutekwa, badala ya kunyamaza na kuishia kulalamika kama Kinana na Warioba, yeye ameamua kuchukua hatua
Nakala: Nape Nnauye