Mtanzania Dkt. Wendeline achaguliwa kuwa Mkurungenzi wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika anayesimamia Nchi 22

Mtanzania Dkt. Wendeline achaguliwa kuwa Mkurungenzi wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika anayesimamia Nchi 22

Aliwahi kutoka kwa sababu labda alikuwa kwenye kitengo ambacho huwezi kula kwa urefu wa kamba.Kwenye taasisi za serikali watu wanajali zaidi kula kwa urefu wa kamba kuliko cheo.
Ni mawazo kama haya ya kipotofu ya 'kula kwa urefu wa kamba' ndiyo yatatufanya tuendelee kuwashangilia wenzetu wanapopiga hatua za maendeleo. Nafasi na vyeo vingi serikalini vinatakiwa kuwa competitive ili watu kama huyu ndugu yetu wenye maono ya mbali na elimu kubwa waweze kushika nafasi strategic. Mfano sioni sababu kwanini kuna wakuu wa mikoa na wilaya wakuteuliwa tu na Rais! Ma RAS na ma DED wanatosha kuwa executives lakini wawe wamepatikana kwa ushindani. Mawaziri, wakuu wa taasisi mbali mbali, hawa wote wanatakiwa kuzipata hizo nafasi thru competition ili mwenye kuweza zaidi ndio awe kiongozi. Hawa wote wangekuwa wanatekeleza vision ya Taifa kwa mikakati madhubuti, siyo ya kichama.
 
Ndio jina lake anaitwa Zarau wale mnaosema majina mabaya yana nuksi kazi kwenu .Zarau huyooo kawa Mkurugenzi benki ya dunia Wenye majina ya mwanzo mazuri ya Billionaire, Tajiri,Mbarikiwa,Favour, Victory nk mpooooo? Tieni neno hapa
Hii imekaaje????
Maana huwa tunaambiwa mtoto usimpe jina baya mfano tabu/shida/masumbuko/mafuriko/pombe magufuli/wasira etc.
 
Hongera zake.

Kuna pongezi cobtroversial za kisiasa za Samia, lakini pia, kidiplomasia, mtu kupewa hizi nafasi ni kura ya imani kwenye uongozi wa serikali yake kutoka nchi nyingine, kwa hivyo serikali ya Tanzania inayoongozwa na rais Samia ina pongezi zake nayo.

Kuna diplomasia fulani ya nchi inahusika kupata hizi nafasi. Nchi ikipwaya kwenye diplomasia hizi, raia wake kupata nafasi hizi inakuwa ngumu.

Jana kuna mtu alikuwa anasema World Bank kuna Watanzania wengi, naona anakuwa vindicated.

Nchi ikipata watu wengi kama hawa kwenye kazi za UN, tukiwa na uongozi mzuri, tunaweza kuongeza ushawishi katika ajenda za muhimu.
..ajenda za muhimu kama zipi?
 
Tanzania kuwa na watu kwenye mashirika ya kimataifa ni sawa na sifuri..anamaliza mkataba wake wa kazi anarudi Tanzania kudowea uteuzi na kuwa bootlicker..ni jambo la kushangaza watu km sefue, omar issa, stergomena na wengine badala ya kusaidia nchi kwa kiwango walichofikia na kutengeneza ajira wao tena wanakuwa mzigo kwa hawa masikini waliowasomesha! angalia mfano wa watu walioelimika kama hawa Donald Kaberuka | SouthBridge ndicho wanapaswa kufanya..hata huyu zarau hana tofauti na hao, kwanza hata tu kuonyesha maandiko/publications alizofanya haijulikani, hizi nafasi wakati mwingine ni za ku-rotate kwa nchi na wala si kwa uwezo wa mtu!
 
Ni mawazo kama haya ya kipotofu ya 'kula kwa urefu wa kamba' ndiyo yatatufanya tuendelee kuwashangilia wenzetu wanapopiga hatua za maendeleo. Nafasi na vyeo vingi serikalini vinatakiwa kuwa competitive ili watu kama huyu ndugu yetu wenye maono ya mbali na elimu kubwa waweze kushika nafasi strategic. Mfano sioni sababu kwanini kuna wakuu wa mikoa na wilaya wakuteuliwa tu na Rais! Ma RAS na ma DED wanatosha kuwa executives lakini wawe wamepatikana kwa ushindani. Mawaziri, wakuu wa taasisi mbali mbali, hawa wote wanatakiwa kuzipata hizo nafasi thru competition ili mwenye kuweza zaidi ndio awe kiongozi. Hawa wote wangekuwa wanatekeleza vision ya Taifa kwa mikakati madhubuti, siyo ya kichama.
Watu wenye uwezo na maono hawatakiwi kwenye mfumo wa ajira nchi hii ndio maana kuna kuteuliwa tena kwa kujuana.
 
Back
Top Bottom