Jamaa alipatwa na misukosuko ughaibuni na makaratasi yake ya uhamiaji yakaharibika kabisa. Badala ya kuendelea kuishi USA pasipo kujua mbele wala nyuma, ameamua arudi Tanzania akapambane huko. Anafanya kitu kinaitwa voluntary deportation ambayo badala ya kuzolewa na kurudishwa kwa lazima, unasalimu amri mwenyewe na kuamua kujirudisha kwenu kwa gharama zako mwenyewe.
Jamaa amejenga nyumba moja Tanzania kijijini lakini. Hana elimu ya chuo sababu misuko suko aliyokumbana nayo ilifanya ashindwe kusoma chuo USA. Hana ndugu wa kutegemea Tanzania wala USA. Na anarudi na USD 10,000 peke yake.
Naomba tumshauri kwamba aifanyie kazi gani hio hela angalau aingize kitu kidogo au ili maisha yasimpige. Asanteni wana JF.