Huu ni uhalisia ingawa kuna watu watakupinga sanaa, 2018 kuna mtoto wa mama angu mkubwa yule dogo alishajikatia tamaa bongo (std seven leaver), hataki kazi, hataki hata kujiendeleza kwa shughuli ndogo ndogo, akili na kila kitu chake kinawaza kuingia “Deben” (Durban). Mentality ya kuzamia ineshamuingia, by that time watoto wengi na mabro wa mtaani kwetu TMK wapo bondeni wanahustle, ikabidi tumpambanie dogo apate anachokitaka. Finally akafanikiwa kuingia kiwanja, alivyofika kule akajionea kwa macho yake maisha ya ndugu zetu mtaani, dogo akalast miezi tu akaomba atumiwe nauli arudi.
Hali inatisha sanaa, vijana wanauza roho, bongo wengine wameshaharibu (either waliondoka kwa misala au kuharibu home kwa kigezo cha kuzamia) kurudi nyuma wanaona sio kweli na ile mentality ya kuonekana failure wanaona bora wakaze tu.
Ushauri, ndugu na jamaa zangu, kwa SA hali ilivyo sasa kama hauna issue ya kueleweka au mtu (host) wa kukupokea na kukupa miongozo ya muhimu, achaa kabisa hizo ndoto, SA kumeharibika sanaa. Mbongo “last number” ameshaharibu sana kwa deals za uporaji, drugs n.k na hapendwi kabisa.