Mtanzania Khalifa Siwa Afariki New York, Ubalozi Watafuta Ndugu Zake

Mtanzania Khalifa Siwa Afariki New York, Ubalozi Watafuta Ndugu Zake

Mwamba umekuja ki Katuga Katuga sana, sasa waambie waheshimiwa majaji kwamba ni jukumu la Kiranga kuzingatia dhima ya huu uzi.

Na Je, una uhakika hajatoa taarifa za kina kwa vyombo husika ikijumuisha ubalozi wa Tanzania USA? Kumbuka yeye anaishi huko na ameeleza jinsi alivyomfaham.

Kwa dhima ya huu uzi, kuna mawasiliano yamewekwa hapo kwa yeyote mwenye taarifa awasilishe huko.
Kuna mengine tunawasiliana jumuiya ya Watanzania NY/NJ, ubalozi, na familia Tanzania

Siwezi ku pre empt wasemaji wa familia.
 
Khalifa alikuwa mtu fulani wa stories sana. Halafu mtu fulani mwenye sura tofautitofauti ambazo usipokuwa makini kumsoma, angeweza kukushangaza.

Siku moja anakuelezea viwanja (clubs) tofautitofauti hata usivyovijua vya New York City, akikupitisha kona zote na habari zake za ndani kabisa kama mtu aliyeujua mji vizuri kwa miaka mingi, halafu ukianza kufikiri huyu ni mtu wa maisha ya kuponda maraha New York City tu, unamkuta anaongelea mambo ya trading na investment kama trader wa floor ya New York Stock Exchange, na sio kuongelea tu, anakuambia kuhusu trades anazofanya.

Kuna siku alinihoji sana kuhusu kazi zangu Wall St., akaingia so deep kwenye mambo ya trading na jinsi quantitative easing inavyoingilia uchumi, kiasi nikajistukia kuwa huyu jamaa si wa kumchukulia poa kama nilivyodhania awali.

Alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kufanya mazungumzo, kwa namna ambayo yanaweza kuwa na masihara halafu masihara yakizidi, atakurudisha kwenye maswali ya msingi, kwa namna ambayo hata anapokupinga, ubishi wake unakuwa wa kirafiki sana, kitu ambacho watu wengine wa New York City / Jersey City, hawakuweza, kwa kuwa na ego, ubishi wao unakuwa na muhuri wa shari za mji huu usiolala.

Khalifa alikuwa mtu wa matumaini, mtu wa cheko muda wote, mtu wa kujishusha - ila si kuwa doormat- kiasi wasiomjua vizuri wangeweza kirahisi kukosea kukisia daraja lake la maisha kwa kumfikiri mtwana.

Alikuwa mtu wa matani sana na kuweza kuunganisha vizuri u Marekani na Utanzania wake. Wengi huzidisha u Tanzania sana, au u Marekani sana, Khalifa aliweza ku balance vizuri sana identities mbili hizi. Sijawahi kumuona amekasirika.

Ukimkuta leo kapiga vitu vya Kinyamwezi kama mtoto wa Harlem au Brooklyn, kesho usishangae ukimkuta kapiga bonge la kanzu kama Shehe wa Msikiti wa Tambaza, anatembea barabarani.

Alikuwa mtu aliyependa maisha na starehe, lakini pia aliyependa kujumuika na watu, na kufanya kazi sana ili kuyapata hayo maisha mazuri. Na mara nyingi kwenye starehe hukohuko mko naye, kumbe mwenzenu anafanya kazi zake pia.

Alikuwa na uwazi fulani ambao binafsi niliupenda, a mix between, on one hand, a New Yorker's "call it as it is, no beating around the bush" attitude, and on another hand, a down home Tanzanian sensibility, a respect for savoir faire.

A type of person with a talent for reading people and rooms, who would immediately know who is who, in a "real recognize real" fashion. An invaluable asset in the New York City circles where you meet all kinds of people, from blueblood billionaires to fresh off the boat paupers.

Never without a story to relate, always a street diplomat to mediate friendly squabbles without enabling any bullshit, he walked the fine line.

An effortless comedian who provocatively challenged Tanzanian norms in a humorous and likable way.

It was like yesterday, the Jersey City parties, the stories, the aspirations, the banter.

He will be missed.

Innalillah wa inna illahi Raji'uun.
Pole sana Mzee.
Momento mori
 
Filmography.


As Bob (Khalifa Siwa) tells his family that he is in a relationship with Monica (Raquel Heslop), his father tries to persuade him to leave her. His friends, mother, sister and brothers do not know what to do to help him out of this drama. Likewise, Monica faces the same challenge. As Monica informs her family about her engagement with Bob, her father doesn't like this relationship because Bob comes from another culture.

Will Monica listen to her family and break up her engagement with Bob? Will Bob's father accept a daughter-in-law from another culture? "Cultural Wars" narrates a dramatic love story in the City of New York. It is a Deogratius Joseph Mhella's first feature film.

Deogratius learned pre- and post- film production in Rome, Italy and he is now entering the American market for the first time. Deogratius's movies focus on African, European and African American issues.
 
Database itasaidia nini kama mtu hataki kuwa registered? Mpaka unaona huyo mtu hana ndugu wala jamaa ujue ndo maisha aliyoamua kuishi hata wite kanzudata asingejisajili.
Ubalozi wetu unakosa coordination ndogo tu na jumuiya.

Khalifa si mtu ambaye hajulikani na ndugu zake hawawezi kupatikana.

Hapo ubalozini kuna watu wanamjua. Yani watu wa ubalozini wengine wanatoka kwenye jumuiya. Nashangaa wameshindwa vipi kuwasiliana na watu wa jumuiya kupata contacts zote.

Ni kama vile wameandika hii taarifa mara baada ya kufahamishwa na Wamarekani, kabla ya kuwasiliana na jumuiya.

Khalifa alikuwa mtu wa watu si mtu tu ambaye hajulikani katika jumuiya, hata hapo ubalozini kuna watu wanamjua.

He is a Siwa, si mtu ambaye ndugu zake hawawezi kupatikana.

Wakati wa nyuma kidogo, jambo kama hili lisingeweza kutokea. Tulikuwa na mtandao mzuri kati ya viongozi wa jumuiya zetu na ubalozi.

Kama ubalozi unapata taarifa kama hii kibusara ungewasiliana na viongozi wa jumuiya husika.

Marehemu ni kati ya wanajumuiya wetu maarufu. Kusingekuwa na shida hata kidogo kupata taarifa zake na za familia yake.

Sasa hivi habari ilivyowekwa ni kama vile mtu kaokotwa haijulikani hata ubalozi utaanzia wapi kupata habari za ndugu zake.

Ndiyo maana watu wasioelewa wanapata taharuki kuona habari za ndugu zake zinapatikana.

Ndugu wanajulikana, wametaarifiwa, wanapanga mipango ya mazishi.

Ubalozi ulikosa coordination ndogo tu na jumuiya.
 
Back
Top Bottom