DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mzeee endelea kumsadia kwa kumpelekea dola kadhaa

Na mm pia Nina ndugu yangu aishie Huko marekani anitwa loiruki
 
Sasa si ndo wee umsaidie hapo kwa kumuhifadhi na nk, huku ukisubiri ndugu zake wajitokezee.

Kumuacha ahangaike na huku unamtangaza, si unamchoresha tyuu.
Si rahisi kama unavyo sema hata kisheria huruhusiwi kwani itakuwa kama utekaji. Sababu huyo mdada hawezi kujieleza au tuseme hawezi kuridhia kitu. Ndiyo maana amesema wahuni 'wanajisevia', jambo jingine ni kosa kumuhifadhi mtu ambaye ni dangerous to the public. Pia hujui status ya ukaaji wake I mean visa nk. Pia huko ulaya na America sehemu ya kuishi ni wewe tu na familia yako. Hakuna Eti utalala sebuleni kwenye coach.
 
Tunaobakia Tanzania na kupambana na Hali zetu ( Shida ) huku tukisoma katika Vyuo Vikuu vyetu na Kula Maharage, Tembele na Dagaa huwa tunachekwa na kudharaulika mno na wale ambao huona Ulaya / Marekani ndiyo Pepo na Suluhu yao ya Maisha na Taaluma. Kudadadeki apambane na hali yake kama nasi tunavyopambana na hali zetu huku Madongo Kuinama Afrika.
 
Hii imfikie SSH , mbona huwa anaenda US mara kwa mara. Anaweza kufanya jambo kupitia balozi wake wa US
 
Yani unachojua wewe ni kuandika kiswahili fasaha tu. Mengine 🚮🚮🚮
 
Kuwe na accountability kwa mabalozi wetu hii ni moja ya kazi zao raisi awawajibishe mabalozi wazembe kama huyu wa marekani
Ili mtu usaidiwe ukiwa huko nje ya nchi ni jukumu lako mhusika ujitambulishe pasipo shaka kuwa wewe ni Mtanzania. Sasa huyo Dada ni Kichaa, jee anavyo vitambulisho vyake? Na msaada mkubwa kwa balozi zetu huko nje ni kukupatia emergency travel document tu wala hata nauli hawatoi kisingizio kuwa hawana fungu hilo.
 
Mimi naona km mtoa mada alichokosea ni kusema kinachomkutaga. walau angesema anaface ukatili but asiseme ni ukatili gani.
 
Eti msaada wa hela ambao hauhitaji!!!? Mgonjwa wa akili anajua anachohitaji? Jamaa kamtendea fadhili sana huyu dada.
Haya mambo ufanyiwe wewe harafu miaka kadhaa unarudi kawaida unajikuta mitandaoni kwamba ulikuwa unalala madarajani na unalawitiwa na wajinga kama mleta uzi ,unajisikiaje
 
Mtu kichaa atajitambulisha vipi, kama balozi kapelekewa taarifa na mleta mada hadi leo hajachukua hatua yoyote, na hapo ndipo tatizo lilipo kazi ya balozi sio tu kukupa emergency travel document it goes beyond that
Balozi ni kama nchi ndogo ndani ya nchi ,ni kufuatilia maslahi ya tanzania na watanzania ndani ya nchi husika, siyo kuvimbisha vitambi tu
 
Ndugu hapa ndio umefikiri mpaka mwisho au tusubiri mengine? Nadhani haujafikiri sawasawa. Rudia kusoma ulichoandika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…