Iyerdoi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2012
- 2,717
- 3,895
Ni sahihi Mkuu. Labda tumwombe mleta dokezo ajitolee tuu(Mungu atakulipa) atupatie Taarifa zake in details:Ni mwaka wa saba (7) sasa tangu hili tangazo lilipo tolewa kwa mara ya kwanza.
Anyways, tuombe ndugu zake wapatikane mkuu, maana huko US hata rafiki hawezi akawa radhi kumuhifadhi mtu alie na shida ya akili.
1. Majina yake kikamilifu: Jina la kwanza, jina la kati na Surname(Ukoo)
2. Anatoka sehemu gani ya Tz: Mkoa, Wilaya, Kijiji
3. Shule aliyokuwa anasoma au kazi aliyokuwa ameajiriwa na ni Wizara gani, Halmashauri ya Wilaya gani, au Taasisi (Serikali au Binafsi) au Shirika gani hapa Tz.
4. Majina ya next of kin au mtu yeyote ambayo huyo binti kama anaweza kumkumbuka.
5. Hapo USA alipokelewa wapi na nani e.g. Chuo au alifikia kwa nani eg. Sponsor n.k.
6. Kama inawezekana, zifuatiliwe Taarifa zake za usafiri alipotoka Tz hadi kufikia Marekani (Najua hapo kuna usumbufu mkubwa lakini basi iwe ni mtu kujitoa sadaka)
7. Waombwe ubalozi wa Marekani hapa Tz kama wanaweza kutoa Taarifa ya mawasiliano ya mwisho na dada huyo kabla hajaondoka kwenda USA kwani huwa ni lazima ubalozi wa nchi husika unakoenda ujue ni nani anayekwenda nchini kwao na sababu za kwenda huko i.e. kwenda nchini USA.
Niwaombe mods wajaribu kumdokeza balozi wa Marekani aliyewatembelea Juzi-kati hapo - labda inawezekana kupata njia ya kumnusuru huyo binti.
Mwisho: Asante kwa kusoma maoni yangu haya mareeeefu ila nashukuru.

