Mtanzania Anarudishwa Bongo Kutoka Marekani. Ana USD 10,000 (23M Tshs) Tu. Mnampa Ushauri Aitumieje?

Mtanzania Anarudishwa Bongo Kutoka Marekani. Ana USD 10,000 (23M Tshs) Tu. Mnampa Ushauri Aitumieje?

DocJayGroup

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2020
Posts
1,654
Reaction score
3,346
Jamaa alipatwa na misukosuko ughaibuni na makaratasi yake ya uhamiaji yakaharibika kabisa. Badala ya kuendelea kuishi USA pasipo kujua mbele wala nyuma, ameamua arudi Tanzania akapambane huko. Anafanya kitu kinaitwa voluntary deportation ambayo badala ya kuzolewa na kurudishwa kwa lazima, unasalimu amri mwenyewe na kuamua kujirudisha kwenu kwa gharama zako mwenyewe.

Jamaa amejenga nyumba moja Tanzania kijijini lakini. Hana elimu ya chuo sababu misuko suko aliyokumbana nayo ilifanya ashindwe kusoma chuo USA. Hana ndugu wa kutegemea Tanzania wala USA. Na anarudi na USD 10,000 peke yake.

Naomba tumshauri kwamba aifanyie kazi gani hio hela angalau aingize kitu kidogo au ili maisha yasimpige. Asanteni wana JF.
 
Asiogope,akija asijimwambafai kama mtu alotoka States..ye ajifanye katoka Ulyankulu na achane na marafiki wale wa bata wanaopigaga story eti fulani yuko states.. kama alipiga kozi mshenzi huko ataajiriwa hata na taasisi kubwa wanaogopa sana wakiskia mtu kapiga kozi States...vinginevyo afanye ujasiliamali ingawa utamcost sana kwa hela hiyo mpaka asimame
 
Kikubwa sana kuliko vyote kwanza mwambie atulie sana, tena mno! Atulize kichwa sana alafu akiona kichwa kimetulia kabisaaaaaa AKUBALI KISAIKOLOJIA KWAMBA KARUDI TANZANIA NA MAISHA YAKE YATAKUWA HAPA, asafishe ubongo aondoe ule ujinga kwamba walioko Tanzania wengi ni washamba, hawajui ku struggle, wavivu, wamepitwa na wakati na yeye ni mjanja kuliko ma age mate wake. Hapa ndio kunakuwaga na mtihani wa kwanza, akiuvuka huu aaaah mbona milioni 20 nyingi tu na atasavaivu. Akicheza tu kaisha jumla, nina mifano mingi sana ya waliorudi wakaishia kuwa walevi mbwa wala bwimbwi na kuishia kuwa malofa ajabu!
 
Hili huwa ni swali gumu sana, kufanya kitu inategemea na mambo mengi kumhusu ambayo hatuyajui...

Fursa zinategemea eneo ulilopo, zinategemea wewe ni expert wa nini au una uzoefu wa kitu gani, zina tegemea pia unapenda nini? Zinategemea mambo mengi mno, inaweza kutegemea pia kama una mke au familia..

Kumshauri mtu cha kufanya ni kumpoteza tu, yeye mwenyewe anatakiwa ajue anataka nini, kila mtu ana interests zake na malengo yake, na pia kitu unachokichukia wewe kuna watu wanakipenda na kinawalipa, biashara iliyosababisha wewe ufilisike kuna watu wanaendelea kupiga faida mpaka kesho!
 
Jamaa alipatwa na misukosuko ughaibuni na makaratasi yake ya uhamiaji yakaharibika kabisa. Badala ya kuendelea kuishi USA pasipo kujua mbele wala nyuma, ameamua arudi Tanzania akapambane huko. Anafanya kitu kinaitwa voluntary deportation ambayo badala ya kuzolewa na kurudishwa kwa lazima, unasalimu amri mwenyewe na kuamua kujirudisha kwenu kwa gharama zako mwenyewe.

Jamaa amejenga nyumba moja Tanzania kijijini lakini. Hana elimu ya chuo sababu misuko suko aliyokumbana nayo ilifanya ashindwe kusoma chuo USA. Hana ndugu wa kutegemea Tanzania wala USA. Na anarudi na USD 10,000 peke yake.

Naomba tumshauri kwamba aifanyie kazi gani hio hela angalau aingize kitu kidogo au ili maisha yasimpige. Asanteni wana JF.

Ningekua mimi ndiye yeye. Kwanza ningejifunza vitu hivi..(na assume kama mtu katoka nje basi ana exposure na ni mtu asiye na ugomvi wa vitabu)


1. Ngetumia mwaka mzima kujifunza forex

2. Ningejifunza jinsi ya kuwekeza kwenye crypto currencies..

3. Ndani ya mwaka huo mmoja ningejifunza digital marketing na SEO!

4. Ningejiuliza nini napenda then ningefungua youtube channel ili nitengeneze videos za nnacho penda.. Na kwa sababu nimesha jifunza SEO hapo kwenye namba 3 basi hapa nisinge teseka! Maana knowledge ya SEO ndio ningeitumia ku rank video zangu youtube!!

hii ni nzuri maana in the long run ina faida!

Baada ya hapo ningefanya hivi...

1. Ningetoa 1000usd ni nunue laptop mpya (kama hana kabisa ila kama anayo anaweza acha).. hii ni muhimu maana hii ndio kama jembe shambani, lazima uwe nalo ili ulime!

2. Ningetenga 3000usd na kufund account ya forex (ningefanya hivi baada ya kuhakikisha nime practise vya kutosha na nna strategy inayo eleweka otherwise ningeacha kwanza).

3. Ningetumia 2000usd na kuwekeza kwenye coin kama ENJIN, eCASH, ZIL etc pia ningeangalia hizi meme coins hasa hizi mpya mpya na kuziwekea walau dola 500...

Hapo ningekua nimebakiwa na 4000usd.. then hii 4000 usd ningefanya hivi..

A. Ningetoa 1000usd nifungue kampuni ya digital marketing.. na hapa ningekomaa sana na kazi za freelancing za nje!

B. Kwa sababu nna laptop (rejea namba 1 hapo juu) basi ningefungua youtube channel na ninge hakikisha natenga 500usd kwa ajili ya kununua mic nzuri!

Mpaka hapo nimebakiwa na kama 2500usd hivi! Hii ningeiweka reserve incase of anything pamoja na matumizi ya hapa na pale!
 
kam aliondoka huku kitambo basi aina ya maisha ya huku yatakua mageni kwake mi ningemshauri arejee huko kijijin alikojenga nyumba akajenge nyingine ili hio pesa isije ikaisha kabla ht hajaelewa nn kinaendelea,then akishayasoma maisha ya huku basi atajua aanze vipi, hawez akaanzisha biashara akafanikiwa km mazingira husika hajayaelewa vizuri
 
dah comment za watu zinafurahisha sana...

mkali asiogope mwambie adondoke tu bongoland ila aache unyamwezi huku kuna wenyewe wenye anga zao kama wako Denver au Miami vile.....

24mil asiingie kichwachwa kwenye risk business aanzie kwenye non risk anapiga mdogomdogo anakula anavaa na kusave kidogo huku akiisoma game....24mil kibongo bongo kama mpambanaji ndani mwaka inabadili ubao...
 
Back
Top Bottom