TANZIA Mtanzania Mansoor Daya Afariki Dunia, alianzisha kiwanda cha kwanza cha Madawa Afrika Mashariki 1962

TANZIA Mtanzania Mansoor Daya Afariki Dunia, alianzisha kiwanda cha kwanza cha Madawa Afrika Mashariki 1962


Mtanzania Mansoor Daya amefariki dunia jijini Dar es Salaam. Daya alikuwa mtu wa kwanza nchini kufungua kiwanda cha madawa Tanzania na Afrika Mashariki mwaka 1962 akianza kwa kuziuzia nchi jirani na baadae akaanza kuuza kwenye soko la ndani.

Mpaka anafariki dunia alikuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya 'Mansoor Daya Chemicals Limited. Kiwanda chake kimekuwa kinazalisha madawa kwa miaka 60 na sasa kina uwezo wa kuzalisha tembe milioni 3 kwa shift moja.

Wateja wake wakubwa ni MSD, mahospitali na cliniki mbalimbali Tanzania na kinachagiza juhudi za kufikia mpango wa Serikali kuhakikisha Tanzania inaagiza chini ya 50% ya dawa zote zinazotumika nchini kufikia mwaka 2030.
Inna li Llahi wa inna Ilayhi rajiun.
 
Halafu anakuja mtu anasema eti viwanda binafsi vilikuwa vinakatazwa halafu leo hii vinaruhusiwa ukiwauliza kuna viwanda vingapi sijui watakujibu nini?

RIP Mdau Mwananchi Mjenga Nchi.......
 
Ushawahi kumsikia mtu mmoja anaitwa Azim Premji? Nina imani unamjua Jenerali Ulimwengu,hawa walizaliwa hapahapa Tanzania mmoja kazaliwa Dodoma na mwingine kazaliwa Kagera walizaliwa miaka mingi tu iliyopita kabla uhuru yaani walikuwepo kwa zaidi ya hiyo miaka 5 unayosema lakini kufika miaka ya 1990's ilibainika sio Watanzania na ikabidi waombe uraia wa Tanzania.
Jirekebishe!
 
Namkumbuka sana, bidhaa nyingi sana za dawa zilikuwa zimeandikwa Mansour Daya.

Ila mbona taarifa ya kifo ni kama ya siku tatu nyuma wewe umeileta leo.
 
Nyerere alikuwa anataifisha mali za weusi wenzake tu kwa kisingizio cha ujamaa
Sema huyo Mhindi sijui alisalimika vipi lakini Nyerere hao wahindi ndiyo aliwakomesha kweli kwa uchache tu pale Buguruni kwa Bakhressa kiwanda kilikuwa cha Mhindi.

Halafu kiwanda cha mabati kilikuwa cha Mhindi na Maghorofa yote yale ya kizamani kuanzia Kariakoo, Upanga na Kisutu kote alitaifisha zilikuwa za Wahindi.
 
Back
Top Bottom