BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Umoja wa mataifa umemteua Ghaamid Abdulbasat kuwa mwanachama wa Kamati ya Ushauri (IAC) kwa niaba ya vijana Afrika na duniani kutekeleza itifaki ya Nagoya ya mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Bioanuwai/Mazingira.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, uteuzi wake unalenga kuimarisha utekelezaji wa mkataba Nagoya baada ya kuzinduliwa kwa mfumo wa kisera wa bioanuwai Desemba 2022 nchini Canada kwenye mkutano wa 15 wa wanachama (COP15) ambapo Tanzania ni mwanachama pia.
"Itifaki ya Nagoya ni makubaliano ya kimataifa yanayolenga kugawana kwa haki na usawa faida baina ya nchi zinazotokana na matumizi ya rasilimali za kijenetiki za mazingira," inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Kama mwanachama wa IAC, Abdulbasat atachangia katika maendeleo ya programu za kujenga uwezo zinazolena kuimarisha utekelezaji wa Itifaki ya Nagoya.
Akizunguma na Mwananchi, Abdulbasat amesema ni hatua kubwa kwake huku akihamasisha vijana wengine wasioamini katika uwezo wao hasa katika maeneo yao ya ubobezi kuamini kuwa wanaweza kufanikiwa zaidi ya walipo.
Pia uteuzi huo ni fursa kwa nchi kusogea karibu na wafanya maamuzi kwa kile kilichoelezwa kuwa kwa kawaida idara ya vijana huwa inawekwa pembezoni kidogo na hata mikataba mingine.
“Nipende kuwahamasisha vijana wengine wasioamini katika uwezo wao linapokuja suala la utaalamu katika eneo fulani kama wahandisi waamini kuwa wanaweza kuingia katika kamati kubwa duniani, vivyohivyo katika sekta ya afya, ubunifu, viwanda, tujifahamu kuwa tayari ni watalaamu,” alisema Abdulsadat na kuongeza
“Licha ya kuwa na ujuzi wa miaka mitatu tusiogopeshwe na watu wa wenye ujuzi wa zaidi ya miaka 10 na badla yake tutumie kama fursa kwa kuiga ujuzi kutoka kwao.
Abdulbasat anatoka kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Biodiversity Organization pia amepokea tuzo mbalimbali zikiwemo za Umoja wa Mataifa katika kuhamasisha, kushirikisha na kufundisha vijana kuhusu uhifadhi na utunzaji wa mazingira toka 2017.
MWANANCHI