Mtanzania aliyeuawa na Hamas alikuwa sehemu ya jeshi la Israel? Serikali itoe tamko Watanzania wangapi wameingizwa kwenye jeshi la Israel

Mtanzania aliyeuawa na Hamas alikuwa sehemu ya jeshi la Israel? Serikali itoe tamko Watanzania wangapi wameingizwa kwenye jeshi la Israel

Je, kwenye zile video wewe umeona yule Mtanzania alikuwa ameshika silaha yoyote ya Moto mikononi mwake na alikuwa anapambana na Wagamgambo wa Hamas? Je, umeona video ya namna hii??
Hata kama alikuwa Mwanajeshi au alikuwa yuko huko kwa ajili ya Kujifunza Mafunzo ya Kijeshi, bado hakustahili kuuawa na wale Wanamgambo wa Hamas, kwa sababu wakati walipomkamata mtu huyo hakuwa na silaha yoyote ya moto au kupambana na Wanamgambo wa Hamas, Sheria za Vita kote duniani zinakataza kuua raia wasio na silaha au kuua Wanajeshi ambao wamejisalimisha kwa majeshi pinzani kwenye maeneo yenye mapigano ya vita.
Kama alijiunga na jeshi ilikuwa haki yake kuuawa na angerudi bongo angeshitakiwa acheni kutetea upuuzi, bashe na makamba wanayajua haya sema wanaogopa kusema itwachafua kisiasa na hatujui vijana wetu wangapi wameingizwa idf
 
Good, unasemaje na Mtanzania amabe aliuawa na jeshi la Ukrat akiwa anapigana na wanajeshi wa Urusi- nae si alikua mwanafunzi?!! Alikua na hadhi ya kujiunga na jeshi la Vita la Urusi?!!

Enzi za Vita vya dunia, Watanzania wengi walipigana vita kwa kupelekwa mstari wa mbele mpaka huko Asia,walikua na vigezo zaidi kushinda Mataifa mengine ya kizungu?!!
Mpaka hapa unakiri uzi ulioanzisha hauna maana tena, kilichobaki ni kuhamisha magoli.

Kama vipi nenda kaanzishe uzi mwingine kumhusu huyo wa Urusi vs Ukraine.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hiyo ya kusomea kilimo ni kupoteza maboya kwa kuwa hawawezi kuweka kila kitu wazi
 
Picha ya Molel na huyo Mwanajeshi wa mchongo tofauti kabisaaaaaaa. Mtahangaika na propaganda lakini wapi? Islaeli imchukue mtu toka Tanzania awe askari wakati hata hapakuwa na vuguvugu la VITA? Ndani ya muda mfupi tayari aamniniwe kuingia Jeshini? Unawalingasha IDF na Talibani wanaookota vijana waliopigika maisha k upigana Jihadi? Uwongo wa kiwango cha rami
 
Kuna aliethibitisha Identity ya alieonekana akiuwawa mkuu?

Nani anauhakika kuwa ni huyo Joshua?
Kwani yule kijana wa kwanza aliyeuawa nani alikosea kuthibitisha kuutambua ule mwili? uliambiwa hakuwa yeye?

Kina identity na information nyinhi tu zinazotosha kutoa taarifa, kuanzia na chuo alichokuwa akisoma.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Mleta uzi kwa hiyo unafurahia kuuwawa kwa kijana Mollel kisa kauwawa na waislamu wenzako?
 
Nilivyoiona hile Video ya Joshua nimeanza kuwachukia sana hawa ndugu zetu wafia dini
 
Kwani yule kijana wa kwanza aliyeuawa nani alikosea kuthibitisha kuutambua ule mwili? uliambiwa hakuwa yeye?

Kina identity na information nyinhi tu zinazotosha kutoa taarifa, kuanzia na chuo alichokuwa akisoma.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Mkuu tuendelee kusubiri kila kitu kitawekwa wazi na muda. Uzuri ulimwengu wa sasa information zipo nje nje ni mtu ku dig tu nakupata ukweli.
 
Je, kwenye zile video wewe umeona yule Mtanzania alikuwa ameshika silaha yoyote ya Moto mikononi mwake na alikuwa anapambana na Wagamgambo wa Hamas? Je, umeona video ya namna hii??
Hata kama alikuwa Mwanajeshi au alikuwa yuko huko kwa ajili ya Kujifunza Mafunzo ya Kijeshi, bado hakustahili kuuawa na wale Wanamgambo wa Hamas, kwa sababu wakati walipomkamata mtu huyo hakuwa na silaha yoyote ya moto au kupambana na Wanamgambo wa Hamas, Sheria za Vita kote duniani zinakataza kuua raia wasio na silaha au kuua Wanajeshi ambao wamejisalimisha kwa majeshi pinzani kwenye maeneo yenye mapigano ya vita.
Weee umeenda kusoma chuo Tel Aviv hamna hata tone la Vita huko Gaza kafata nini na yeye ni mgeni??
 
Jamaa alitukanwa sana kule twitter
Screenshot_20231217-213440.png
 
Mtuma picha umekurupuka kwa macho ya kawaida na kwa msaada wa DNA hao ni watu wawili tofauti
 
Kama alijiunga na jeshi ilikuwa haki yake kuuawa na angerudi bongo angeshitakiwa acheni kutetea upuuzi, bashe na makamba wanayajua haya sema wanaogopa kusema itwachafua kisiasa na hatujui vijana wetu wangapi wameingizwa idf
Pole yako sana wewe mtu, hii inathibitisha ni kiasi gani ulivyo mjinga na zumbukuku. Hivi unafikiri Wanajeshi wa Tanzania waliopo kwenye vitengo mbalimbali vya ulinzi kama vile Usimamizi wa Rada za Kijeshi, Opereta wa Ndege na Meli za Kijeshi pamoja na Waendeshaji au Wahandisi wa Mitambo mbalimbali ya kijeshi kama vile Vifaru, Mafunzo yao ya kijeshi kuhusu vifaa hivyo wote wamesomea hapa Tanzania? Je, hapa Tanzania tuna viwanda vya kutengeneza au kuunda vifaa vya kijeshi kama vile Vifaru, Meli, Ndege au Rada za Kijeshi?
 
Good, unasemaje na Mtanzania amabe aliuawa na jeshi la Ukrat akiwa anapigana na wanajeshi wa Urusi- nae si alikua mwanafunzi?!! Alikua na hadhi ya kujiunga na jeshi la Vita la Urusi?!!

Enzi za Vita vya dunia, Watanzania wengi walipigana vita kwa kupelekwa mstari wa mbele mpaka huko Asia,walikua na vigezo zaidi kushinda Mataifa mengine ya kizungu?!!
Mbona yule story yake ilikuwa wazi.

Mosi alikuwa mwanafunzi na aliyekua mfungwa gerezani kutokana na makosa aliyoyafanya nchi ya ugenini.

Pili baada ya vita kutokea Russia walikua wanatumia mercenaries wa Wagner group ambao yule kijana ndio aliingia nao makubaliano nao.

Tatu yeye aliiingia makubaliano ya kununua uhuru wake(kuachiwa huru) akikubali kuingia vitani licha ya kutokua na mafunzo ya kijeshi.

Katika vita aliuwawa na ilielezwa sababu ya yeye kujikuta uwanja wa vita ni makubaliano ya kimkataba aliyoyafanya yeye kuingia vitani angali sio mwanajeshi pengine leo angekuwepo hai akitumikia kifungo kama asingetaka kununua uhuru wake kwa kuingia mstari wa mbele vitani.

Mtanzania yule hakuwa mwanajeshi bali mwanafunzi aliyeenda kusoma katika harakati za kusoma alivunja sheria za huko na kuwekwa gerezani kamba ambavyo wapo hata watanzania wengine huko gerezani Hongkong tangu 2013.

Ndio maana hata ya kufariki ilijulikana wazi amefia uwanja wa vita kama mpiganaji sio mateka/raia

Huwezi kunishawishi katika nchi iliyo vitani na kijana ni mwanajeshi kama wanavyodai anakatiza mtaani pekeyake akiwa na nguo ya wazi juu, jeans ,baiskeli , hana hata kisu cha kujihami hii inawezekanaje kweli ndugu?
 
kuna watu ni faida kubwa sana kwao mkiendelea kubishana hivi na mkiamini mnavyoamini.
 
swali langu ni rahisi sana, waliouwawa kwenye mashambulizi ya Hamas ndani ya Israel ni wengi sana, kwanini hili la mtanzania ndio linaonekana kubwa na kusambaa mno?
 
Mkuu tuendelee kusubiri kila kitu kitawekwa wazi na muda. Uzuri ulimwengu wa sasa information zipo nje nje ni mtu ku dig tu nakupata ukweli.
Ukweli utajulikana taratibu hata ID itatolewa kabisa..

Yupe wa Ukraine watu walikubali kwamba yeye alijiunga na jeshi kabisa.
 
Hii kitu inafichwa fichwa sijuwi Kwa maslahi ya nani.Kwa sababu kwenye video wale Hama wanamuhoji kuwa we Sio Muyahudi Kwa nini umekuja kuuwa ndugu zetu??Hebu tueleze ukweli .Yule alipewa visa kuwa anaenda kusomea kilimo ila tamaa ya pesa ikamfanya akaingia jeshini na kauwa raia wengi sana huko Gaza.Ila mihemko ya wabongo utadhani wanachambua mpira hawataki kutafuta ukweli.
Acha kudanganya watu.
 
Hiyo picha ukiangalia vizuri iko edited .

Branch hiyo inaitwa Israel Border Police(Magav).

Na ukiangalia requirements za kujiunga na unit hiyo huyo bwana mdogo hakuwa anafit hata kwa asilimia 10% hana vigezo.

Pili operation za majeshi kubadilishana mbinu za kijeshi zipo sana na hazijaanza leo nakuwekea hapa bona fide evidence mjionee

Jeshi moja kubadilishana mbinu za kimedani ni kawaida

Hii ni jeshi la US na IsraelView attachment 2847801

Hii ilikuwa ni hapa hapa Tanzania.

Tusitafute justification kusingizia Joshua alikua mwanajeshi wakati hakuna uthibitsho hata chembe wa yeye kuwa mwanajeshi zaidi ya kuwa mwanafunzi aliyetambulika kutokea chuo cha kilimo.
Hata Tarimo watu walijua yupo Urusi kama mwanafunzi lakini alipouawa kule Bakhmut ndipo ukweli ulipodhihiri kuwa alikuwa akipigana upande wa Urusi.
 
Back
Top Bottom