DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ni mwaka wa saba (7) sasa tangu hili tangazo lilipo tolewa kwa mara ya kwanza.
Anyways, tuombe ndugu zake wapatikane mkuu, maana huko US hata rafiki hawezi akawa radhi kumuhifadhi mtu alie na shida ya akili.
Ni sahihi Mkuu. Labda tumwombe mleta dokezo ajitolee tuu(Mungu atakulipa) atupatie Taarifa zake in details:
1. Majina yake kikamilifu: Jina la kwanza, jina la kati na Surname(Ukoo)
2. Anatoka sehemu gani ya Tz: Mkoa, Wilaya, Kijiji
3. Shule aliyokuwa anasoma au kazi aliyokuwa ameajiriwa na ni Wizara gani, Halmashauri ya Wilaya gani, au Taasisi (Serikali au Binafsi) au Shirika gani hapa Tz.
4. Majina ya next of kin au mtu yeyote ambayo huyo binti kama anaweza kumkumbuka.
5. Hapo USA alipokelewa wapi na nani e.g. Chuo au alifikia kwa nani eg. Sponsor n.k.
6. Kama inawezekana, zifuatiliwe Taarifa zake za usafiri alipotoka Tz hadi kufikia Marekani (Najua hapo kuna usumbufu mkubwa lakini basi iwe ni mtu kujitoa sadaka)
7. Waombwe ubalozi wa Marekani hapa Tz kama wanaweza kutoa Taarifa ya mawasiliano ya mwisho na dada huyo kabla hajaondoka kwenda USA kwani huwa ni lazima ubalozi wa nchi husika unakoenda ujue ni nani anayekwenda nchini kwao na sababu za kwenda huko i.e. kwenda nchini USA.
Niwaombe mods wajaribu kumdokeza balozi wa Marekani aliyewatembelea Juzi-kati hapo - labda inawezekana kupata njia ya kumnusuru huyo binti.
Mwisho: Asante kwa kusoma maoni yangu haya mareeeefu ila nashukuru.
 
Unatakiwa kuelewa mipaka yako na kuheshimu privacy ya mtu.

Kwanza umeenda kumrekodi bila ya ridhaa yake, unalazimisha kumpa msaada wa hela ambao auhitaji; halafu unamposti mitandaoni huo ni udhalilishaji.

Pili unalazimisha msaada kwa mtu ambae ajakuomba na hataki hiyo ni kuingilia rights zake. Dada anaonekana ni mzima maana unakiri umewahi kuongea nae na hata hapo kwenye video inaonekana anajielewa huo uchizi unampa wewe.

Tatu hujui changamoto zake za maisha hadi kua homeless, ungeanzia kudadisi hapo kimetokea nini kwenye maisha yake hadi kufikia alipofika.

Nne kama lengo ni kutaka ndugu zake wapate habari ungeweza anzisha mada kwa title yoyote na ku-crop sura yake tu na kuomba msaada kama kuna mtu anamfahamu huyo dada wakupe details za ndugu zake uwape taarifa, wao ndio wana mamlaka ya kwenda serikalini na kuomba msaada arudishwe.

Umemkosea sana huyo dada na kumdhalilisha.

Ni rahisi sana kwako kuja na hoja ya privacy, na kwenda mbali zaidi kwa kumuona anaonekana hana matatizo ya akili kwasababu humjui huyo dada wala hujaona maisha anayoishi

Tujitahidini sana kuangalia nia ya muhusika kufanya hivi kuliko kukimbilia kutafuta perfection
Angalia amefanya juhudi gani kabla hajaja kupost hapa JF
Inaonekana mleta hoja amefikia mahali sasa anaona ajaribu platforms nyingine kujaribu kusidia..... sio watu wote wana moyo huo mkuu
 
Tunaobakia Tanzania na kupambana na Hali zetu ( Shida ) huku tukisoma katika Vyuo Vikuu vyetu na Kula Maharage, Tembele na Dagaa huwa tunachekwa na kudharaulika mno na wale ambao huona Ulaya / Marekani ndiyo Pepo na Suluhu yao ya Maisha na Taaluma. Kudadadeki apambane na hali yake kama nasi tunavyopambana na hali zetu huku Madongo Kuinama Afrika.
Mtani, mbona umekuwa mkali hivyo? Humuonei huruma Mtanzania mwenzio who knows huenda AKAWA dadako toka Busegwe.
 
Ubalozi wetu wana habari ushahidi ninao kunasiku Rais wetu atakuja hapa marekani lazima ajue hili najua kukutana naye hapa marekani nirahisi sana Mimi sitanyamaza nataka mtu anichukulie hatua kwa kutaka kuokoa maisha ya huyu dada
Naam. Excellent. Shikilia hapo-hapo. Lobbying and Advocacy. Ikiwezekana hata kuwamobilise waTz walio na uchungu na mwenzetu huyo Mtz anayedhalilika kana kwamba hana kwao, kuandamana mbele ya Mh. Rais na kuwasilisha Hoja tena iwe ni kwa lugha ya Kiswahili.:HYPERCLAPHD:
 
Kwandi,bila ndugu, hawezi kusaidiwa? Serikali zote yale yale. Angekuwa anatuma pesa nyumbani,angekumbukwa. Ila kwa vile fuse zimechomoka,ndo basi. Wangelipa uzito,si siku kadhaa anasafilishwa na kupelekwa hospital zinazowashughulikia,wakati watu wake wa karibu wakitafutwa?
Uongozi wa chuo, Dean of students ulipaswa kutoa taarifa kwa ndugu zake kwa maana wanazo particular za wanafunzi wao
 
Katika vitu ambavyo vinaumiza wengi ni huu ugonjwa, Marekani kuna wataalam zaidi luliko huku, nadhani akipatiwa msaada akiwa huko itakuwa bora zaidi kuliko akija huku.

Kuna vitu vingi vinasababisha mtu kuingia kwenye hili tatizo so kila mtu anaweza akapata ni kuomba tu Mungu atusaidie.

Hongera sana kwa juhudi zako za kumsaidia mtanzania, umefanya jambo jema la thawabu
 
Hizi ndio akili kama za ubalozi wetu USA

Hivi akimchukua halafu usiku ukute kamchinja mwano itakuaje? Si mtaanza kulaumu tena kwamba kanini unamuona mtu ana shida ya akili na unamuhifadhi kwako?
Why risk wakati kuna watu wameajiriwa wanalipwa na wana bajeti ya mambo yote hayo?

Mara nyingi mtu akifanya jambo jitahidi kuangalia nia yake badala ya kukimbilia kutafuta ubaya
Mwanzo nilikua najiuliza inawezekanaje mtu akachapwa vibao hadharani lakini Sasa Ndio napata majibu huyu dada kunasikunilimkuta na Hali ambayo haifai hata kuandika au kumuelezea mtu nadhani ningempiga picha siku hiyo navkumpost Ndio ingekua kumdhalilisha Ila nilijitahidi nikamtafutia namna ya kusitiri mimi nilichukua hiyo video na picha sioni tatizo lolote labda kosa langu nikutaka watanzania na ndugu wajue ukweli wa mwenzetu
 
Uongozi wa chuo, Dean of students ulipaswa kutoa taarifa kwa ndugu zake kwa maana wanazo particular za wanafunzi wao
Tujitahidi kuandika kiswshili tueleweke kwa hiyo Leo Kama umeacha chuo hata hapo bongo uongozi wa chuo utatafuta ndugu zako kuwaambia umecha chuo? Tukikaa kimya itasaidia huyu dada kupata msaada tunajaza comment zisizo na tija hapa
 
Ndiyo km hamsaidii kwa chochote, aache kumtangaza, anamchoresha dada was watu, mxxiiiiieeeeew.
No; hajamchoresha. Kwa mawazo yako labda, hebu pendekeza kwa mfano angemsaidia kwa chochote kama kipi?
Haja mtangaza kwa nia mbaya kama ww unavyolichukulia suala hili.
Labda nikuulize; Je, ukienda Hospitali halafu katika mojawapo ya hatua za uchunguzi ukaambiwa uvue nguo utasema "sitaki mnanidhalilisha" ? au wakakuchoma sindano utasema nurse ni makatili wanakuumiza?
Nikuombe tu mkuu hebu ujaribu kujiweka kwenye nafasi ya huyo dada ambaye ni mgonjwa wa Akili. i.e.Reasoning ability yake haiko sawa e.g. linganisha na akili ya mtoto mdogo. Anahitaji msaada hata kama hajasema. Ww mwenye akili timamu tafadhali inakupasa ufanye kitu.. Je, huko anavyoishi na wanachomfanyia wanaume vibaka wa Marekani, kwako ni sawa tuu sio kitu kiovu aisee? Mbona unakuwa kana kwamba na ww ni mmojawapo wa watu makatili wasio na huruma?
 
Mkuu asante kwa taarifa nadhani ndugu zake wanaeza kupata habari!ila huko US si kuna vituo vya kutunza hawa watu!i think ni busara ukampeleka huko ktk vituo ili apate matibabu huku ndugu wakisubiriwa!si serikali ya US ndo inawatunza au hali ikoje huko.
Hiyo ni kazi ya Social Security Administration na Police Ndiyo wenye dhamana au jukumu la kumtoa hapo Huyo dada na kumpeleka either, mental health facilities au hospital. Wewe kama wewe huwezi.
 
Katika vitu ambavyo vinaumiza wengi ni huu ugonjwa, Marekani kuna wataalam zaidi luliko huku, nadhani akipatiwa msaada akiwa huko itakuwa bora zaidi kuliko akija huku.

Kuna vitu vingi vinasababisha mtu kuingia kwenye hili tatizo so kila mtu anaweza akapata ni kuomba tu Mungu atusaidie.

Hongera sana kwa juhudi zako za kumsaidia mtanzania, umefanya jambo jema la thawabu
Nikweli huku kuna msaada zaidi wa kimatibabu lakini hapo ndipo swala na ndugu au serekali linapo hitajika vichaa hapa marekani niwengi sana lakini wengi wao ni ma dawa ya kulevya au uhuni uliopitiliza lakini huyu dada huwezijua nini kinamsibu vichaa wa madawa wakua kwenye magurupu lakini huyu anaishi porini mwenyewe zaidi ya kusubiri usiku kwenda kwenye majalala kuokota vyakula
 
No; hajamchoresha. Kwa mawazo yako labda, hebu pendekeza kwa mfano angemsaidia kwa chochote kama kipi?
Haja mtangaza kwa nia mbaya kama ww unavyolichukulia suala hili.
Labda nikuulize; Je, ukienda Hospitali halafu katika mojawapo ya hatua za uchunguzi ukaambiwa uvue nguo utasema "sitaki mnanidhalilisha" ? au wakakuchoma sindano utasema nurse ni makatili wanakuumiza?
Nikuombe tu mkuu hebu ujaribu kujiweka kwenye nafasi ya huyo dada ambaye ni mgonjwa wa Akili. i.e.Reasoning ability yake haiko sawa e.g. linganisha na akili ya mtoto mdogo. Anahitaji msaada hata kama hajasema. Ww mwenye akili timamu tafadhali inakupasa ufanye kitu.. Je, huko anavyoishi na wanachomfanyia wanaume vibaka wa Marekani, kwako ni sawa tuu sio kitu kiovu aisee? Mbona unakuwa kana kwamba na ww ni mmojawapo wa watu makatili wasio na huruma?
Huyo sio katili nayeye ni mgonjwa wa akili angekua timamu asinge sema hivyo sio vichaa wote wsishio maporini wengine wako majumbani Kama huyo
 
Nikweli huku kuna msaada zaidi wa kimatibabu lakini hapo ndipo swala na ndugu au serekali linapo hitajika vichaa hapa marekani niwengi sana lakini wengi wao ni ma dawa ya kulevya au uhuni uliopitiliza lakini huyu dada huwezijua nini kinamsibu vichaa wa madawa wakua kwenye magurupu lakini huyu anaishi porini mwenyewe zaidi ya kusubiri usiku kwenda kwenye majalala kuokota vyakula
Ikitokea nimekuja huko nitakutafuta, natamani sana kumuona ili niweze kumsaidia. Sipendi kuona watu wanapitia mambo magumu kama hivyo, nina experience ya kutosha kwenye hili tatizo so ninapoona mtu anapitia kitu ninachokijua na kimenipitisha kwa namna fulani roho inaniuma sana na watu wa hv wanakuwaga smart sana upstairs
 
Sasa si ndo wee umsaidie hapo kwa kumuhifadhi na nk, huku ukisubiri ndugu zake wajitokezee.

Kumuacha ahangaike na huku unamtangaza, si unamchoresha tyuu.
Kwa hiyo wewe na ubalozi wa Tanzania hapa marekani Nani anajua? Soma email ya balozi wa marekani anadai picha nilizo tuma hazikutosha wewe unasema nimemzalilisha jitafakari kwanza ikiwekekana futa huo ujinga wako nitaweka picha na video zakutosha mpka hata rais azione Tena hata zikiwa mbaya nitaomba ziwekwe Ila zifunikwe Ila ubalozi uchukue hatua haraka kabla huyu dada hajakutwa na umauti
 
Unafkiri bila kufanya hivyo watu wangeamini hilo analolisema....
And unapataje lidhaa kwa mtu mwenye matatizo ya akili tena uliyokuwa neglected.
Umejuaje ana matatizo ya akili?

Kama anadhani ana matatizo ya akili kwanini asipige simu ‘mental health unit’ wamchukue bure kwa matibabu aihitaji kudhalilishwa.

Hii ndio shida yetu watanzania mtu akianza na leading statement we automatically take that viewpoint as undisputed fact, wakati mleta mada hajui ata jina la ubini wa huyo dada wala background story yake zaidi ya kutengeneza narrative yake based on is own interpretation of her situation.
 
Ikitokea nimekuja huko nitakutafuta, natamani sana kumuona ili niweze kumsaidia. Sipendi kuona watu wanapitia mambo magumu kama hivyo, nina experience ya kutosha kwenye hili tatizo so ninapoona mtu anapitia kitu ninachokijua na kimenipitisha kwa namna fulani roho inaniuma sana na watu wa hv wanakuwaga smart sana upstairs
Karibu sana huyu anatakiwa ubalozi umsaidie haraka sana hao Ndio kazi Yao
 
Back
Top Bottom