Mtanzania Anarudishwa Bongo Kutoka Marekani. Ana USD 10,000 (23M Tshs) Tu. Mnampa Ushauri Aitumieje?

Aingie kwenye ufugaji wa kuku na ng'ombe wa maziwa
Nimefanya ufugaji kuku toka mwaka 2008 mpk leo, sio rahisi na inahitaji mtaji mkubwa ili utoboe. Unatakiwa uwe na ardhi, mabanda, running capital, wateja wa uhakika na utaalam kwenye ufugaji otherwise utalia
 
Aende nchi za Europe. Baadhi elimu ni bure, kazi kupata ni rahisi sio kama USA.
Ukitolewa USA kwa deportation. Na nchi za European Union, Canada et al hauwezi pata viza. Unakuwa kwenye system yao. Hapa ni bongo tu au nchi nyingine za Africa
 
Mambo ya Youtube channel, forex etc watu wengi wanajaribu na hawatoboi ng'ooo. Atapoteza muda hapo na pesa itaisha na hamba kitu
 
Amtafute mwanamke wa kimachame aliyetulia, amuonyeshe namna ya kuwekeza hiyo pesa.
Ushauri wangu ni AKAE mbali kabisa na mademu wa Tz. Hio 24m itakuwa sifuri. Asitegemee mwanamke au mtu amsaidie kutoka. Ni yeye tu apambane ndio maybe ataweza
 
Nimefanya ufugaji kuku toka mwaka 2008 mpk leo, sio rahisi na inahitaji mtaji mkubwa ili utoboe. Unatakiwa uwe na ardhi, mabanda, running capital, wateja wa uhakika na utaalam kwenye ufugaji otherwise utalia
Biashara yeyote sio rahisi siku hizi.. changamoto nyingi sana. Enzi za wakina Mengi marehemu walivyoanza .. competition haikuwa kubwa sana kama siku hizi.
 
Watu sidhani wana pesa sana kama wakati wa Kikwete. Watu hawana pesa sasa ivi. Lakini watu ni wapambanaji sana wa fursa. Kwa hio japo sio watu wengi wenye 24m.. ila wenye hio hela wachache wanajua sana kuiwekeza vizuri sana na Teari wanajua biashara za Bongo vizuri. Sasa jamaa hapo ndio akienda kichwa kichwa 24 m inaisha fasta
 
Nipo hapa mkuu,
ww mpenzi ulinisikitisha sana siku moja. Ila mie bado nakupenda. Nikupe info tu za ile biashara yangu ya tours kwa sasa nimepaki tu magari na lodges hazifanyi kazi sana. Nimerudi ughaibuni huku kuna fursa nzuri za pe$$a. Bongo bado assets zangu zipo, na nitazifanyia kazi ila biashara huko covid nk zilivuruga. Ila nilihuzunika ile post fulani ukasema maneno badala ya kuniuliza.
 
Kama ni dereva anunue bajaji apige kazi boss yeye mwenyewe.atunze chombo vizuri.
Bajaji ni mkoa wowote inalipa na atajiamlia mwenyewe muda gani apumzike?
Never be ashamed of your hustle πŸ‘πŸ‘πŸ‘
 
Ningekuwa mimi hiyo pesa natoboa vizuri ila watu wengi walioishi nje huwa ni wagumu kukubali matokeo.Mfano anaeza kufika bongo akaishi hotel miezi 6,badala ya kufikana kutafuta dalali amtafutie chumba then atie godoro huku anasoma mchezio mtaani.
 
Anunue gari used ya 5m iliokaza ilio kama Van! Anunue mahotpot na kutafta wapishi wazuri wa mama ntilie kisha wapike na kuenda kuuza msosi kariakoo hatojuta
Extrovert uko vizuri. Problem hapo atahitaji nyumba Dar, gari aitengeneze ifae kuwa ya kutembeza chakula. Apate wafanyakazi wazuri. Hio inahitaji $$ zaidi na muda. Ila ni idea nzuri brother πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘
 
Anunue zile gari ndogo afanye Uber huku akijipanga vizuri kusoma mazingira ya huku bongoland, Mimi mtu akiniambia niende nje ya tanzania siendi ng'o maana ukirudi wenzako wamepiga hatua kubwa

Inategemea unaenda kufanya nini na unakifanyaje,

Kuna wale wapo wanafanya kazi sio za ujuzi na malipo ni ya kutosheleza kuishi huko tuu.

Kuna wale wanaosoma na wakimaliza wana struggle kidogo then wanarudi bila mtaji.

Kuna wale ambao wanafanya kazi za ujuzi na wana experience na pesa ni ndefu wanalipwa.

Hawa wote kinachobaki ni wanahusisha vipi akili zao na uwekezaji nyumbani.
Unatumiaje likizo zako kujifunza nini cha kufanya nyumbani, una watu wa aina gani supportive.

Maisha ya Udayaspora hayana formular [emoji3]
 
Anunue zile gari ndogo afanye Uber huku akijipanga vizuri kusoma mazingira ya huku bongoland, Mimi mtu akiniambia niende nje ya tanzania siendi ng'o maana ukirudi wenzako wamepiga hatua kubwa
Inategemea. Mimi binafsi USA ndio imenitoa. Ila mimi niko tofauti na waTz wengi. Nilikuja kutafta maisha. Naishi kwa kujinyima nk. Wabongo wengi wakija huku ni starehe tu na wanasahau nyumbani. Mwisho wa siku ndio inakuwa hivi. Ni kuwa na malengo. Kazi USA zipo nyingi. Ila Tz kazi za mshahara mzuri ni changamoto kwa wengi. Inategemea tu.
 
Ni kweli maisha ya diaspora hayana formula ila majority waishi Kwa shida heri tu kurudi nyumbani na huyu mleta mada alienda kwa shule lakini kufika kule akashindwa shule Sasa anaona arudi home wakati angekuwa bongoland angekuwa mbali sana, home is home tu mzee
 
Ww itakuwe umeishi nje ya Tz. Well said brother. Umechanganua vizuri sana. Need say no more.
 
Extrovert uko vizuri. Problem hapo atahitaji nyumba Dar, gari aitengeneze ifae kuwa ya kutembeza chakula. Apate wafanyakazi wazuri. Hio inahitaji $$ zaidi na muda. Ila ni idea nzuri brother πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘
Kwa hio pesa akija nayo kwangu mradi unasimama freshi tu! Mie tayari nina watu na gari ila mtaji wa kununua hayo ma vitu ndio sijapata bado ila haitahitaji zaidi ya 1M kuanza!

Asije akavamia biashara za kutumia mtaji mkubwa wakat hana uzoefu bora hela ibaki nyingi ya reserve hatosota sana kabla ya kuanza kuingiza faida. Anaweza fungua business ingine!
 
Hapana my dear. Mimi niko vizuri. Ili uhakikishe youtube channel yangu ni

Ndio mimi kwa hio channel. Na tz nimejiwekezea vizuri sana tu. Na nina makaratasi nasafiri vizuri sana tu. Hii mada hainihusu mimi.
 
Poa bro. Nitumie namba yako basi inbox.. nitawaunganisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…