Ningekua mimi ndiye yeye. Kwanza ningejifunza vitu hivi..(na assume kama mtu katoka nje basi ana exposure na ni mtu asiye na ugomvi wa vitabu)
1. Ngetumia mwaka mzima kujifunza forex
2. Ningejifunza jinsi ya kuwekeza kwenye crypto currencies..
3. Ndani ya mwaka huo mmoja ningejifunza digital marketing na SEO!
4. Ningejiuliza nini napenda then ningefungua youtube channel ili nitengeneze videos za nnacho penda.. Na kwa sababu nimesha jifunza SEO hapo kwenye namba 3 basi hapa nisinge teseka! Maana knowledge ya SEO ndio ningeitumia ku rank video zangu youtube!!
hii ni nzuri maana in the long run ina faida!
Baada ya hapo ningefanya hivi...
1. Ningetoa 1000usd ni nunue laptop mpya (kama hana kabisa ila kama anayo anaweza acha).. hii ni muhimu maana hii ndio kama jembe shambani, lazima uwe nalo ili ulime!
2. Ningetenga 3000usd na kufund account ya forex (ningefanya hivi baada ya kuhakikisha nime practise vya kutosha na nna strategy inayo eleweka otherwise ningeacha kwanza).
3. Ningetumia 2000usd na kuwekeza kwenye coin kama ENJIN, eCASH, ZIL etc pia ningeangalia hizi meme coins hasa hizi mpya mpya na kuziwekea walau dola 500...
Hapo ningekua nimebakiwa na 4000usd.. then hii 4000 usd ningefanya hivi..
A. Ningetoa 1000usd nifungue kampuni ya digital marketing.. na hapa ningekomaa sana na kazi za freelancing za nje!
B. Kwa sababu nna laptop (rejea namba 1 hapo juu) basi ningefungua youtube channel na ninge hakikisha natenga 500usd kwa ajili ya kununua mic nzuri!
Mpaka hapo nimebakiwa na kama 2500usd hivi! Hii ningeiweka reserve incase of anything pamoja na matumizi ya hapa na pale!